gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 759
- 1,250
Anaitwa Maria Ngoda, mkazi wa mtaa wa Zizi la Ng'ombe, Iringa. Siku ya tukio alikutwa karibu na makazi yake na ndoo iliyosadikika kuwa na vipande 12 vya nyama. Baada ya utambuzi, vikabainika ni nyama ya Swala.
Nyama hiyo, imetajwa kuwa na thamani ya TZS 900,000. Maria akajitetea akasema hakujua kama nyama hiyo ni ya Swala, pia sio yake alikabidhiwa na kijana anaitwa FUTE ili auze. Maria anasema, ndoo ilikuwa na vipande 13, Fute akaondoka na kimoja.
Baada ya hilo, uongozi wa Mtaa ukaongozana na Maria mpaka nyumbani kwa ndugu Fute. Lakini, kabla ya lolote kujadiliwa, uongozi huo UKAMLAZIMISHA Maria ajitwike ndoo hiyo kichwani na safari ikaanza kuelekea kituo cha polisi. Maria akawekwa chini ya ulinzi. Fute hakuguswa, akabaki kuwa mtu huru.
Jalada la mashtaka likafunguliwa, kesi ikafika kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa. Tangu kesi inaanza mpaka kumalizika kwake, Maria hakuwa na mwakilishi (WAKILI). Maria AKAKIRI kukutwa na nyama hiyo, lakini akagoma kuwa yeye sio MMILIKI. Baada ya utetezi huo, na kesi kufungwa, upande wa DPP ukaoimba mahakama kutoa ADHABU KALI ili iwe fundisho kwa wengine. Ndipo Hakimu Mkazi Mkuu wa Iringa, siku ya tarehe 3 Novemba 2023, akamuhukumu Maria kifungo cha miaka 22 gerezani.
JE, SHERIA INASEMAJE!
Maria amehukumiwa chini ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 (The Wildlife Conservation Act, 2009, R.E 2022) kifungu cha 86(1),(2),(c), sambamba na Sheria ya Uhujumu Uchumi, SURA 200, kifungu vya 57(1) ukisoma sambamba na Aya 14 ya Jedwali la kwanza (First Schedule) na kifungu 60(1) na (2) vinavyotaja adhabu ya miaka isiyopungua 20 lakini isiyozidi 30 mtuhumiwa anapokutwa na hatia.
Sheria hii inakataza kuua, kuuza au kukutwa na nyama ya mnyamapori pasipo KIBALI, na wanyama hao wameorodheshwa kwenye sheria ya Wanyamapori kwenye Jedwali la Kwanza, Sehemu ya Kwanza.
MJADALA NA UDHAIFU WA KESI:
Wengi, ikiwemo na mimi tunaamini huyu mama hakutendewa haki kwa sababu hakuwa na mwakilishi (Wakili). Upande wa DPP ulitumia UDHAIFU huo ili kutimiza lengo la kumfunga mtuhumiwa. Pia, mahakama japo ya kupewa taarifa kupitia utetezi wa Maria kuna mtu mwingine anaitwa FUTE ndiye MMILIKI wa hiyo nyama, mahakama haikutuma SUMMONS ili Fute aje kutoa ushahidi.
Pia, sheria imetaja aina ya USHAHIDI unaotakiwa uwasilishwe na baadi ya NYARAKA za utambulisho ili mtuhumiwa akutwe na hatia, kitu ambacho Maria asingekuwa na uwezo wa kuzitambua au kuziCHALLENGE. Tukio hili kisheria ni "NEGLIGENCE" au/na "MISCARRIAGE OF JUSTICE".
Katika hatua hii, Maria ana haki ya kukata RUFAA chini ya Katiba ya nchi, ibara 13(6)(a), na ndicho kinaenda kutokea. Binafsi nataka haki itendekee, hata kama ni kufungwa, basi mtuhumiwa afungwe baada ya KUSIKILIZWA KWA UKAMILIFU kama Katiba inavyosema, haki ambayo hakupewa.
Mwisho, kuna haja ya kupitia sheria hizi maana hazitoi haki, na hazina MASLAHI kwa Taifa. Pia, kuna UDHAIFU katika UTEKELEZAJI wa sheria hizi, na wengi wako magerezani kwa sababu ya udhaifu huu. Tangu sheria hii imeanza kutumika, wananchi wengi wameumizwa na wanaendelea kuumizwa na hakuna tija kwa Taifa.