Wanasheria wa Zanzibar wakerwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria wa Zanzibar wakerwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Jun 5, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Posted on June 4, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Rais wa Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Awadh Ali Said akiongea katika sherehe za kuadhimisha siku ya sheria duniani katika bustani ya Victoria

  Wamefanya kitendo hiki kwa lengo la kumuogopesha (intimidate) Wakili Abdulla Juma na labda kuwahadharisha mawakili wengine waache au waogope kuwatetea watuhumiwa wa kesi hizi zinazoendelea na nyenginezo. Mabomu hayo yameathiri sana ofisi na kuifanya kutokalika kwa siku tatu na hadi wakati huu hatujuwi athari za kiafya zilizowakuta mawakili waliokuwemo ndani ya ofisi hiyo. Vitisho na hujma dhidi ya mawakili vina lengo la kudhoofisha ustawi wa utawala wa sheria, haki za binaadamu na utawala bora. Endelea kusoma taarifa hii

  ZanzibarLawSociety
  P.O.BOX 3319, Zanzibar, Tanzania. Bwawani Hotel – Ground Floor, Suite # 107 Tel/Fax +255 24 2234890 begin_of_the_skype_highlighting +255 24 2234890 end_of_the_skype_highlighting Mobile: +255 773 092511 begin_of_the_skype_highlighting +255 773 092511 end_of_the_skype_highlighting Email: zls@zanlink.com
  Our Ref: ZLS/Council/09/2012 30 Mei, 2012
  Kamishna wa Polisi
  Makao Makuu ya Polisi
  Ziwani, Zanzibar
  Kamishna Mussa Ali Mussa,
  KUH: MALALAMIKO YA CHAMA CHA WANASHERIA ZANZIBAR KWA KITENDO CHA POLISI KUPIGA MABOMU OFISI YA WAKILI
  Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), kwa masikitiko makubwa, kinaomba kuwasilisha kwako malalamiko yetu kufuatia kitendo cha Polisi kupiga mabomu ofisi ya wakili ya AJM Solicitors iliopo Amani, Zanzibar. Jumatatu tarehe 28 Mei 2012 majira ya asubuhi katika Mahkama ya Mwanakwerekwe iliopo nje kidogo ya Manispaa ya Zanzibar, walifikishwa katika mahkama hizo watuhumiwa kadhaa kwa mashtaka mbalimbali yahusuyo uvunjifu wa amani. Hii ilikuja baada ya Jeshi la Polisi kuamua kumchukuwa kutoka msikitini Sheikh Mussa Juma Issa, Imam wa msikiti wa Kwa Biziredi majira ya saa 1.30 usiku wa Jumamosi 26 Mei 2012. Wafuasi wake walimfuata hadi polisi Madema alipowekwa ndani. Baada ya muda kupita na taarifa kuenea ndipo waumini wa dini ya Kiislam walipoanza kumiminika kituo cha Polisi, Madema wakisubiri kujua khatma ya kiongozi wao.
  Watuhumiwa waliokamatwa Jumamosi tarehe 26 Mei na Jumapili tarehe 27 Mei 2012 walifikishwa mahkamani asubuhi ya tarehe 28 Mei 2012. Kama sote tunavyoelewa, ni msingi mkuu wa sheria zetu kwamba mtuhumiwa huwa hana hatia yoyote mpaka pale Mahkama itakapotamka hivyo baada ya kesi kuendeshwa kisheria. Na ni haki ya kikatiba kwa mshtakiwa kupata utetezi wa kisheria kutoka kwa watu wanaotambuliwa na sheria kuwa mawakili. Wakili Abdulla Juma Mohamed wa AJM Solicitors & Advocates Chambers ni wakili wa utetezi katika kesi ya Jinai inayotokana na MAD/PCR/45/2012 ya Mahkama ya Wilaya Mwanakwerekwe (Mhe. Janet Sekihola) na pia kwa kesi nyengine ya Mahkama ya Wilaya Mwanakwerekwe (Mhe. Mohamed Ali) inayotokana na MKD/PCR/05/2012 inayomkabili Mbarouk Said Khalfan na Mussa Juma Issa. Wakati watuhumiwa katika kesi ya kwanza wanashtakiwa kwa uzembe na ukorofi (kif. 181(d) Sheria ya Jinai 6/2004), kesi ya pili ni ya shtaka la mkusanyiko usio halali (kif. 55 na 56 Sheria Nam 6/2004).
  Baada ya kesi tajwa hapo juu kuakhirishwa, Wakili Abdulla Juma aliondoka na kuelekea katika Mahkama ya Ardhi, Vuga Zanzibar. Majira ya saa 6.30 mchana ofisi yake ya uwakili iliopo karibu na Amani Roundabout, ilishambuliwa na Polisi ambao waliingiza mtutu/mitutu ya bunduki ndani ya madirisha na kupiga mabomu ya machozi. Sisi tunaamini kabisa kwamba askari waliofanya hivi wamefanya wakijuwa kabisa kwamba kitendo chao kinakiuka maadili yote ya kazi yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao. Wamefanya kitendo hiki kwa lengo la kumuogopesha (intimidate) Wakili Abdulla Juma na labda kuwahadharisha mawakili wengine waache au waogope kuwatetea watuhumiwa wa kesi hizi zinazoendelea na nyenginezo. Mabomu hayo yameathiri sana ofisi na kuifanya kutokalika kwa siku tatu na hadi wakati huu hatujuwi athari za kiafya zilizowakuta mawakili waliokuwemo ndani ya ofisi hiyo. Vitisho na hujma dhidi ya mawakili vina lengo la kudhoofisha ustawi wa utawala wa sheria, haki za binaadamu na utawala bora.
  ZLS inalaani kwa nguvu zote kitendo cha Polisi cha kupiga mabomu ofisi ya wakili. Tunasema kitendo hiki kinalitoa thamani Jeshi la Polisi na kinaondosha imani ya wananchi kwao na pia kuharibu uhusiano wa karibu unaopaswa kujengwa baina ya raia na jeshi la polisi kupitia dhana ya “Polisi Shirikishi”. Sisi kama maofisa wa mahkama tunasikitishwa sana na hali hii na tunakutaka ufanye uchunguzi na watakaobanika kufanya kitendo hiki wachukuliwe hatua zifaazo. Tunaamini kwamba utendaji kazi wa Polisi hauendi kiholela – kila kikundi kinakuwa chini ya udhibiti na uangalizi wa Jeshi la Polisi kama taasisi. Hivyo hakutakuwa na ugumu wowote kumtambua askari aliefanya uhalifu huo. Vyenginevyo utatujengea imani kwamba kitendo hiki kina baraka zote za Jeshi la Polisi.
  Wako katika kuheshimu Sheria za Nchi,
  ………………………….
  Awadh Ali Said
  Rais, ZLS
  Nakala kwa:
  1. Mhe. Jaji Mkuu, Zanzibar
  2. Mhe. Mwanasheria Mkuu, Zanzibar
  3. Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria, Zanzibar
  4. Mhe. Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Zanzibar
  5. Mhe. Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Zanzibar
  6. Mkurugenzi wa Mashtaka, Zanzibar
  7. Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Tanzania
  8. Rais, Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) – Arusha, Tanzania
  9. Rais, Chama cha Wanasheria wa Uganda
  10. Rais, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika
  11. Mwenyekiti, Chama cha Wanasheria wa Kenya
  12. Mwenyekiti, Chama cha Wanasheria wa Burundi
  13. Mwenyekiti, Chama cha Wanasheria wa Rwanda
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kinajipanga kumburuza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa atashindwa kuwafungulia kesi Polisi walio vamia ofisi ya Mwenzao na kupiga mambomu ndani ya ofisi hio kiholela.

  hii ndio kuvunja haki za kibinadamu kwa kuwazalilicha Wanasheria na wandishi wa habari, wote hawa wana umuhimu mkubwa katika jamii.

  Jee kuna ubaya gani Wakili kuwatetea wateja wake?
   
 3. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huu ndo uanasheria uchwara, iweje mlaani aliyepiga mabomu pekee bila kulaani waliosababisha mabomu yapigwe-upuuzi mtupu na double standard ya hali ya juu. Na je hayo mabomu zanzibar nzima yalipigwa ktk ofisi ya huyo wakili tu au pia yalipigwa kwengineko,if yes ni sababu zipi zilizofanya yapigwe na kwengineko. Je mnajua kuwa mabomu huwa yanapigwa kwa ajili ya kuhami hali ya hatari inayotishia usalama wa taifa? Hivi mauaji ya Pemba na mabomu yake mlimfungulia kesi the then IGP mahita vilee enh! Acheni siasa msiingie huko mtamalizwa madogo-ushauri tu.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Njia pekee ni kuwafungulia polisi mashtaka; vinginevyo huu mchezo wa polisi kufikiri kwa vile wana mabomu wanaweza kufanya lolote kwa raia yoyote utaendelea sana. Tumeona Arusha, tumeona Songea na tayari tulishayaona Zanzibar. ZLS wasiishie kuandika malalamiko waende mahakamani. I support them.
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  MKJJ DOUBLE FACE, sasa jua hata makanisa jamaa walipanga kwa makusudi kubadilisha move ila watu wamewashika pabaya mwaka huu
   
 6. Z

  ZIGZAG Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  polis hawa ndio wachomaji makanisa, polis hawa hawa ndio wanaotengeneza vikaratas vya uunguja na upemba kwa kuondosha zana ya muungano, na kwa vifaa ambavyo tunavilipia kodi sisi wananchi, polis hawa ndio wanaotengenza scandal za kuchoma bar ili zanzibar isusiwe na nchi za magharibi, wachunguzeni askari hawa ndio source ya machafuko. ivi tujiulize ni kwa sababu nchi hii haijatokea vita ndio askari wanatumia nafas ya kutumia silaha zao kwa hamu walizonazo kuwanyanyasa raia?
   
Loading...