Wanasheria wa JF mnasemaje kuhusu Hukumu ya Lema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria wa JF mnasemaje kuhusu Hukumu ya Lema?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by CHUAKACHARA, Apr 5, 2012.

 1. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Wana FJ, hivi ni jaji gani ameisikiliza kesi ya Lema. Nina wasiwasi na majaji wetu watukufu waliomwagwa na JK kama fadhila au kutimiza azma ya kuwepo na majaji wengi/wakutosha bila kuzingatia ukomavu kushika nafasi ya high court judge. Nasema hivyo kwa sababu ukisoma hukumu za majaji hao ukalinganisha reasoning yao katika hukumu zao na reasoning katika hukumu zilizotolewa na Majai wa zamani kama Lugakingira, Mroso, Katiti, Makame, Lubuva etc you will come to a conclusion kuwa kuna tatizo na waheshimiwa wa leo. Just do a sim,eresearch, read some few high court decisions of today's judges and read also those of the retired judges I have mentioned. Nawaheshimu sana Majaji wetu watukufu, lakini.....
   
 2. mwakichi

  mwakichi JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: May 14, 2011
  Messages: 420
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  naomben msaada wa sheria hapa
   
 3. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 180
  Ninavyofahamu kosa la rushwa ndo mtu haruhusiwi, lakini ya kashfa nadhani anaruhusiwa kugombea
   
 4. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  jamani mimi Sheria sijui ila naona kama kuna utata jinsi hii hukumu ilivyotolewa, Je wanasheria wa JF mnasemaje?

  Je Lema sheria inaruhusu kugombea tena au ni kosa gani mtu akifanya haruhusiwi kugombea?

  Magamba bana tabu sana, mpaka ifike 2015, TZ imekuwa jangwa....
   
 5. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naombeni msaada kidogo. Nimejaribu kuuliza hili swali kwa watu kadhaa, lakini sijapata jibu linaloondoa shaka. Je, Ni sheria gani imetumika kumvua Lema ubunge?

  Kuna sehemu nimesoma ambapo wanadai hii ni kesi ya madai (tort). Ivi kweli, kesi ya madai ina nguvu ya kumvua mtu ubunge? Nijuavyo mimi, kesi ya madai hulipwa kwa fidia. Kwa mfano, nimekutukana (defamation), utadai msamaha na fidia ya pesa kadhaa. Je, Ubunge unaweza kuwa ni fidia halali kwenye kesi ya madai?

  Natanguliza shukrani.
   
 6. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nimepatwa na kigugumizi kwa yaliyotokea na yanayo endelea kutokana na hukumu dhidi ya Lema,hivi kulikuwa na haja ya Batilda kuwepo japo mara1 kuhojiwa pale mahakamani?sasa vipi? Naomba wataalam wa sheria wachambue hii hukumu kwa manufaa ya umma.DALILI YA UMWAGAJI WA DAMU ZIMEFIKIA 71%.
   
 7. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Lema anasema kuna mkono wa ikulu! Yani uwezo wa kufikiri yule tulimpangisha ikulu si tu umesimama bali sasa unarudi nyuma kabisa.
   
 8. k

  king86c Senior Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  UKWELI AMBAO HAUPINGIKI maisha ya watanzania ni magumu sana utawala wa sheria unatumiwa vibaya na watu wachache kuweka vimada vyao madarakani bila kuangalia nguvu ya umma iko wapi matumizi mabaya ya sheria ndio yamechukua cmkondo katika kesi ya leo bila kujali haki ya mpiga kura mwananchi ambaye alitunza shahada yake kwa ajili ya kupiga kura kumchagua mtu ambaye anaona atamletea maendeleo.G LEMA MPAKA SASA NASEMA KUWA NI MBUNGE WANGU NILEMCHAGUA NA SIO MIMI TUU WANANCHI WA JIMBO LA ARUSHA ZAIDI YA ELFU 56000 SASA IWAJE leo hii mahakama ambayo inatakiwa kusimamia sheria inapinda sheria ili watu wachache waweze kupata madaraka matusi mangapi tumeshudia kwenye kampeni za uchaguzi ALIYOYASEMA LUSINDE YANAFAHAA KWENYE KIOO CHA JAMII BASI NA YEYE ATOLEWE UBUNGE na wasii wanachadema wenzangu ambao tuko tayari kuleta mabadiliko tulete mabadiliko haya yote yatakwisha na mwaka 2015b ni mwaka wetu wa kuongoza nchi nchi hii imejengwa na misingi ya democrasia sio demokrasia ya cham tawala DR SLAA .FREEMAN MBOWE NA WANACHADEMA TUKO TAYARI KUANZA KAMPENPENI MAPEMA TUNASIKILIZA UONGOZI WA CHAMA PEOPLE POWERS ALUNTA CONTINUA VIVA FOREVER
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sio kesi ya tort. Kavuliwa ubunge chini ya Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 (Tanzania Election Act 1985)

  Sidhani kama kulikuwa na haja Batilda kuwepo. Istoshe sio yeye aliyefungua hiyo kesi.

  NEC itaweza tuu kumwondoa kwenye daftari la wapiga kura na kum-disqualify kupiga au kutopigiwa kura kama mahakama ita-certify kuwa imemwondolea ubunge wake kwa kujihuisha na vitendo vya rushwa or "illegal practice".

  Hapa wapi?
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Pasco no lawyer..alipata upper second UDSM faculty of law. Tumsubiri aje.
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hawafundishi sheria za uchaguzi pale. Inabidi waanze mara moja maana zinaelekea kuwa na soko sasa.
   
 12. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa lipo katika Katiba yetu inayompa Rais mamlaka ya kuhonga vyeo. Wazungu wana msemo wa "anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo" Usemi huu unadhihirika pale Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama kinachotawala anapowazawadia watu mbalimbali vyeo na kuwaapisha ili wafanye kazi kwa utii kwake (Na siyo taifa). Yeye pia ana mamlaka ya kuteua na kutengua, kwa vile usipomfurahisha ana uwezo kikatiba wa kukutema. Hii inafafanua kwa nini ma DC, ma RC wanajitanabaisha na CCM huku wakijinadi ati wao ni watendaji wa serikali! Si tunawaona wanavyohangaika kuwapokea mke na watoto wa Rais kama wajumbe wa serikali? Si tunawaona wanavyovalia mabiramu (Mabango) ya CCM hata katika hadhira zisizo za kichama na kupamba majukwaa kana kwamba Rais anakuja kufanya mkutano na wanachama wake? Kumaliza tatizo hili njia ni moja tu, nayo ni kuondoa vipengele vyote vinavyompa Rais madaraka ya kifalme kama ilivyo sasa.
   
 13. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  kutamka maneno ambayo hayatakiwi kwenye kampeni mpaka kuvuliwa ubunge sio "illegal practice"?
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Well, hakuna specific definition kwenye sheria husika sheria yenyewe inasema tuu it is "illegal practice" kupiga au ku-induce mtu mwingine kupiga kura wakati unajua wewe au huyo mtu haruhusiwi kupiga kura au mmepigwa marufuku kupiga kura, ku-tender invalid voter card ili upewe karatasi ya kupigia kura, ku-publish false information kuwa mgombea fulani amejitoa kwenye uchaguzi kama njia ya kuji-promote mwenyewe kama mgombea na interference with public meeting.

  Lakini naona kama amekutwa na hatia chini ya kanuni, taratibu na Sheria ya Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 ambazo zinakataza mgombea kutoa lugha za matusi, kashfa na kejeli. Katika moja ya hoja zilizombana Lema ni pamoja na ya Lema kuthibitika kutumia kashfa, kejeli na udhalilishaji katika mikutano yake (Inadaiwa ni kauli za Lema kuwa Batilda ni hawara wa mzee wa Monduli na kwamba ana mimba ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa).

  Hoja nyingine iliyokubaliwa ni kauli ya Lema katika mikutano yake akiwataka wananchi kutomchagua Batilda kwa sababu ni mwanamke, ambapo Jaji aliita kauli hiyo kuwa ni ya ubaguzi wa kijinsia. Sheria ya Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 inawataka wagombea "kukataa aina yoyoye ya ubaguzi katika misingi ya jinsia, ukabila, dini au rangi."

  Bora zaidi ni kuipata hukumu yenyewe.
   
 15. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Sasa mbona ulituambia amevuliwa ubunge kwa kuvunja sheria ya uchaguzi ya 1985?

  Kingine, kama "illegal practice" haiko specific, basi hatujui kama alichofanya Lema ni illegal practice ama hapana.

  Na tatu, "Sheria ya Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2010" inaitwaje kwa jina lake rasmi la Kiingereza?
   
 16. bht

  bht JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  EMT na Anhauser sheria ya 2010 sio inayohusu gharama za uchaguzi?
   
 17. M

  Majamba Jr Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sheria ya uchaguzi ndo imetumika. Buy ur time tafuta hiyo sheria then isome kwa kina utaona kifungu ambacho kinasema mbunge atavuliwa ubunge iwapo mahakama yenye mamlaka ya kuckiliza kesi hiyo imejiridhisha kuwa mbunge husika alijihusisha na mkosa anayoshitakiwa. Kesi ya Lema haikuwa ya madai wala ya daawa isipokuwa ilikuwa Ellection case.@Chapakazi
   
 18. M

  Majamba Jr Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuona udhaifu wa hukumu kwa report za magazetini.Mimi nadhani kwanza tupate Copy of the Orignal Judgement then tuisome halafu tutaona mapungufu if any na hapo ndo Wanasheria wa JF tunaweza sema tunaionaje hyo hukumu.@Chuakachara
   
 19. P

  Prince edu Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! Ur rily great thnker,lakin kwa vile ninavyojua mimi m2 aliyetukana au kutoa maneno ya kashfa humlipa 2 fidia aliyem2kana,au vp hapo?
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sheria ya Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 ni regulations tuu ambazo zimetengezwa na Tume ya Uchaguzi chini ya kifungu cha 124A cha Sheria ya uchaguzi ya Mwaka 1985. Kifungu hicho kinaipa mamlaka NEC kuandaa maadili ya uchaguzi baada ya kushauriana vyama vya siasa na serikali. Kwa hiyo, hayo maadili ni sehemu ya sheria ya uchaguzi. Both sheria ya uchaguzi na hayo Maadili ya uchaguzi vitakuwa vimetumika kwenye kesi ya Lema.

  Kuhusu whether or not alichofanya Lema ni "illegal practice" ni mpaka kusoma hukumu yenyewe kujua kama kulikuwa na allegation kama hiyo in the first place and how the judge addressed it.

  Sina nakala ya Kiingereza ya hizo regulations. Ninayo nakala Kiswahili tuu. Official title ni "Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2010".
   
Loading...