Wanasheria fafanueni matamshi ya Mh. Waziri Kairuki

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,417
1,839
Matamshi ya Mh. Waziri Angela Kairuki yamenichanganya mimi na naamini Watanzania wengi pia wameshituka. Ni kweli Katiba yetu inasema ili mtu awe kiongozi wa kisiasa analazimika tu kujua kusoma na kuandika lugha ya taifa. Kama ndivyo, mbona kuna mtu aliyekuwa mbunge wa kuchaguliwa lakini ubunge wake ukateuliwa na mahakama kwa sababu alighushi (alifoji) wasifu wake kuhusu kisomo chake?

Katiba hiyo hiyo aliyonukuu waziri si ndio ilitumika kutunga sheria iliyomng'oa huyo mbunge? Nadhani jina lake lilikuwa 'Kihiyo' na ndio maana tumewahi kusikia watu wanamwita mtu asiyesoma 'Kihiyo' Kosa lililowafanya hao watu wafukuzwe kazi sio kuwa na elimu ndogo bali kufoji vyeti vinavyoonyesha wana elimu kubwa.

Je, katika kuonyesha kwamba mwanasiasa anajua kusoma na kuandika haulizwi cheti hata cha darasa la nne? Na kama atatoa cheti cha darasa la nne ambacho amekifoji hatakuwa na kosa kisheria? Kama atakuwa na kosa kwa nini vyeti vya wanasiasa wote visichunguzwe ili hata kama kuna aliyefoji cheti cha darasa la nane afukuzwe? Na je, hao wanasiasa si wanalipwa na pesa za serikali? Kwa nini vyeti vyao navyo visichunguzwe ili wasiwe wanakula mshahara wasiostahili?
 
Natamani wapinzani wakinukishe bungeni kudai wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nao pia wawemo kwenye uhakiki. Ila kwa kuwa bunge limejaa wachumia tumbo wa ******** ndio basi tena
 
 

Attachments

  • FB_IMG_14934440338926181.jpg
    FB_IMG_14934440338926181.jpg
    109.6 KB · Views: 45
Back
Top Bottom