Wanasayansi wa hypersonic wafungwa 🤣

Hiyo habari nilisoma mchana hao wanasayansi hawajafungwa kisa walichotengeneza, tena nilidhani labda wametoa siri. Kumbe wamefungwa sababu walishiriki makongamano ya kimataifa ya hypersonic missile technology, vile vitu vya kufanya presentation na maprofesa wenzako wa Japan au Korea. Pia wamechapisha maandiko katika majarida maarufu ya kimataifa kama ambavyo wanasayansi wa afya na siasa wanachapisha. Mwishowe wamejikuta wanakamatwa tena kimyakimya na kesi zao zinafichwa mbele ya public.

Taasisi yao inalalamika mazingira waliyokamatwa hayaridhishi, kipimo cha kusema wametoa siri hakiwezi tolewa na watu wa usalama ambao yawezekana hawajui hypersonic ni nini, kipi ni siri ya kitaifa na kipi kinajulikana.

Hayo matatizo kwa wanasayansi wa Urusi ni kawaida enzi na enzi, mfano Pavel Dulov alivyotengeneza Vkontakte, Facebook ya Urusi serikali ililazimisha inunue shares kubwa iathiri maamuzi ya platform kama access ya database. Dulov akajiondoa akaanzisha Telegram nako wakamzingua akakimbia nchi.
 
Ukisikia tawala za kidhalimu ndio kama hizo sasa! Mfumo wa urais uliojigeuza ufalme; mbaya kuzidi absolute monarchy.
 
Ndio nchi ambayo waswahili wanaipigia chapuo eti ni mkomboz wao

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…