Pamoja na sifa kedekede ambazo zimekuwa zikimwaga hapa jamvini juu ya hypersonic za Urusi.
Hypersonic hizo zimekuwa dhaifu mno mpaka sasa Urusi katumia zaidi ya kumi lakini ufanisi wake ni wa chini sana, hivyo kushindwa kuimaliza vita.
Kwa hali hii hamna namna ndiyo maana Putin analialia kwa sasa, ni wazi kwamba nguvu zake za kijeshi zimeanza kunyongonyezwa.
__
Marekani: Urusi yarusha makombora ya kasi 'hypersonic ' zaidi ya 10 tangu vita kuanza
Pentagon inaamini kwamba Urusi imetumia silaha zake za hypersonic takriban 10 hadi 12 tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, kwa mujibu wa afisa mkuu wa ulinzi.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne, afisa huyo alisema Marekani haina "hesabu kamili" ya kutumwa kwa silaha hiyo.
Urusi inadai kuwa kombora la Kinzhal ambalo linaweza kulenga shabaha hadi kilomita 2,000 (maili 1,240) na linaweza kuruka kwa kasi ya zaidi ya kilomita 6,000 kwa saa, lilirushwa kwa mara ya kwanza kwenye shabaha nchini Ukraine mwezi Machi.
Hivi karibuni, maafisa wa Ukraine walidai kuwa silaha hiyo ilitumiwa huko Odesa mwishoni mwa juma.
Afisa huyo wa Marekani, hata hivyo, alisema kuwa "hana chochote cha kuashiria" kwamba zilitumiwa dhidi ya sehemu zilizokuwa zinalengwa katika jiji hilo.