Wanaowagawia riziki wanapigana Nyie mnazidi kuwa masikini

Bsyotyo

JF-Expert Member
Apr 20, 2022
617
988
Leo hii angalieni mnavyoangaika Kwa Sababu Viongozi Tuliowachagua Hawana Huruma na Wananchi wao na Wala hawana Huruma na Hii Nchi ,wamekuja Kuvuna Vya Kwao na Familia Zao tu Zinemeeke na Keki ya Taifa.(Kodi zako)

Nchi za hao Wagawa Riziki walipokuwa wanazijenga Hawakuwa na

1. Demokrasia
2. Vyama Vingi
3. Kubembelezana
4. Haki za Wanawake
5. Uzazi wa Mipango
Na Mambo kibao waliowaletea Ninyi

Walihakikisha Nchi zao zinapigana Kuwa Leading countries Waliwaangusha Maraisi wasioendana na Kasi ya Maendeleo wanayoyataka wao. Walipigana Na Kuzijenga Nchi zao walitembelea mpaka Ma-bara mengine kuchukua watumwa na Kwenda Kujenga Nchi zao kwa Nguvu na Bila Kubembelezana Na Mtu yeyote yule wala Kutokujali haki za Binadamu wala Jinsia ya mtu

Walizaliana Vya Kutosha Na Kuwa Wengi sana Na kuwa na Man Power kubwa Ya Kuendesha Nchi zao .

Wameweka System sasa za Wao kuwatawala Nyie Mzidi kuwa watu wa hovyo na Muwategemee wao ili Msiwe na Ubavu wa Kujitegemea Wenyewe kwa Lolote lile

Wakawaletea

1. Elimu isiyoendana na Kasi ya Ulimwengu na Mnazidi kuikumbatia. Mtu kaka yake Amesoma Bachelor anasota Mtaani hajui A wala B katika Maisha(si kujiajiri wala kuajiriwa) ila kuna Kundi hilo hilo la Waafrika linawapeleka watoto wao kusoma Bachelor hiyo hiyo bila hata Kuwaza Kwa Akili zao wenyewe

2. Wamewaletea Uzazi wa Mpango wao ukiangalia Nchi zao wameshafika mil 300 mpaka Bil 1 huko Nyie Nchi Yenu Mpo Mil 50+ hata Mil 80 hamjafika ,mnameza Mavidonge ya Kuzuia kuzaa. Kisingizio Maisha magumu tutamleaje. Si kwamba Maisha ni magumu hamna vya Kwenu vya Kufanya muwalee hao watoto wenu. Nguo mnataka zitoke kwako.Sabuni zitoke kwao..Mafuta ya Kupikia yatoke kwao.. Gesi zitoke kwao.. Sukari itoke kwao. Sasa unadhani ukizaa wewe utamleaje wakati wagawa Riziki hizo ni wao . Wasipokupa hivyo vitu au wakaamua kukuwekea Vikwazo ndio ushakuwa Masikini Hueleweki wewe tena unakuwa Mtanga tangaji kila mahali kuomba Misaada.

Maana Mpaka Pesa unazozitumiaga wewe zinatokaga Kwao Wakikuwekea Vikwazo tu Hata Hizo Pesa Zinakosa Thamani

3. Wamewaweka kwenye Upetevu wa Kidini na Kuwagawa Ki-makundi makundi ili msielewane Nyie kwa Nyie. Leo hii likija Swala la Kitaifa Utashangaa Mnajiita sisi ni Wakaskazini hatuendani na Hao utasikia Sisi ni Wa kanda maalum hatumkubali huyo.. Sisi ni Wa-nchi fulani Hatutaki wa Nchi hiyo . Sasa Jiangalieni Mlivyo,

Wao Wamekuwa Wamoja ,lugha moja,kiongozi mmoja ,Nchi Moja Hakuna Atakayeleta Chokochoko nchini Mwao wakamuacha Salama, Ila Nyie mpaka Madini Yenu yanatoroshwa Mmekaaga Kimya Tu Utadhani Wanatorosha Madini ya nchi Nyingine kumbe Ni Madini Ambayo Yangeweza kuwatatulia Shida zenu za Barabara na Maji.

4. Mnajenga Vitu visivyoleta Tija Kwa Taifa.
Wekeni mazingira Salama kwanza Kabla Hamjaweka Wasomi wakiwa Wengi watakushinda Baadae. Huu ni ukweli mchungu. Huwezi kusomesha Watoto wako Wote Wakaaenda Shule lazima Wengine wasiende ili Nyumba Yako Uijenge Vyema, Hata Wao Wanataka Muwe Wajinga milele ili wanufaike Na Nyie Siku Zote. Wanajua Elimu wanayowapeni Haitawaletea Madhara Yeyote maana Ni Elimu ya Kujua Mambo Ya Miaka 50 yaliyopita Haiwezi kuleta Madhara Kwa Ulimwengu wa Nyuklia wa Sasa na Smartphones na Artificial intelligence.

Riziki Hazitoki kwa Mungu ila Zinatoka kwa Binadamu mwenzako. Akikubania Riziki ndio huzipati, msijidanganye Kwamba Mungu huwa anagawa. Leo hii Ukiwa na Watu wengi katika Mzunguko wako katika Maisha ndivyo Riziki zako zinaongezeka, ukiwa na Mzunguko mdogo ndivyo Riziki zako zitapungua. Na ukiwa na Vyako Ndivyo wahitaji wanakuwa wengi utakaowapa Na Unauwezo pia wa Kuwanyima Hivyo hivyo

Ndicho kinachotokea Sasa, Wagawa Riziki wanapigana kwa Ya Kwao, hamuyajui Ila Angalieni Mnavyoathirika , Hamna Chakula ,Mafuta,Usafiri ni Shida, Bei zimepanda Zinamuathiri Hadi Asiyejua Kusoma na Kuandika halafu Nyie mnakomalia Kujenga Shule Badala ya Kujenga Nchi Yenu Iwe na Vya Kwake Vya Kujitegemea.

Kama Wao waliweza Kuchimba Mafuta Nyie Mnashindwaje, Kama Waliweza Kuzalish Umeme Wa Kudumu Mnashindwaje Nyie, Kama Waliweza Kuwa na Usafiri wa Uhakika Nyie mnashindwaje. Nchi Kubwa Kama Hii Mnakosaje Sehemu ya Kuweka Watafiti wa Kujua Mafuta Yapo Wapi..


Waafrika Tumeoza Akili Zetu. Tunashindwa Kujua bila Sisi Wenyewe Kujitambua Na Kuwa na Mambo yetu Wenyewe hatutatoka Kwenye Mitego yao hata Siku Moja.

ASANTENI...

View attachment 2211200


Mifano Mizuri ya Vitu Vyetu wenyewe


Screenshot_2022-05-04-13-09-07-54_0b2fce7a16bf2b728d6ffa28c8d60efb.jpg
 
Hakika umenena vyema... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
Ubishi wao unatokana na Kutokujali Nchi yao Na Watu wao. Wanajali amejenga Nyumba Yake ana Magari Ya Kifahari . kumbe Hajui amebeba Laana Za Kodi za Watanzania waliotoa kwenye Mazao yao tena kwa Jasho kubwa sana . wao wanazikusanya Wanajipangia Vikao vya Uongo na Kweli ili Pesa Zitoke wakazile bila Huruma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom