Fumbo la Riziki

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Mafundi na wakufunzi wa lugha wameitafasiri kama ni 'Neema ya Mungu kwa viumbe wake'. Zingatia maneno '...kwa viumbe wake' ikimaanisha sisi wanaadam na wasio na visivyo binaadam.

Neema hii kwa viumbe hupatikana kwa njia kuu tatu ambazo ni:

1. Kufanya kazi
Hii inajumuisha kufanya kazi za halali na kupata kipato chako kwa kadri ya jasho lako. Imani zote kubwa zinatutaka tufanye kazi ili tuipate riziki yetu (soma Quran 62: 9-11) na (Biblia kitabu cha 2Wathesalonike 3:10).

2. Kutumia mabavu
Hata wale wanaotumia nguvu kupata riziki,nao hupata riziki hii kutoka kwa Mola. Isipokuwa tu riziki waipatayo si halali yao na wala hazina baraka za Mungu Mwenyezi.

Hii tunaita ni kulazimisha riziki. Ndo sababu watu wa aina hii hufananishwa na Wanyama wa msituni (kundi la MAHAYAWANI) ambao baadhi yao riziki zao humaanisha kupoteza uhai wa viumbe wengine. Mfano ni wanyama wote walao nyama. Hayo ndio maumbile ya riziki zao na hawana namna nyingine.

Hii dhana ya ulazima wa kufanya kazi ili upate kuishi inamuhusu pia mnyama huyu muuaji ambaye analazimika kukimbia mbio zaidi ya swala au Pundamilia ili apate nyama kama riziki yake,maana yake ni kwamba asipokuwa tayari kukimbia riziki yake hatoipata.

3. Bahati na Subira
Bahati zipo kwa waliojaaliwa kuwa na bahati tu. Hii ni ile rizki uipatayo bila jasho wala matarajio kwayo. Wapo wanaookota pesa. Wapo wanaoomba kazi wasizo na sifa nazo lakini wakaamua kujaribu liwalo na liwe na hatimaye likawa pasipo na matarajio yao. Palipo na shamba lako mwekezaji au serikali ikapahitaji na kukulipa mamilioni.

Wachimbaji madini wadogo wanajua maana ya bahati licha ya jasho wanalokamua migodini. Kwa ziada tu,bahati nayo huwa haitafutwi,ndo sababu Mungu hataki mshiriki hiyo michezo ya Bahati nasibu(Kamari na Ushirikina pia). Bahati yenyewe ndio humfuata au hukutana na mwenye kuistahili pale alipo.

Kwa upande wa Subra,hii huenda sambamba na namba moja(1) na tatu (3) hapo juu. Aliyefanya kazi kusubiri mshahara mwisho wa mwezi anaishiriki dhima hii ya subra. Kazi zote zenye matokeo makubwa si ya malipo au faida ya papo kwa papo, hii ndo kusema kwamba SUBRA ni nyenzo muhimu kwa Mja kuisaka na kuipata rizki.

Tazama mshairi na mwanafasihi mmoja almarhum Shaaban Dede Kamchape aliimba kwenye wimbo wake maarufu wa 'Dunia Duara' alilifumbua fumbo hili la RIZIKI kwa kalamu. Ninanukuu sehemu ya shairi lake:

"...Samaki baharini,...huishi vipi,...wadudu mapangoni,....wanyama porini, ....na wasiojiweza huishi vipi,....ntaivuta subira, siku itafika.

Dunia DUARA jamaee, hapa shska huzunguka,leo kwangu kesho kwako,Jua halina mpaka,huangaza kote.."

DEDE alihoji kwa mwenye kujua, wale samaki watamu baharini,wadudu wa mapangoni na wanyama kule porini wanaishi vipi ikiwa hawalimi,hawafanyi kazi kuajiriwa wala biashara hawana,lakini mbona wanaishi?

Hakika hakuna mwenye jibu na kama yupo basi atasema hiyo ndiyo rangi na sura halisi ya riziki ambayo humfikia Mja kwa kadri ya Mipango ya Mungu Mwenyewe na si vinginevyo. Na mwisho Dede anaonekana alikua akiuliza swali ambao analijua jibu lake,akajiapiza kuivuta SUBIRA mpaka siku ya zamu yake itapofika,anayo YAKINI kwamba kuna siku zamu yake itafika tu na atapata kwa kadri ya jasho alilolikamua kwa kazi anayoifanya.

Tabia za riziki
Riziki inajitambulisha kwa tabia zake kwa waja,nazo ni kama ifuatavyo:

1. Kila upatacho si chako peke yako.

Hapa tunakumbushwa kuwa na tabia ya kugawana na wenzetu kila kidogo tukipatacho. Tabia ya kutoa.
Na kutoa kwa wenzako kuna njia mbili,moja ni kwa hiyari na ridhaa yako mwenyewe na mbili ni kutoa pasi na ridhaa wala ufahamu wako.
Ukigawana na wenzako iwe ndugu jamaa au marafiki itahesabika kama Sadaka. Hii inafahamika sana.
Lakini hii ya pili wengi wetu huishiriki bila kujua,na kwa sababu haikuwa hiyari yetu tumethubutu kuipa jina baya la HASARA.

️EBU tazama umejiandalia chakula chako kizuri,kisha aidha chote au sehemu ya chakula hicho kinamwagika au kinakushinda kumaliza na inakulazimu kumwaga.
Fikiria kikishaanguka sakafuni hatima yake ninini,huwa ni chakula cha wadudu na viumbe uwajuao na usiowajua. Hii sasa ndo ile dhana iliyosemwa kwenye tafsiri ya neno RIZIKI na baadae kushereheshwa na Dede kuwahusu 'viumbe' kwa maana ya wanaadam na viumbe wengine. Hawa nao wanahitaji riziki ya kila siku kama wewe na hasa vile vinono vya kunukia tazama sisimizi wanavyovishambulia. Sasa kwa wewe kuangusha chakula au kumwaga ndo umetumika bila kujua kuwalisha viumbe wa Mungu.

️ jiulize unapodondosha pesa ambayo kuna anayekuja kuiokota aidha ikamfaa yeye au yeye akaitumia hiyo pesa kumsaidia mwingine.
Tazama ukinunua nanasi au tunda lolote wewe utakunywa juisi yake na makapi hayakufai utayatupa. Ebu jaribu kufuatilia uone ni viumbe wangapi iwe panyq,Inzi,mende sisimizi na wadudu jemsi kwa aina zake wanavyoyafakamia makapi hayo ambayo kwako wewe tayari ni uchafu.

Riziki huwa haichagui,msanii Selemani Msindi alilithibitisha hili kwenye shairi lake la 'Usinichukie' pale aliposema " ...kama unanichukia basi ewallah,..yote namwachia Allah,.....wote anatupa mvua misikiti na makanisa,...wote anawapa jua masikini na wenye pesa. .."
Mwisho nimalizie,umewahi kujiuliza kwanini tajiri analazimika kuajiri sisi akina kapuku tukamfsnyie kazi kiwandani kwake au nyumbani kwake, jibu ni kwa sababu wewe unaweza kufanya hicho anachokihitaji na asichokiweza yeye kufanya. Huwa hatupewi vyote,aliyepewa fedha nyingi huyu hawezi(sio hajui) kushika shepe na kuanza kuchanganya zege.

Ni lazima apate mtu wa kumtumikisha kazi zake ili mwisho wa siku yeye ataendeleza biashara zake na sisi masikini tutapata riziki zetu za elfu tano tano kwa malipo ya vibarua kwa tajiri huyu.

Hata wewe mwenye fedha za kujenga majengo mazuri ya kuendesha biashara ya shule,majengo yako hayatokufaa kama hutopata waalimu wa kukufanyia kazi ya kuwafundisha wanafunzi wanaolipa ada.

Hilo ndilo jibu la Fumbo la Riziki, linatulazimu kuheshimiana kwa sababu tunahitajiana ili maisha yaendelee.

Ndimi,

M. Majaliwa,Adv.( Mwalimu wa Kiswahili, ukiniita 'Galacha' wa Kalamu nitaitika bila taabu)
 
Interesting
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom