RedDevil
Ndugu yangu RD vita vya ukombozi vinahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana vinginevyo huwa ni ngumu sana kuufikia ukombozi. Afrika Kusini wakati wa mapambano ya kuuondoa ubaguzi still kulikuwa na waafrika wenzao (vibaraka) waliokuwa wanabeza, kukejeli harakati za kujikomboa. Si kwamba walikuwa hawajui ubovu wa ubaguzi lakini kutokana na roho isiyo ya kizalendo(hata kama walilipwa) walidiriki hata kusabotage harakati za wazazi wao(kina Mandela).
Vivyo hivyo hapa kwetu Tanzania hali ni hiyo hiyo. Kuna makundi ya aina tatu(maoni binafsi), kundi la kwanza ni lile linalofaidika na utawala uliopo(viongozi, wafanyabiashara). Kundi la pili ni la watu wanaotumika bila wao kujijua(wafanyakazi, wanachama wa vyama vya siasa) na kundi la tatu ni lile linalofanyakazi kwa niaba ya kundi la kwanza kifupi niwaite vibaraka(agents kama NEC, Msajili, UWT, Polisi, Media nk). Hili kundi la tatu linajua linachokifanya tofauti na kundi la pili.
Nafikiri RedDevil utakuwa unazungumzia hili kundi la tatu(vibaraka). Hili kundi ni hatari sana katika harakati zozote zile ziwe za kijamii, kisiasa, kiuchumi, kimaendeleo nk. Hatari kwa misingi kuwa effect yake inagusa moja kwa moja maisha ya binadamu, chukulia polisi au media, tendo moja zuri au baya linalofanywa na vyombo hivi haliishii kwenye ofisi au mitambo yao tu linakwenda hadi kijijini kule kwa mtu anayelima matuta ya viazi.
Vibaraka hao hao ndio wanaoendesha kampeni humu JF ya kuwakatisha tamaa wanaharakati wanaoonekana kutaka mabadiliko. Waliopo humu JF ingawa wanajitahidi sana kujificha (kutumia posts ofcourse) kwa kutoonyesha upande wowote lakini ukifuatilia posts zao lengo ni lile lile la kukatisha tamaa. Mfano mtu anakuja kuja na post hii ''Slaa ni kiongozi mzuri lakini kafanya makosa kuachia jimbo''. Post kama hii ukiisoma kwa juu juu si rahisi kum pin point mtu wa aina hii yupo upande gani, ila ukiichunguza kwa makini ni sentensi ya kukatisha tamaa(kubomoa) zaidi ya kujenga.
Kuna mifano mingi ya watu wanaofanya hivyo humu ila sidhani kama ni busara kuwaongelea hapa, it is very sad. Lakini waelewe kuwa historia huwa inajirudia leo watawafanyia wenzao kesho si mbali itakuwa zamu yao kulipa the price. Kama Mlalahoi alivyosema the best thing to do ni kuwa ignore, hata kama kila siku kutakuwa na members wapya wa design hiyo lakini itafikia time wataanza kujiondoa wenyewe, kwa sababu ukombozi haukomi siku ya uchaguzi, navyojua mimi ukombozi unaanza baada ya uchaguzi.