Wanaovuliwa ubunge kwa tuhuma za rushwa wapewe adhabu stahili

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Japo si mwanasheria lakini najua adhabu ya kutoa rushwa ni kifungo na viboko siku ya kuingia jela na siku ya kutoka, ili mkosaji akamwonyeshe mkewe (au mumewe - akina mama oyee!) Sasa kuna mbunge wa Sumbawanga amevuliwa ubunge na moja kati ya vielelezo mahakamani ni kutoa rushwa. Haitoshi kumvua tu ubunge, apandishwe sasa katika kizimba cha jinai ili apate adhabu stahili.
 
Napendekeza kwa kuanzia warudishe mshahara, posho na malipo waliyopewa kama wabunge na kuwajibishwa kama matapeli wa haki
 
Japo si mwanasheria lakini najua adhabu ya kutoa rushwa ni kifungo na viboko siku ya kuingia jela na siku ya kutoka, ili mkosaji akamwonyeshe mkewe (au mumewe - akina mama oyee!) Sasa kuna mbunge wa Sumbawanga amevuliwa ubunge na moja kati ya vielelezo mahakamani ni kutoa rushwa. Haitoshi kumvua tu ubunge, apandishwe sasa katika kizimba cha jinai ili apate adhabu stahili.

Adhabu hiyo ya viboko ilikuwa wakati wa Nyerere!
 
Japo si mwanasheria lakini najua adhabu ya kutoa rushwa ni kifungo na viboko siku ya kuingia jela na siku ya kutoka, ili mkosaji akamwonyeshe mkewe (au mumewe - akina mama oyee!) Sasa kuna mbunge wa Sumbawanga amevuliwa ubunge na moja kati ya vielelezo mahakamani ni kutoa rushwa. Haitoshi kumvua tu ubunge, apandishwe sasa katika kizimba cha jinai ili apate adhabu stahili.
Ajabu ni kuwa wakati wa mchakato wa uchaguzi Takukuru walijinasibu kuwa wapo makini wakiangalia vitebndo vya rushwa. Ukiondoa kesi ya Mwakalebela, sijasikia kesi nyingine kubwa ya mbunge aliyenaswa kwa kutoa rushwa. lakini juzi mahakama imethibitisha kuwa Aeshi alitoa rushwa, hivi hii takukuru ilikuwa inafanya nini mpaka isione haya? na tena, mahakama imeshasema huyu alitoa rushwa, tuone takukuru watafanya nini kumshitaki huyo kwa rushwa kwa maana uthibitisho umeshapatikana
 
Hapa kimsingi yeyote ambaye inabainika kapata uongozi kwa namna yoyote ambayo si halali na hata kutenguliwa na Mahakama basi Mahakama haina budi kuwapa adhabu stahiki kulingana na sheria inavyojieleza"
 
napendekeza kwa kuanzia warudishe mshahara, posho na malipo waliyopewa kama wabunge na kuwajibishwa kama matapeli wa haki
kaka hapo nakuunga mkono arudishe na lile deni la milioni 90 walizokopeshwa then apigwe mvua ya miaka
 
Kwa mujibu wa sheria ukikutwa na hatia ya kujishughulisha na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi adhabu yake ni kuenguliwa ubunge na kutouhusiwa kugombea kwa miaka mitano, nitakuja na vifungu husika baadae kidogo
 
Back
Top Bottom