Wanaoutaka urais 2015: Yupi anafaa?



Na mnastahili mbaki bila lami hivyo hivyo. Mmewezaje kumwacha mpiganaji kama huyu na kwenda kuchagua watu wasio na uwezo. Huoni kama mmetucheleweshea maendeleo ya Taifa kwa kumchelewesha Magufuli kuja kututumikia..?
 

Sasa hivi umebadilika....shughuli kubwa ni kutoa kucha na kung'oa meno tu
 
Bora umewaambia ndugu yangu, watu wanafikiri kubwabwaja na waandishi wa habari ni Urais. Quote again ''Wazee wa hekina na busara wako kimya kabisa ndio watakaotoa Rais wetu 2015''.:flypig:

Busara yao iliisha kwa kumchagua huyu ******
 
Rais Anatoka kwenye system wanamtandao wenyewe wanakwambia sasa sijui ni yupi yetu macho

Inaekea kuwa mwenzetu bado unaamini kuwa Rais lazima tu atoke CCM ................. hata baada ya kudhihirika wazi kuwa wameshindwa kutuongoza vema.
 
Ndahani for presidency.....naomba support yenu
 
Hafai huyu aliuza nyumba zetu za serikali kwa bei ya kutupa na mpaka leo hataki kukiri kosa lake..mbabe na ana-umimi kama Zito

hivi ukitafuta mtu asiyye na kosa kabisa basi hatutapata kiongozi sababu kila mtu ana mapungufu yake ndio maana tunaangalia mchapa kazi other factors remain constant.
 
Kama umejituma basi you are a let down in the first place. Kwanini unakubali kujikomba kana kwamba huna la kufanya la maana kwa ajili yako, familia yako na taifa lako? Think twice.
 
Kama mtu asiyekuwa na akili ameuweza urahis magufuli atashindwa vipi?
 


Siku hizi wakijua unakipawa chauongozi wanang'oa meno kaka we acha tu
 

Ngoja nikusaidie kidogo tu ndugu yangu inaonekana uelewa wako ni mdogo juu ya nyumba za serikali na kazi za mawaziri ni kwamba Waziri humshaauri Rais juu ya jambo analoliona kwa uelewa wake kuwa halifai, lakini ni hiari ya Rais kukubali ushauri au kuukataa ushauri wa Waziri wake yeyote, hapo dhambi ya Magufuli iko wapi? Magufuli kama alivyo binadamu yoyote ukiwemo wewe na mimi tunamapungufu yetu tunachoangalia ni ni advantage na disadvantage ya huyo mtu percent ikizidi kwenye faida unamchukua na ikizidi kwenye hasara unamwacha ila kamwe dhambi ya nyumba ni ya Mkapa. Dr. Pombe hakuwa na uwezo wa kuuza nyumba yoyote ya serikali bila idhini ya Ben, na hatatokea duniani binadamu atakayewaridhisha watu wote, hata ukipewa wewe uongozi utalaumiwa tu, wameshindwa mitume na manabii wakaambulia kuuawa itakuwa Magufuli!!! Dr. Magufuli hana chema hata angetoa roho yake mtasema anapenda sifa ndiyo maana kajitoa roho. Mungu anajua nani atatuongoza baada ya JK hatuna sababu ya kulumbana kwa kuwasema watu vibaya wakati kazi wanazofanya zinaonekana. Kwa mfano ni waziri gani katika historia ya nchi hii alishakataa barabara iliyojengwa kwa msaada wa nchi yoyote kwa maelezo kwamba ina kasoro tofauti na Magufuli? Pale TANROAD alikuwepo Mrema aliyeshindikana mpaka kwa wabunge walishindwa Dr. Shukuru kwawambwa pia alimshindwa lakini Magufuli aliporudi Ujenzi Mrema mwenye ajira na sifa zenye utata yuko wapi? Tatizo kubwa kwetu watanzania tumezoea kubembelezwa na kudanganywa kama watoto tunafurahi sana. Lakini tukiambiwa ukweli inakuwa tatizo na tatizo la Magufuli ni kusema ukweli na kusimamia anayoamini ni ya kweli hana kasoro nyingine. Na mwajiri wake anajua kuwa ni mchapa kazi ndiyo maana kila baraza la mawaziri likivunjwa yumo huo ni uthibitisho tosha kwamba anafaaa ni mawaziri wangapi wameshaachwa toka JK aingie madarakani angalia wengine hata mwaka hawakumaliza mfano Waziri Maige, (Simon Mbilinyi, Juma Ngasongwa Enzi ya BWM) na wengineo kuingia tu uwanjani wakapewa kadi nyekundu tena kwa mambo ambayo hawakuyafanya.
 
Kama mtu asiyekuwa na akili ameuweza urahis magufuli atashindwa vipi?

Santo huogopi kung'olewa kucha na meno kusema baba riz1 hana akili? shauri yako watafuatilia modemu yako mpaka ulipoiweka siajabu hutaonekana tena hapa JF maana Mabwepande iko shughuli kama hujui muulize zombe na ulimboka watakuambia mimi huyoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo vichakani.
 
kunakijana aliyesoma UDOM mwasisi wa kikundi cha class struggle na aliyewahi kuwa waziri wa chakula na uwekezaji anaitwa Richard Mtui naona huyo anafaa kuwa rais wa Tanzania tumtafute tumuombe anatufaa.

Richard Mtui nimwsoma naye anafaa kuwa waziri wa chakula jinsia na wanawake
 
Wadau;
Watu wenye dhamira ya dhati kabisa kabisa ya kuifanya nchi hii kuendelea Ki- Viwanda na Ki- Uchumi wamebakia kuwa Madereva taxi na Vinyozi tu, Wengine woote ni wachumia tumbo. Period !

Mimi nilishasema, wanaojulikana hawafai, wanaofaa hawajulikani.

Kwa sababu ili kujulikana inabidi uanze chini kwenye ubunge ubunge huku.Na huko kumejaa rushwa tupu na dirty party politics.

Kwa hiyo watu wenye uwezo na integrity wanashindwa.

Wanaoweza mikiki hiyo na kuja kuibuka kwenye national politics wanakuwa wachafu tayari na kwa hivyo hawafai.
 
Ni magufuli aliyesimamia uuzwaji wa nyumba za serikali kwa bei ya kutupa. Nyingine alimgawia mchumba na mdogo wake. HAFAI KUWA RAIS
 
mkuu hapo kwenye blue pana husika!!! mimi huyu jamaa nampenda sana,ila shida ndo hiyo yuko kwenye kile chama kileee...sio siri akibadili chama hata mimi kura ntampa mana uwezo anao na amedhiirisha hilo kwa misimamo yake tofauti na huyu DHAIFU!!
 
Kuna jambo huwa nadhani watu wengi huwa hawajiulizi kabla ya kufanya maamuzi ya kujitangazia kuwa wanautaka urais. Watu hawa huwa fikra zao huishia kuwa kuwa rais ni kula bata na starehe za kufa mtu. Kumbe lah. Nadhani mkimuuliza JK kwa sasa hamasa aliyokuwa na mawazo aliyokuwa nayo wakati anautafuta urais kwa udi na uvumba atakupa jibu tofauti ingawa kwa sasa hali ilivyo ni siri yake. Naelewa kuwa mtu yeyote anao uhuru wa kukitafuta kiti hicho lakini.....sidhani kama wengi huwa wanajiuliza unyeti wa nafasi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…