Wanaotangaza vifo vya watu mashuhuri kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii wajumuishwe kwenye uhujimu uchumi, hawana nia njema na Taifa letu

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,859
20,713
Shetani kazi yake ni kuharibu, kuua na kuiba, ndivyo Biblia inavyosema. Kwa hiyo kila mahali utakapo shuhudia uharibifu, vifo na wizi, ni lazima mkono wa Shetani upo. Si ajabu kwa hiyo kwamba Shetani hufurahia matukio hayo na hufanya kila mbinu chafu ili watu waibiwe, wafe na kuwe na uharibifu.

Kumezuka siku za hivi karibuni tabia ambayo si ya kawaida na kiungwana kabisa kwa binadamu, ambayo sina shaka yeyote kwamba ina mkono wa Shetani. Tabia hii ni tabia ya kutangaza na kushabikia vifo vya watu mbali mbali, hasa wenye mamlaka au ukwasi, katika hali inayo-ashiria kwamba matangazo hayo yanafurahia vifo hivyo. Kiukweli ni Shetani tu anayeweza kufurahia kifo cha binadamu yeyote.

Ukitafakari kwa kina matangazo hayo, utagundua pasi shaka yeyote kwamba ushabiki huu wa watu kufa una misingi ya kishetani. Najua wapo watu wenye nia mbaya na taifa letu, hii ni pamoja na kuona kwamba Taifa letu linapata majanga ya kila aina,i li lisifanikiwe kwa njia yeyote ile. Makundi yenye nia hii ovu ni ya watu ambao waliigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi na hata kulifanya kuwa soko la madawa ya kulevya.

Ni vigumu hasa kuona watu hawa wanapata faida gani kwa hararaka haraka kwa kuitangazia dunia kwamba Tanzania watu wanakufa sana. Hata hivyo ukitafakari kwa kina utagundua sababu ya kushabikia vifo hivyo!

Sababu ya msingi ni Ili Tanzania ionekane kwamba ina ugonjwa wa Corona na hivyo kuharibu uchumi wa nchi yetu. Haishangazi kwa hiyo kwamba Ubalozi wa Marekani umetangaza kwamba Tanzania sio salama kutembelea, eti kwa kuwa kuna Corona wakati Marekani kwenyewe tatizo lipo, tena kubwa sana hata kuliko Tanzania. Haishangazi pia kwamba Marekani imetangaza eti nia yake ya kuisaidia Tanzania ishinde Corona wakati kwao wameshindwa! Nia ya matangazo yote haya ni ile ile, kuifanya dunia iamini kwamba Tanzania kuna Corona na hivyo kuharibu tashwira yake kimataifa na uchumi wake.

Tupo kwenye vita ya kiuchumi ambapo tumediriki hata kuanzisha mahakama za mafisadi. Hawa wanaotangaza vifo vya watu mashuhuri kwenye mitandao ya kijamii na forums zingine,hawana tofauti yeyote na wahuju uchumi, wawe rounded up na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Tukiwachekea tutakula mabua.
 
Nani kakwambia Marekani watu wanakufa na Corona kuliko hapa kwetu? Au umesikia kwa Mzee baba?

Unalinganisha vipi wewe nchi mbili kuja na kauli nyepesi kama hii?

Habari zingine za uongo na kweli kama hizi muwe mna zipeleka Chatto vijijini.

Mijini wana uelewa zaidi. Huko hamuwezi kutoboa.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Natamani sana nikuone unavyo fanana.Si ajabu ni wa ajabu ajabu kama mawazo yako yalivyo.

Hebu toa majibu ya haya: Watu hao hawafi wanazushiwa? Je,korona haipo? Kati ya hao wangapi una hakika hawajafa kwa korona?
Ningekuona wa maana kama ungelaani wasiojulikana waliotupaka tope la kutaka kuua na kuteka wakosoaji wa "mtukufu" wenu asiye na chembe ya ubinadamu!
 
Nia ya matangazo yote haya ni ile ile,kuifanya dunia iamini kwamba Tanzania kuna Corona na hivyo kuharibu tashwira yake kimataifa na uchumi wake.
Kikubwa ulichotaka kuwasilisha ni hiki.

Karibu dunia nzima inapambana na huu ugonjwa. Sasa "taswira ya nchi" inaharibika vipi kujulikana kwamba kuna corona na watu wanakufa? Kila mahali wanakufa.

Hata wasipotangaza vifo haihalalishi kwamba huo ugonjwa haupo. Tusifiche matatizo tujitahidi kuyatatua sio hadi vifo "vituumbue".
 

Ivi mkuu ulisoma Civics kweli? kuna kitu kinaitwa freedom of speech and expression wacha watu watoe taarifa
We unafikiri nini kazi ya mass media labda?
Mimi nilisoma Political Science achana na Civics,ila hakuna uhuru usio na mipaka.Aliyekuambia kuna 100% freedom of speech kakudanya.Hata hao waliokudanganya kwamba kuna kitu kinaitwa freedom of speech kwao hakuna.
 
Kikubwa ulichotaka kuwasilisha ni hiki.
Karibu dunia nzima inapambana na huu ugonjwa. Sasa "taswira ya nchi" inaharibika vipi kujulikana kwamba kuna corona na watu wanakufa? Kila mahali wanakufa.

Hata wasipotangaza vifo haihalalishi kwamba huo ugonjwa haupo. Tusifiche matatizo tujitahidi kuyatatua sio hadi vifo "vituumbue".
Wewe sio scientist,ndio maana udaku wa mainstream media,Bill Gates na akina Anthony Fauci ambao ni first class scientific cons umekubeba.I pitty you people. Kila upepo unawabeba you do not have independent minds!Inasikitisha.
 
Wewe kama ni profesa,kiongozi wa serikali,kiongozi wa kanisa au tajiri jiandae.
 
Acha ufala swali la kujiuliza ni je hawajafa kweli? Kama wamekufa kweli wacha waseme tu
 
Acha ufala swali la kujiuliza ni je hawajafa kweli? Kama wamekufa kweli wacha waseme tu
Sio ubinadamu kushabikia kifo,after all kila mtu atakufa,it's just a matter of time.Ni Shetani tu anayefurahi binadamu wakifa,tena dhambini.
 
Back
Top Bottom