Ulongupanjala
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 8,523
- 14,002

Habari zenu wadau
Hivi huu utandawazi ndio umetufikisha hapa,yaani mtu anatafuta mwenza wa maisha kama anatafuta shamba boy
Ni kweli watu wapo serious kutafuta wenza wao wa maisha kwa style ya kama ya attachment niliyoweka au ni utani tu.
Ina maana siku hizi ili mradi uwe na smart phone/tablei/ipad/computer na iwe na internet basi wewe unapata mke kiulaini? Siku hizi hakuna kuzungushwa mara njoo kesho mara keshokutwa na kama domo zege bado unapata mwenza kiurahisi tu? Kweli maisha yanabadilika kila kikicha.
NB:Nimeanza kupokea PM,sihitaji mwenza,ninaye tayari ila ninauliza je hao wanaotumia style ya kujitangaza kama attached file,je ni sahihi.
Weekend njema wadau