ARCHBISHOP
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 271
- 488
Dah! Huyu si anatoaga mpaja misaada? Nimemsahau jina.Kuna yule nani sijui wa Makongolisi Chunya, ni hobby kama hobbies nyingine.
Mh! HatariMkuu hizo ni hobby kama kuogelea na kwenda gym tu...
Mbona wadau wanaenda kuogelea na hela wanatoa beach??
Na yeye anapiga kwa kutumia vocha yake kama hobby..
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]Edward kabamba Edward kabamba hahah
Hawa kuna kitu nyuma ya pazia sio bureKuanzia clouds, east africa radio, capital radio, radio one na zingine sikosagi kusikia jina la spora malisa khaa sijui huwa anaweka alarm? kwenye kutuma msg pia huwezi mkosa sikuhizi namsikia mpaka bbc swahili.
Kuna mmoja alikuwa anaitwa Ugali Sokwe!!Edward kabamba,na mwingine waziri wa njaa na mipango ya gafla(huyu alikua na jina reeefu afu ndo anamalizia na hayo maneno[emoji23] eti waziri wa njaa na mipango ya gafla)
Mzee unaona mate mpaka kwenye redio?Matola ndo anawafahamu vizuri magwiji wa kupiga simu kwenye hizi radio.
Halafu hata kwenye kusalimiana wanasalimiana wenyewe kwa wenyewe.
Kuna jamaa mmoja huwa anapiga simu kwenye kipindi kinachoongozwa na somebody Mbogo, huyu jamaa akiwa anatoa hoja zake hadi mate huwa yanamtoka nadhani. Na hakosi kila nikisikiliza hiko kipindi.
Baba mzazi babaEdward kabamba Edward kabamba hahah
"Wanapata wapi muda na pesa?" Nijambo ambalo nimekuwa nikijiuliza tokea nikiwa mdogo.
Kuna watu walikuwa vinara wa kupiga simu redioni, leo wengine wamepotea, wengine wamepunguza, watu kama Suzzy Ngodoki, Pagija wa Pagija, Mwili Obale, n.k
Leo wameibuka wengine wanapiga simu kuchangia mada kila redio, utawasikia Clouds kila kipindi, RFA, Redio one, E fm.
Najiuliza hawa watu wanafanya kazi gani? Huu muda wanautoa wapi wakushinda wakitoa maoni redioni? Je, ni ushamba au ni ujanja?
Maoni kutolewa na watu wale wale kila siku, redio hazioni kuna dalili ya kufeli? Wengi wao hutoa maoni mepesi sana, unaweza dhani wanafanya mradi siku isipite bila kuchangia maoni redioni.
Wewe una mtazamo gani? Nani umemzoea kumsikia?
Lawena SondaBaba mzazi baba