Wanaopenda kufanya kazi ulaya

Wanaopenda kufanya kazi ulaya

mpigilie

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
310
Reaction score
136
Wakati nafanya kazi uingereza,masharti haya yalikua yamebandikwa ofisini kwetu:
1. Marufuku kucheka ofisini
> Kucheka kunapunguza concentration kazini

2. Hairuhusiwi kwenda kujisaidia haja kubwa
> Tendo hilo linachukua mda mrefu hivyo ni wastage of time

3. Kusalimiana ni mara moja tu kwa wiki (jumatatu tu)
> Salamu zinapoteza muda

4. Mawasiliano yote ni kwa njia ya computer,including salamu,kucheka,kuomba msaada mfano kama umeumia,kupiga miayo kama ishara ya uchovu...


Wadau mnaweza kunikumbusha masharti mengine niliyoyasahau
 
hayo masharti nilihadithiwa na jamaa mmoja ni ya kuzimu
 
Hayo masharti,mmmh
na Ban Ki Moon naye anayafuata?
 
Naomba watuletee huku maana kuna watani zangu wanaalimiana nusu saa na ushee kila baada ya masaa mawili wakionana
 
mkuu kama hajakubwa ni wastage of time sasa nafanya kazi kwa sababu gani
 
Naomba watuletee huku maana kuna watani zangu wanaalimiana nusu saa na ushee kila baada ya masaa mawili wakionana

Unawazungumzia wale wa kanda za juu kusini??
 
kujamba marufuku coz utasababisha watu wapoteze muda kwa kujipuliza kufukuza harufu chafu...hii naikumbuka sana kipindi nipo germany kwenye ofisi ya kusafirisha mizigo kwa treni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom