Wanaopaswa kumlalamikia refa ni Azam Fc dhidi ya Dodoma jiji na siyo Yanga Sc dhidi ya Ihefu Fc.

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,265
12,764
Azam walizulumiwa goli Lao la haki kabisa bila ya kipingamizi, goli lilifungwa lakini mshika kibendera alinyanyua juu kibendera kuashiria kuwa mfungaji kaotea Lakini katika marejeo ni goli halali kabisa bila hata ya kupepesa macho Azam walizulumiwa.

Mchezo wa Yanga Sc wanapaswa kulaumiwa benchi la ufundi na kocha wake kwa kuanza na wachezaji toka benchi katika mechi ngumu Kama hii.

Nilipoona kikosi tu nikajua kocha wa Yanga Sc kawazalau Ihefu na hata uchezaji wa wachezaji kipindi Cha kwanza ilikua hakuna molali walioona Kama mechi wameimaliza baada ya kupata goli dakika za mwanzo.

GOLI LA KWANZA LILILOFUNGWA NA IHEFU LILIKUA NI KOSA LA BEKI (MAMUNYETO)

Back pass na Diara baada ya kurudishiwa pass ikamshinda akalazimika kufanya madhambi na pigo huru lilizaa goli Tena goli ambalo wachezaji walikabia kwa macho mpaka mchezaji wa Ihefu anamalizia mpira uliotemwa na Diar

Lawama zote ziende kwa benchi la ufundi kwa kuzarau mechi ngumu Kama hii na ndiyo maana Yanga wamehukumiwa lakini kusema kuwa Yanga inahujumiwa ni kutoa maneno kwa kupaniki tu.

Kidooogo Refa alaumiwe kwa kuminya muda wa nyongeza maana Ihefu walilala sana lakini kwa maamuzi ya uwanjani siwezi kumlaumu muamuzi.

Wanayanga hampaswi kumlaumu muamuzi wanaotakiwa kulalamika ni Azam Fc ndiyo walihujumiwa wazi wazi na siyo Yanga Sc tubadilike.
 
Ngoja wanakuja na mawe yako mkuu, leo wamechanganyikiwa wanaogopa kumsema kocha maana walituaminisha ni kocha bora wanaogopa kuwasema wachezaji maana huwa wanadai wa kikosi bora na kipana akitoka mtu anaingia mtu sasa leo nani alaumiwe
 
Ngoja wanakuja na mawe yako mkuu, leo wamechanganyikiwa wanaogopa kumsema kocha maana walituaminisha ni kocha bora wanaogopa kuwasema wachezaji maana huwa wanadai wa kikosi bora na kipana akitoka mtu anaingia mtu sasa leo nani alaumiwe
Kocha kapanga kikosi dhaifu.
 
Back
Top Bottom