JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 6,835
- 14,209
Hizi akili huwa mnazitoa wapi?hatutaki serikali iajiri per se,kwenye taasisi zake,tunataka iweke sera bora,Sekta binafsi ichangamke,izalishe ajira kibao,Kama wasomi wa vyuo wa korea,japan,china,wanazungumzia ajira,sembuse sie wa ulimwengu wa tatu,hata USA,ajira nyingi zimetengenezwa na sekta binafsi,iliyosaidiwa na sera bora za uchumi zinazosimamiwa na Serikali,Kazi ya serikali sio kuajiri. Huko vyuoni mnaposoma huwa mnaambiwa mkimaliza mtaajiriwa?
Hatutaki kwenda TRA,Bandari,TBS,TBC,tunataka tukiingia kwenye kilimo,mazao yapate soko,sio serikali ishindane na sisi kwa kuanzisha wakala anayesaga na kukoboa nafaka,
Viwanda vya magari South Afrika,sio mali ya serikali,mashamba makubwa ya kisasa sio ya serikali,ni watu binafsi,
Ukienda Zanzibar,wazungu wote wanaoanzisha mahotel,wengi wao,hawajawahi kuajiliwa serikalini,walifika hapo walipo kutokana na mpango madhubuti ya serikali,
Kampuni inayotengeneza bidhaa ya samsung,kule korea,ni ya mtu binafsi,hatuitaji serikali ijenge nyumba,ilime,serikali hii haiwezi kufanya biashara,iangalie TTCL,hoi,haiwezi hata kushindana na halotel!