






Hawa ni wajumbe wa Bodi ya chuo cha Ufundi Arusha ambayo imelalamikiwa sana kwamba ilifumbia macho au nayo ilikuwa sehemu ya ufisadi mwingi uliofanywa na menejimenti ya chuo. Kuanzia kulia ni: Lyne Ukio, Karoli Njau, Hyacintha Makileo, Benedict Lema, Thomas Katebalirwe, Suzan Mosha na Christian Wambura Nyahumwa. Kimsingi Bodi hiyo kwa sasa haipo kisheria lakini bado inafanyakazi bila kufahamika msingi wa kuendelea kuwepo kwake
Kwa muda sasa kumekuwa na malalamiko ya matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi wa kutisha uliofanywa na Menejimenti ya chuo kwa kushirikiana na wajumbe wa Bodi.
Imesemekana Mkuu wa chuo anatumia nguvu kubwa kuhakikisha wajumbe hawa wanaendelea kuwepo kwenye Bodi kwa lengo la kuendelea kukiteketeza chuo licha ya chuo kuwa na sheria mpya ambayo kimsingi inahitaji Bodi hiyo kuundwa upya.
Msingi wa kuundwa upaya kwa Bodi ya chuo licha ya tuhuma za ufisadi zinazoihusu Bodi hiyo ni kutokana na kuwa na muundo mpya wa Bodi kutoka na Baraza la Elimu ya Ufundi, NACTE. Sheria ya NACTE ndiyo iliyotumika kuanzisha Chuo cha Ufundi Arusha. Kadhalika, umuhimu wa kuunda upya Bodi ya chuo kunatokana na muda wa aliyekuwa M/Kiti wa Bodi hiyo Marehemu Abrahamu Nyanda kuitumikia Bodi hiyo kuisha, na hivyo kuwa hakuna Bodi kisheria.
Sababu nyingine ya kutakiwa Bodi hiyo kuundwa upya ni jinsi Bodi hiyo ilivyokuwa imeundwa hapo awali. Hapo kabla, Bodi ya chuo iliundwa bila kuzingatia maslahi ya Taifa na aliyependekeza wajumbe kwa mamlaka ya uteuzi aliangalia zaidi mambo binafsi na kuzingatia urafiki, undugu na kusoma pamoja ukilenga kupata maslahi binafsi zaidi ya Taifa.
Kumsaidia Mh Rais katika vita dhidi ya ufisadi, ni vyema mamlaka za uteuzi wa wajumbe wa Bodi za Mashirika na Taasisi za umma kuwa makini katika uteuzi wao. Ni vizuri wakakumbuka kuweka mbele utaifa, uzalendo, sifa za mjumbe, uwezo na uwakilishi kitaifa.
Sehemu zote za nchi zina watu wenye sifa zinazostahili, siyo kitu kizuri watu kufanya kazi ya Taifa kama ya familia kwa kuwa na watu wa aina moja na wenye nia moja hasa ya kulihujumu Taifa.