Wanaojiita BAKWATA Arusha ni mavuvuzela?

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Habari za uhakika kutoka uongozi halali wa BAKWATA Arusha na Mufti Mkuu Dar, zinasema waliolaumu Chadema na kutambua Meya wa Arusha ni BAKWATA vuvuzela. Siyo viongozi halali wa BAKWATA, ni wahuni watoto wa familia moja ya mzee Mkindi ambao wamekula dili na ccm na polisi
 
Jamani CCM naivulia kofia wanavyohangaika na matamko toka UDOM hadi kwenye nyumba za ibada na sasa nasikia wanataka kuhonga maiti sijui isije NMC kweli kiboko, hii yote ni laana inayowaandama usiku kucha ya wizi wa kura, na wasipotubu itawamaliza, angalia hata humu siku hizi wameanza kupungua na wengine kugeuka.
 
nani kasema define fufuzela ni nani na vuvuzela ni nani?
 
Hivi kule sijui wapi sijui singida nimesikia eti sijui askofu anasema sijui watu wanatumwa kufanya fujo sijui wawe busy na shughuli fujo haziwezi kufanyika, ivi yule mgeni rasmi sijui mama nani vile? ni mbunge. Je ni wa chama gani? Anadai eti Kikwete angefanya vizuri sana kama watu waliotumwa wasipofanya fujo. Naomba mnisaidie ivi ni nani huyo alietumwa? sijamuelewa.
 
Inawezekana kabisa kwani nashangaa kiwango cha uchambuzi na tamko lililofanywa na hao wanaojiita BAKWATA ARUSHA. Wamedhihirisha wametumia ushabiki zaidi kuliko kufikiri . Shame on them, hizi rushwa zitatufanya hata kukana wanetu jamani
 
Jamani CCM naivulia kofia wanavyohangaika na matamko toka UDOM hadi kwenye nyumba za ibada na sasa nasikia wanataka kuhonga maiti sijui isije NMC kweli kiboko, hii yote ni laana inayowaandama usiku kucha ya wizi wa kura, na wasipotubu itawamaliza, angalia hata humu siku hizi wameanza kupungua na wengine kugeuka.

CCM sasa wananena kwa lugha.

kila mtu anawasiliana na shetani kivyake. hakuna anayemuelewa mwenzake.

kweli chadema kiboko!!!!
 
huu upepo wa chadema umewavuruga kabisa ccm kila m2 analopoka vyake ,akiaribu kesho katibu wa chama anatoa tamko hatujamtuma ni maoni yake binafsi..na wenye njaa nao hela ya kahawa tu na ugolo nao wanatoa matamko yasiyo na mashiko..nimeukubali upepo huu wa chadema na mabadiliko.
 
hivi hawa chama cha mauaji (CCM) wakikubali kushindwa tatizo liko wapy,ni ulafi tu,pambaaaaaf sao
 
Chanzo cha habari tafadhali.

Hivi chanzo maana yake nini? Nakuambia it is confirmed, na nimekutajia shehe mkuu wa arusha na mufti mkuu dar. Unataka nini zaidi? Au mpaka gazeti Fulani liandike? Au mwanasiasa aseme? Akidanganya je?
 
CCM sasa wananena kwa lugha.

kila mtu anawasiliana na shetani kivyake. hakuna anayemuelewa mwenzake.

kweli chadema kiboko!!!!

Things fall apart, center is unable to hold. Natamani mwandishi mmoja angekusanya kauli mbali mbali za viongozi wa serikali na ccm kwa mwezi huu wa January peke yake. You will get a very interesting picture
 
Hivi kule sijui wapi sijui singida nimesikia eti sijui askofu anasema sijui watu wanatumwa kufanya fujo sijui wawe busy na shughuli fujo haziwezi kufanyika, ivi yule mgeni rasmi sijui mama nani vile? ni mbunge. Je ni wa chama gani? Anadai eti Kikwete angefanya vizuri sana kama watu waliotumwa wasipofanya fujo. Naomba mnisaidie ivi ni nani huyo alietumwa? sijamuelewa.

uandishi wako bwana, kama unajua kitu kama haujuhi
 
fufuzela ni CCM, na vuvuzela ni waislam feki walihongwa hela chafu zinazonuka damu watoe tamko kumtambua Meya.
Huu upuuzi wa kuingiza dini ya watu kwenye upuuzi sikubaliani nayo. Uislamu ni dini sawa na ukristo pia nina uhakika wakristo na waislam safi wanajua ukweli wa kinachoendelea ndani ya nchi yetu na wanaiunga mkono CHADEMA kwa sababu kinasimamia ukweli na wala si vinginevyo!

Wanaotapatapa kwenye CCm watatumia njia zote kujitambulisha kwa dini wakitarajia kusaidiwa na dini lakini hawataweza maana hakuna dini inayokumbatia wizi, utapeli, ung'ang'aniaji wa madaraka, ubabe na ufisadi.
 
"Center Bolt" ya CCM.....imekatika na sasa gari laenda upandeupande, hala hala abiria ndani ya gari hilo kaeni chonja.
 
Jamani, nilichelewa kuona taarifa hii hapa ya BAKWATA. Mbona aibu ya mwaka kwa CCM!! Aibu hii yote wenzetu CCM watapeleka wapi uso wao mbele ya jamii ya Tanzania?

Kwa siku za jirani kidogooo naona nyota kutoka mashariki na inasema hivi kwamba wajumbe wengi ndani ya bunge hili karibia watashinikizwa na wapiga kura wao ama wakihame hili jahazi MV UFISADI linalozama kwa uongo na janja za nyani kwa jamii na kwamba wasiposikia sauti hizo kwa wakati mwafaka na basi wabakie wazame nayo.

Pia kwa mitaji hii ya mikashfa mizito mizito nchini kama vile Maruani Dowansi, EPA, MEREMETA, Mauaji ya Kinyama Arusha, Rushwa kwa familia ya Marehemu Ismael, 'BAKWATA' wa Kukodisha Arusha, 'Diwani wa Kuchonga' Chatanda, na Uchakachuaji wa Uchaguzi Mkuu, dalili zote zinaonyesha ya kwamba sehemu kubwa ya Wabunge wa CCM Uadilifu watapiga kura za chuki dhidi ya CCM Kikwete na kupitisha muswada wananchi kujiandikia wenyewe katiba mpya bila udalali.

Hiyo CCM Kikwete ambayo wabunge wengi wataiasi bungeni Dodoma sawa sawa na jinsi ambavyo mawaziri wengi tayari wamekwishaonyesha njia, wakati mwingine hujulikana kama CCM UFISADI aka Wanamtandao / Wachacharikaji / CCM Rostam Aziz ambao husemekana kwamba ndio walioufadhili mauaji ili kututisha wananchi tusiendelee kuwabana kwenye katiba mpya amba mpaka sasa imewafanya waitwe CCM Chama Cha Mauaji.

Kitakachowasambaratisha ambayo tayari imeshaondo madiwani 3 nchini kutofungamana na hiki kikundi ni HOFU KUBWA YA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YENYE DAMU MIKONO YOTE wakati utamaduniwa Ki-Tanzania hata siku moja haivumili sura ya kumwagana damu katika jamii yetu yenye upole, na ustaarabu katika haki.
 
Nadhani ushiriki wa mashehe wa bakwata wa ukweli kwenye mazishi leo na kauli Yao umedhihirisha ukweli jinsi ccm inavyotumia dini kuchonganisha watz
 
Back
Top Bottom