Wanaoisema vibaya serikali mitandaoni kukiona

Wanaoisema vibaya serikali mitandaoni kukiona

ok, Huyu Masauni anafahamu katiba ya Jamhuri ya muungano au anatumia katiba ya Zanzibar?

Mwambieni huku bara katiba inaruhusu watu kuongea wanachotaka bali wasivunje sheria, Mwambieni Zanzibar watu wa huku bara wanatubania ardhi ya kujenga

Mwambie Masauni kuna mambo ya msingi ya kuelimisha watu wake kama PGO, Atumie muda kuwaelekeza watu wake mambo ya PGO na kutenda haki

Mwambieni Masauni awe anasikiliza kauli za Rais kuwa Jeshi la polisi lishughulike na mambo yake ya msingi wasitoke kwenye lengo la kuanzisha Jeshi la polisi

Hivi watu bado hawakujifunza awamu ya sita ya JPM kuwa haya mambo yalitengeneza chuki mpaka kwa mara ya kwanza watanzania wakaanza kufurahia vifo vya viongozi wa kisiasa

Hapa JF tu watu walitoa kauli za kuombea Viongozi wafe kwa korona. Na viongozi waliokufa watu walishangilia

Angekuwa mkristu masauni ningesema kwanini Wagalatia mna roho ngumu na mmeweka pamba masikioni

Sasa huyu ustadh Masauni ameshaanza kupandisha mabega tena, Naona Masauni Mabega yameanza kupanda sasa

Tumkumbushe masauni alikuwepo Kangi Lugola yeye alivaa mpaka bendera ya Taifa na alitembea na ilani mitaani kama anaeneza injili

Hiyo wizara Kangi Lugola alishona suti zenye Rangi ya bendera ya Taifa

Ni muhimu viongozi wakakumbuka nchi imepita wakati gani

Hawa watu mambo yakiwa magumu wanaanza kuwalilia viongozi wa dini wawashauri wananchi

Masauni aache viongozi wa dini wapumzike, Tumechoka na makongamano ya Amani kila wakati na upatanisho wa kisiasa

Rais alishasema watu waongee, Yeye ameshajisahau anaingilia mamlaka ya Rais
SURATI%20ZUBAA%20%20Ndio%20surati%20zubaa%2C%20pengine%20tumesomewa%2C%20Sivyo%20tusingebung'a...jpg
 
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh Hamad Masauni , amewaonya wale wote wanaoisema vibaya serikali ya awamu ya 6 Mitandaoni , ambapo ameliomba jeshi la Polisi kuimarisha mifumo yake (ya utambuzii) kwa kushirikiana mamlaka zingine ili kukomesha jambo hilo .

Mh Waziri ameyasema hayo wakati wa kumkaribisha Mh Rais Samia Suluhu Hassan ili kufungua Kikao cha viongozi wa Polisi Mkoani Kilimanjaro .

Kazi Iendeleeee .
Alisemwa Trump na wengineo kibao sembuse! Waacheni wananchi walio na maone wawaambie ili mjirekebishe akusemae anakurekebisha wakikaa kimya mnaharibu zaidi.
 
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh Hamad Masauni , amewaonya wale wote wanaoisema vibaya serikali ya awamu ya 6 Mitandaoni , ambapo ameliomba jeshi la Polisi kuimarisha mifumo yake (ya utambuzii) kwa kushirikiana mamlaka zingine ili kukomesha jambo hilo .

Mh Waziri ameyasema hayo wakati wa kumkaribisha Mh Rais Samia Suluhu Hassan ili kufungua Kikao cha viongozi wa Polisi Mkoani Kilimanjaro .

Kazi Iendeleeee .
Mwambie Mungu pekee ndo tunamwogopa, mwanadamu lazima akosolewe.

Akiwa kiongozi na akanuka RUSHWA na WIZI, lugha ngumu lazima itumike.

Amen.
 
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh Hamad Masauni , amewaonya wale wote wanaoisema vibaya serikali ya awamu ya 6 Mitandaoni , ambapo ameliomba jeshi la Polisi kuimarisha mifumo yake (ya utambuzii) kwa kushirikiana mamlaka zingine ili kukomesha jambo hilo .

Mh Waziri ameyasema hayo wakati wa kumkaribisha Mh Rais Samia Suluhu Hassan ili kufungua Kikao cha viongozi wa Polisi Mkoani Kilimanjaro .

Kazi Iendeleeee .
Kwa hiyo wanataka sote tuwe waimba mapambio, wakamuulize Magufuli pamoja na ubabe wake tulimsema mpaka akajitosa kwenye covid 19
 
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh Hamad Masauni , amewaonya wale wote wanaoisema vibaya serikali ya awamu ya 6 Mitandaoni , ambapo ameliomba jeshi la Polisi kuimarisha mifumo yake (ya utambuzii) kwa kushirikiana mamlaka zingine ili kukomesha jambo hilo .

Mh Waziri ameyasema hayo wakati wa kumkaribisha Mh Rais Samia Suluhu Hassan ili kufungua Kikao cha viongozi wa Polisi Mkoani Kilimanjaro .

Kazi Iendeleeee .
huyu alifoji nyaraka za umri wake huyu...atulie kwanza
 
Wakitimiza majukumu yao hakuna atakayewasema vibaya, lakini wasipotekeleza wajibu wao tutawakumbusha, na kuwakumbusha sio kuwasema vibaya, by the way ukifanya mazuri, utasemwa kwa mazuri yako, ila pia ukifanya mabaya....
Definition ya kuisema vibaya ni kusema vipi ?? Kutumia maneno yepi ? Ni muhimu kufahamishana !
 
Mmesikia nyie

Tangazo hilo

Ova
Tangazo limesikika,je tunasonga mbele au tunarudi nyuma kama jibu ni ndio kwenye maeneo Gani? Na kama jibu ni hapana kwenye maeneo Gani? Je Kwa jibu lolote nini kifanyike Kwa maana ya kuboresha ama kurekebisha mapungufu yetu."Kwani hata maandiko yanasema pindi watu wangu wakinyamazishwa hata mawe yataongea"Ama tunachosubiri ni mawe yaongee 🤔
 
nibsawa watu wasitukane tu na kuvunja sheria ila kusema ukweli tutasema.
mkipiga lesa tutasema
mkicheza rafu tutasema
habari za kusema ohh serikali isisemwe msitufundishe uoga
huyo waziri angejua ni ugonjwa kuisifia serikali ambayo haifanyi vizuri asingeropoka huo ujinga
 
Back
Top Bottom