Wanaoipinga CCM ni kosa kukimbilia nje ya nchi?

Wanaoipinga CCM ni kosa kukimbilia nje ya nchi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,146
Reaction score
48,386
Kuna mzaha hufanywa na baadhi ya watu dhidi ya wanasiasa wanaoipinga CCM wanapokimbilia nje ya Tanzania.

Kuna hoja kwamba huwezi kupigania maslahi ya Tanzania na watanzania ukiwa nje ya Tanzania. Na wengine hufika mbali zaidi kwa kuwaita watu hao ni vibaraka wa mabeberu.

Lakini Historia ya Tanzania imejaa orodha ya watu waliokimbilia Tanzania wakati wanapigania haki kwenye nchi zao.

Mtu kama Eduardo Chivambo Mondlane, Samora Moises Machel na wenzao wa FRELIMO walikimbia kwao Msumbiji na kuja Tanzania wakiwa wanapigania uhuru wa nchi yao.

Viongozi kadhaa waandamizi wa Pan Africanist Congress (PAC) na African National Congress(ANC) waliwahi kupewa hifadhi ya kisiasa Tanzania pamoja na kupewa mafunzo ya kijeshi Kwa vijana wao kwenye makambi mbali mbali yaliyokuwa hapa nchini.

Watu kama Milton Obote wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Nelson Mandela wa Afrika ya Kusini na watu wa aina ya Laurent desire Kabila, kwa nyakati tofauti waliwahi kupewa hifadhi hapa Tanzania wakati wanapigania nchi zao.

Wakati huo wale tuliowapokea walikuwa wanakuja Tanzania kwa kuwa sisi ni mabeberu? Kwa nini hatukuwarudisha kwenye nchi zao ili wapambane wakiwa kwao?

Nahisi CCM Sasa inaongozwa na watu wasioijua kabisa historia ya chama chao.

Wakulaumiwa ni kina Pascal Mayalla na johnthebaptist ambao hawawafundishi vijana wao (Uvisisiemu) historia ya nchi hii.

Leo hii rafiki yake johnthebaptist Marehemu Hashim Mbitta akifufuka ataishangaa CCM hii ya zama hizi. Atadhani labda ni chama cha makaburu ila sasa kinaongozwa na watu weusi.
 
Jujipanga kwa mapambano ni mbinu ya kushinda pambano lenyewe,au?
Retreat and going Back to the drawing board.

CCM ya Sasa haina wale Watu kama waliokuwepo wakati Pius Msekwa akiwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kulikuwa na watu kama kina Kanali Mhando ambao walikuwa wakisema wanakuwa wamesema. Alipokuja Kikwete chama kikamong'onyoka na Magufuli akaubomoa kabisa hata ule mfumo dhaifu ulioachwa na Kikwete.
 
Back
Top Bottom