Wanangu na nyie mtazaa tu

Wanangu na nyie mtazaa tu

Hahahahahhaaaa nimecheka kisa chenu na mdogo wako,hasa hapo mlipopata guts za kufunga mlango kwa nje.

Mdogo wako nae ana mtoto?

Jaribu kupata watoto wengine watapunguza makali ya utundu wa mtoto wa kwanza.

Out of Topic: sijui kwa nini nikikuona namkumbuka TIZED.

Kasie.
Hahaha mdogo wangu bado hana mtoto.

Kuhusu hiyo out of topic, nadhani kwasabau natumia picha ya Ben Carson thats why unamkumbuka Tized. Sijui yuko wapi, amekuwa kimya sana.
 
pole sana mkuu. ninachoshukuru ni kwamba mlifanya makosa na mkamkwaza.

mama yangu mimi alikuwa anatamka laana tu hata km umekosea kitu cha kitoto kabisa.
anatunyima chakula,
kipigo tena uchi wa mnyama.
miaka inakatika chakula ni ugali na mchicha..ila yeye bia kwa sana... yani mama yako mzazi anakuchukia saaana! bila kosa. RIP mama I love you.
Duh!
Huyu maza itakuwa alikuwa na masaibu yanamfikia hana Wa kumexpress so machungu yanahamia kwa kids..lazima maza alikuwaga anapita magumu sana maana sio rahisi mamaza kuwa wakuda to that extent
 
Nimewaza hivyo
Analyze na Tized wana mfanano fulani hivi, halafu kwenye story telling namuona mentor kwa analyze.....
Tized yu wapi Kasie? Alikuwa mshikaji sana kwenye I'd yangu ile kongweee yenye majanga siitumii tena...
Hahahahahhaaaa nimecheka kisa chenu na mdogo wako,hasa hapo mlipopata guts za kufunga mlango kwa nje.

Mdogo wako nae ana mtoto?

Jaribu kupata watoto wengine watapunguza makali ya utundu wa mtoto wa kwanza.

Out of Topic: sijui kwa nini nikikuona namkumbuka TIZED.

Kasie.
 
ni kweli mkuu mara baada ya kutuzaa mahusiano na ndugu zake yalitetereka sana..

wali.fukuza nyumbani na hawakumpenda tena...
Duh!
Huyu maza itakuwa alikuwa na masaibu yanamfikia hana Wa kumexpress so machungu yanahamia kwa kids..lazima maza alikuwaga anapita magumu sana maana sio rahisi mamaza kuwa wakuda to that extent
 
Hahahahahhaaaa nimecheka kisa chenu na mdogo wako,hasa hapo mlipopata guts za kufunga mlango kwa nje.

Mdogo wako nae ana mtoto?

Jaribu kupata watoto wengine watapunguza makali ya utundu wa mtoto wa kwanza.

Out of Topic: sijui kwa nini nikikuona namkumbuka TIZED.

Kasie.
Unamkumbuka tized sababu ya avatar
 
Halafu akishatema mate chini? What next?
Kuna mtoto wa ndugu yangu alimwambia mama yake ‘fuc.k you’ baada ya mama anayemsomesha nje ya nchi anamlipia hata hicho chumba alichomkuta amelewa chakali! Tema mate chini ndugu yangu
 
pole sana mkuu. ninachoshukuru ni kwamba mlifanya makosa na mkamkwaza.

mama yangu mimi alikuwa anatamka laana tu hata km umekosea kitu cha kitoto kabisa.
anatunyima chakula,
kipigo tena uchi wa mnyama.
miaka inakatika chakula ni ugali na mchicha..ila yeye bia kwa sana... yani mama yako mzazi anakuchukia saaana! bila kosa. RIP mama I love you.
 
Wakati dingi anatwambia hii kauli mimi na mdogo wangu, hapo alikuwa amevimba kwa hasira akiwa hana cha kufanya.

Nakumbuka enzi hizo na mdogo wangu, mimi nikiwa kidato cha nne, mdogo wangu akiwa cha 3. Tulikuwa watundu japo sio watukutu. Kuna siku tuliondoka home bila kuaga, alaf kuna kazi tuliambiwa na mshua tuifanye ila tukasahau.

Tulirejea nyumbani majira ya saa kumi na moja kosoro jioni, njaa kali hatukuwa tumekula kitu tokea asubuhi. Kufika home, mzee alitugombeza sana, alafu akasema kwavile tumeona tumeshakua basi hataki tena kutuona nyumbani, akatusukumizia nje kisha akafunga mlango. (Hapo kumbuka tuna njaa ya hatari na home hawakutuwekea chakula siku hiyo).

Tulikaa pale nje, njaa kali. Nyumba yetu ilikuwa imezungukwa na midizi, na uzuri kulikuwa na ndizi mbivu zimeiva, faza alisema angezitoa jioni. Tulipoona mkungu bado upo, tukakubaliana na dogo tule zile ndizi. Dogo akaenda kufunga ule ule mlango ambao baba alitufungia kwa ndani, dogo akaufunga kwa nje ili kumdhibiti mzee endapo atataka kutoka.

Tulijitahidi sana kuukata taratibu ule mgomba walau usitoe kishindo chochote, ila dingi kwavile alizijua akili zetu, naona machale yakamcheza, ghafla akaja. Kufila mlango anakuta mlango umefungwa kwa nje, kuja kuchungulia kwenye dirisha la jikoni anatukuta vidume tunaushambulia ule mkungu bila wasiwasi.

Alitwangalia pale dirishani, mwishowe akatwambia "Na nyie mtazaa tu"

Siku ikaisha, miaka mingi ikasogea. Sasa hivi nina mtoto wa kiume mkubwa tu, umri miaka 5 anaishi kwa babu na bibi yake (wazazi wangu). Kwavile mimi niko mbali, huwa nina kawaida ya kumpigia simu na kuongea nae mara kwa mara.

Last week nimekaa sehemu na rafiki zangu, nikaona ngoja nimpigie baba ili niongee na mwanangu, nikaongea nae vizuri tu huku nikijaribu kumuuliza mambo kadhaa kadhaa ya shule. Katika kuendelea kuuliza, ghafla dogo akaniambia "BABA UNAMASWALI SANA , PUMBAVU WEE" kasauti kake kalisikika na wote waliokuwa karibu na mimi pale, na upande wa pili nikasikia bibi yake anakachapa. Nikakata simu.

Baadae faza akanipigia simu, akaniambia "mwanangu nilikwambia na wewe utazaa tu". Sikumjibu,nilikaa kimya tu, then tukaendelea na story zingine.

Dah, haya mambo aisee.

Analyse.
😂🤣🤣🤣🤣 kweli na nyie mtazaa tu hata ipite miaka mingapi
 
Back
Top Bottom