Wanangu na nyie mtazaa tu

Wanangu na nyie mtazaa tu

Kwa hiyo aliacha kabisa tabia ya kujibu vibaya?
We acha msoto wa miezi sita na hata vimchepuko vilivyokuwa vinampa jeuri vikamkimbia! Mama yake kwa vile alikuwa soja alimkomesha kweli kweli mpaka kuomba msamaha! Unajua usingo maza unahitaji mtu aliye Tafu. Sasa ana adabu na yupo mwaka wa mwisho na GPA nzuri tu
 
pole sana mkuu. ninachoshukuru ni kwamba mlifanya makosa na mkamkwaza.

mama yangu mimi alikuwa anatamka laana tu hata km umekosea kitu cha kitoto kabisa.
anatunyima chakula,
kipigo tena uchi wa mnyama.
miaka inakatika chakula ni ugali na mchicha..ila yeye bia kwa sana... yani mama yako mzazi anakuchukia saaana! bila kosa. RIP mama I love you.
 
Hahahahahhaaaa nimecheka kisa chenu na mdogo wako,hasa hapo mlipopata guts za kufunga mlango kwa nje.

Mdogo wako nae ana mtoto?

Jaribu kupata watoto wengine watapunguza makali ya utundu wa mtoto wa kwanza.

Out of Topic: sijui kwa nini nikikuona namkumbuka TIZED.

Kasie.
 
NA WEWE LISTORY REEFU PMBV WE.

Joke
Wakati dingi anatwambia hii kauli mimi na mdogo wangu, hapo alikuwa amevimba kwa hasira akiwa hana cha kufanya.

Nakumbuka enzi hizo na mdogo wangu, mimi nikiwa kidato cha nne, mdogo wangu akiwa cha 3. Tulikuwa watundu japo sio watukutu. Kuna siku tuliondoka home bila kuaga, alaf kuna kazi tuliambiwa na mshua tuifanye ila tukasahau.

Tulirejea nyumbani majira ya saa kumi na moja kosoro jioni, njaa kali hatukuwa tumekula kitu tokea asubuhi. Kufika home, mzee alitugombeza sana, alafu akasema kwavile tumeona tumeshakua basi hataki tena kutuona nyumbani, akatusukumizia nje kisha akafunga mlango. (Hapo kumbuka tuna njaa ya hatari na home hawakutuwekea chakula siku hiyo).

Tulikaa pale nje, njaa kali. Nyumba yetu ilikuwa imezungukwa na midizi, na uzuri kulikuwa na ndizi mbivu zimeiva, faza alisema angezitoa jioni. Tulipoona mkungu bado upo, tukakubaliana na dogo tule zile ndizi. Dogo akaenda kufunga ule ule mlango ambao baba alitufungia kwa ndani, dogo akaufunga kwa nje ili kumdhibiti mzee endapo atataka kutoka.

Tulijitahidi sana kuukata taratibu ule mgomba walau usitoe kishindo chochote, ila dingi kwavile alizijua akili zetu, naona machale yakamcheza, ghafla akaja. Kufila mlango anakuta mlango umefungwa kwa nje, kuja kuchungulia kwenye dirisha la jikoni anatukuta vidume tunaushambulia ule mkungu bila wasiwasi.

Alitwangalia pale dirishani, mwishowe akatwambia "Na nyie mtazaa tu"

Siku ikaisha, miaka mingi ikasogea. Sasa hivi nina mtoto wa kiume mkubwa tu, umri miaka 5 anaishi kwa babu na bibi yake (wazazi wangu). Kwavile mimi niko mbali, huwa nina kawaida ya kumpigia simu na kuongea nae mara kwa mara.

Last week nimekaa sehemu na rafiki zangu, nikaona ngoja nimpigie baba ili niongee na mwanangu, nikaongea nae vizuri tu huku nikijaribu kumuuliza mambo kadhaa kadhaa ya shule. Katika kuendelea kuuliza, ghafla dogo akaniambia "BABA UNAMASWALI SANA , PUMBAVU WEE" kasauti kake kalisikika na wote waliokuwa karibu na mimi pale, na upande wa pili nikasikia bibi yake anakachapa. Nikakata simu.

Baadae faza akanipigia simu, akaniambia "mwanangu nilikwambia na wewe utazaa tu". Sikumjibu,nilikaa kimya tu, then tukaendelea na story zingine.

Dah, haya mambo aisee.

Analyse.
 
Mimi niliwaambiwa wadogo zangu wa kiume kuwa kina siku nao wataoa...

Mimi ni mkubwa kwetu na katika hao madogo, niliwasomesha kwa hela yangu. Na wakawa wanakuja home lakini malalamiko na shemeji yao yakawa ndo wimbo wa taifa. Walipoanza kuoa mmoja baada ya mwingine nikawaambia sasa mnao, YAKUMBUKENI MALALAMIKO YENU YA ZAMANI.... walirudi kuja kusema kweli kuoa ni KIPAJI
 
Pole mkuu

Nimejaribu kuvaa uhusika wa mtoto wangu kuniambia pumbavu nimefeel maumivu...pole sana
Hivi ni mm peke yangu ambae huwa nadhaniaga ww ni Me, maana kila nikiiiona avatar yako na hilo jina huwa sishtukagi....haha

Uskute hapo we ni mlimbwende mkareeeee hatari
 
Tuliwahi ambiwa mimi na kaka yangu hatutalala ndani kwa kuwa tulitoka shuleni hatukufanya kazi nikiwa darasa la 5 na kaka la 6 kweli bi mkubwa kama saa tatu tunamuaga tunaenda kulala akasema mnadhani nimesahau? tokeni nje akatufungia nje ilikua kama saa 4 kasoro hivi. Tukafungua zetu banda la kuku, kwa kijijini enzi hizo mlango wa banda ulikua panawekwa tu jiwe kubwa mradi tu mbwa asiweze ingia ndani, baada ya kama nusu saa akafungua mlango akaanza kututafuta tena ameita wee sisi kimya na tunamsikia vizuri. Alipokwenda kwa jirani na sisi tukatoka bandani na kuingia chumbani tukalala, aliporudi anakuta tupo ndani tukaambiwa ngoja kukuche atatuchapa ila hakuna kilichotokea. I love you mama
 
Back
Top Bottom