Wanandoa kutumia tendo la ndoa kama silaha ni ujinga

Wanandoa kutumia tendo la ndoa kama silaha ni ujinga

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,544
Reaction score
6,304
Kuna wanandoa wanaishi maisha ya ajabu sana mathalani unaweza ukamkuta mwanamke anatumia tendo la ndoa kama sehemu ya kujihami na kufikishia hisia zake kwa mumewe Mara kwa Mara na kuna wakati anaamua hata kumnyima mwenzi wake anapohitaji ili mradi tu aweze kufikisha hoja yake mezani. Hii ni kwa pande zote lakini upande wa dada zetu ukifuatilia utagundua kuna tofauti. Kufanya hivyo ni utoto wa tafakuri na kujiharibia taratibu, ni kama kujilipua mwenyewe.

Unamkuta mtu hakuambii chochote ila mkiwa kwenye burudani anakuibulia hoja ya ajabu inayofikia hatua ya kuharibu kabisa mkururo wa hisia za raha Kiswahili cha mitaani wanasema "anakukata stimu" huu ni ujinga mkubwa sana kama ukiendelezwa ni rahisi sana wanandoa kuchokana na kutofurahia tendo la ndoa ambalo ni zawadi yao wote.

Tubadilike zama zimebadilika sana.
 
kumbe ndo mambo yako hivyo duh!
 
kumbe ndo mambo yako hivyo duh!
Kaka usiombe ndoa zimeficha mengi.
Mazowea na kuzowean sana bila mipaka huponza wengi.
Use Mwanamke au Mwanandoa ndani ya ndoa au nje ya ndoa mazowea yasiyo na mipaka ni bomu
 
Mwanamke akianza mikwara ya namna hiyo, tayari kuna shida.
Mwingine unakuta anaona ni kamtindo kakufikishia hoja zake mfano unapokuwa naye pale unapohisi upo juu sana unasikia "deaar halafu hujawahi kuninunulia nguo nzuri ya Siku kuu tangu mwaka huu uanze halafu MTU anakomaa umjibu hapo hapo kabla ya....aaaagh..oyoooo...
 
Akikatiza tendo na kuleta mada za kijinga naachia kati naenda kuoga, navaa fresh naenda kuangalia tv au kama ni mchana natoka kidogo.

Mda wa kazi ni kazi sio kuibua mada za kijinga.
 
Biblia imeandika kuwa "Wanaume wanapaswa kuishi na wake zao kwa AKILI"
Wanawake wao waliambiwa "tiini waume zenu"suala la msingi ni kuelewa wajibu wa kila mmmoja na mipaka ya kila mmoja
Mwanamke kutii kulikoandikwa siyo kutii mpaka upumbavu ndiyo maana biblia imeandika muwe na kiasi,wapole kama huwa na wajanja kama nyoka.
Akina Baba kuishi kwa akili ni kulikoandikwa ni kule kunakomtanguliza Mungu na kuomba hekima na Busara kama kichwa cha familia siyo kutegemea akili zako tu bila kuomba msaada wa Mungu.
 
Kama kila Siku mkianza kufanya anaanza kuleta hoja mbali mbali dawa yake unamaliza shida zako huko pembeni ukija home hufanyi ili akose nafasi ya kuleta hoja

Ila sipo sirias saana
Mimi pia mwanamke akileta hizo mambo zake nitakuwa namkomesha.[emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom