Wananchi wilaya ya Ludewa wazuia msafara wa Zito Kabwe - Aeleze sababu za kusuasua mradi madini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
IMG_2884.JPG


WANANCHI wa Kijiji cha Mkomang'ombe Wilaya ya Ludewa, mkoani Iringa, juzi waliuzuia msafara wa wajumbe wa Kamati ya Bunge na Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (POAC) kuondoka kijijini hapo hadi waelezwe sababu ya kusuasua kwa miradi ya Mchuchuma na Liganga.

Kamati hiyo ambayo mwenyekiti wake ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA) ililazimika kuwatuliza wananchi hao waliokusanyika kando ya barabara ya Mkomang'ombe na Ludewa kuanzia majira ya saa 7 baada ya msafara huo kwenda umbali wa kilometa zaidi ya 50 na kuamua kurudi eneo hilo ili kuwasikiliza wananchi hao.

Akiihoji kamati hiyo kwa niaba ya wenzake mkazi wa kijiji hicho Augustino Haule alisema toka mchakato wa mradi huo wa Mchuchuma na Liganga uanze ni zaidi ya miaka 10 sasa ila hakuna jipya zaidi ya ahadi za serikali zisizotekelezwa na kutaka kujua sababu ya kudanganywa na serikali ni zipi na kwa faida ya nani.
Alisema sababu ya wao kushinda eneo hilo wakisubiri msafara huo ni kutaka kupata ufafanuzi wa majibu ya maswali yao.

"Kweli tumefurahi sana kukutana na kamati hii chini ya Mbunge mchahari Kabwe ….tumekuwa tukikusikia na kukuona katika TV pekee ila ukweli sisi wananchi tunakupenda sana na tuko nyuma yako tena tunaomba uongeze ukali zaidi wewe na chama chako CHADEMA kisonge mbele …," alisema mwananchi huyo huku akishangiliwa na wananchi wenzake.

Akijibu maswali ya wananchi hao Kabwe alisema kamati hiyo imefika katika kijiji hicho kwa ajili ya kuona mali iliyoko katika eneo hilo na jinsi inavyotumika.
Kabwe alisema ni kweli kamati nyingi za Bunge na viongozi wa serikali wamepata kufika hapo na kuendelea kutoa maneno matamu juu ya miradi hiyo hali ambayo wananchi tayari wameonyesha kuchoka kusikia utamu wa maneno hayo na kutaka vitendo katika utekelezaji wa miradi hiyo.

"…Hicho ndicho cha kwanza kabisa kilichofanya kamati hii kwa kuanzia kuja huku kwenu (Ludewa) kuona miradi hii ili iweze kuanza kwa wakati …Makamu Mwenyekiti wa Kamati hii ni mbunge wenu tena anawatetea vema na sisi tukasema tuanze huku ila lengo letu ni kuwatetea na kuona miradi hiyo inaanza kufanya kazi na kuwa kamati hii haitaki tena maneno katika utekelezaji wa miradi hii…tunataka ndani ya kipindi chetu cha miaka miwili na nusu miradi hii ianze kufanya kazi," alisema Kabwe.
Alisema serikali na Bunge ina nia nzuri ya kuona miradi hiyo inatekelezwa ili kuhakikisha wananchi wananufaika zaidi.
Source: Tanzania Daima
 
Back
Top Bottom