Wananchi wenye hasira kali ni sheria?

Kiroroma

JF-Expert Member
Feb 6, 2009
370
114
Hapa sijaelewa,Mwananchi mmoja huko Lindi aliuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kukutwa akiiba kuku!
Mambo haya yamezoeleka tuu , kwani Kamanda wa Polisi amesema kirahisi tu kuwa " polisi wamethibitisha ameuwawa na wananchi wenye hasira kali".Sasa swali langu ni mmoja kama hasira kali za wananchi zinatawala utawala wa sheria basi hata watuhumiwa wa EPA,Rada,Richmond,na wahujumu uchumi wengine watoswe basi tuwamalize kwa hasira kali za wananchi!!Iweje wao wasalimike vibaka roho zao zilinganishwe na thamani ya kuku?
 
Hakuna cha hasira kali ni unafiki na laana tunayoiendekeza.Kama tungekuwa na hasira kali,Lowassa asingepokewa kwa shangwe jimboni kwake,Rostam na wahindi wenzake wasingeendelea kutuibia.matokeo yake unasubiri mtu aitiwe mwizi unaanza kupiga wakati hujui alichoiba.Huu ni wendawazimu
 
Vitendo hivi vimezidi sana na wahanga wake ni watu maskini wenye njaa na wasio na njia halali za kujipatia kipato.Utawala wa sheria uko wapi kama hawa walitegemea maisha bora sasa wanambulia bora maisha?Huku mkono wa wananchi wenye hasira ukielekezwa kwao kuhitimisha safari zao za maisha ili hali wale wenye kukwapua mabilioni na mabilioni ya watz wakipeta na kupigiwa shangwe na hoi hoi!!!!
 
Back
Top Bottom