Wananchi wengi wajitokeza kuiaga CCM

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,943
3,819
Sio siri tena ,wananchi wengi hujitokeza kuiga CCM kwa sherehe ,sherehe ambazo zinatokea kwa kufanywa matamasha ya muziki,asie na mwana abebe jiwe kumuona Raisi wa mwisho wa CCM, muungano wa vyama viwili vilivyotupatia uhuru.

Wengi wakisema mwaka huu kila kitu ni historia hivyo kushiriki kwake kunawekezeka katika kizazi kijacho,kuwa na Chama tawala kipya katika historia ya Tanzania vilevile kukiaga chama kikongwe wakisema kikapumzike kwani kimetutoa mbali sana na kutujengea madaraja,reli na kutuletea ndege ambavyo hatukuwa navyo kabla na hata baada ya miaka 40 ya uhuru.

Kwa hiyo muonekano wa wanaohudhuria kila upande ni muitikio mkubwa sana,upande mmoja unaagwa na upande mwengine unakaribishwa na kupokewa kwa matumaini mapya ya kizazi kipya cha Kitanzania.
Hongera Chadema hongera CCM hongera Saint Tundu Lissu hongera Magufuli yapo maisha baada ya uchaguzi kama raisi mstaafu mbona wapo wengi.
 
wasanii wa CCM waikimbia CCM dakika za mwisho ,upepo sasa unavumia kwa Tundu Lisu,CCM si shwari tena.
 
Back
Top Bottom