Wananchi wengi sana wanaojitokeza katika ziara za Rais Dr Magufuli na kumshangilia zinatoa picha gani kiutawala

Ukijaribu kufuatilia ziara za Rais Magufuli ndani ya nchi na msafara wake wananchi wengi sana wanajitokeza kila kwenye kijiji au miji midogo iliyopo kanda ya barabara na karibu maeneo hayo yote Rais husimama na kuwasilimia kwa muda mfupi.

Lakini kikubwa nachokiona katika ziara hizi kwanza ni ile idadi kubwa inayojitokeza na pili namna wanavyoshangilia hotuba zake na kumfurahia Rais Magufuli na tatu anavyosikiliza kero zao na zingine kuzitatua on the spot.

Hali hii unaweza kuitafsiri vipi kiutawala na haya maneno maneno ya kila siku hali ngumu kimaisha,utawala unakandamiza haki na demokrasia na kuuwa watu?

Lakini hata kwenye viwanja vya michezo na ma-concert kama fiesta watu wanakwenda wengi pia, tena sehemu nyingine kwa kulipia.
 
Wengi wanaoenda huwa wamevaa T-shirt za njano na kijani. Hivyo inaonekana huenda makusudi na sare zao
 
Wengi wanaoenda huwa wamevaa T-shirt za njano na kijani. Hivyo inaonekana huenda makusudi na sare zao
 
Furaha ya masikini ni kuona tajiri akifunguliwa kesi mahakamani,mwajiriwa serikalini anafukuzwa kazi hadharani na kupitia vyombo vya habari.Pia furaha nyingine ya masikini ni pale anapoona mwananchi anayelalamika mbele ya kiongozi halafu kiongozi anaamua kumpa hela.Wao hufurahia mambo ya leo ambayo hayana faida kwa wote.Wakati huohuo masikini hao husahau kudai mambo hao ya msingi hususani kilimo.
 
Huyu ndiye Raisi wetu hasa twende tukamuangalie nani au tumsikilize nani kama wengine wote wanafanya kwa mijibu wa matamshi yake.

Mie naona wapo sahihi tu wala sio kosa na kila binadamu ana vipaumbele vyake.
 
Ni wachache wanaojua Demokrasia imebanwa na hata Maisha kuwa magumu wao wana ona ni mipango ya Mungu tu...
Naeza kusema hapa tatizo wengi sio wasomi..
Tena taarifa zao za habari wanaskiza TBC fm na kuangalia TBC1 Ambayo siku zote hainaga baya la serikali
Lumpen proletariat ndizo tabia zao, unconscious of themselves, unconscious of their fate and their Generations to come. Akipata mihogo akala, basi siku imeisha.
 
Msafara wa rais wa kuusimamisha ni nani? Hata wale wanaoenda kulia mbele yake huwa wanaandaliwa, yule dingi aliovumbua tanzanite mkulu alitumiwa meseji kabla ya kufika mererani, Mkuu huu ni unafiki wa kiwango cha lami!
Nadhani ni unafiki kiwango cha standars gauge
 
Ukijaribu kufuatilia ziara za Rais Magufuli ndani ya nchi na msafara wake wananchi wengi sana wanajitokeza kila kwenye kijiji au miji midogo iliyopo kanda ya barabara na karibu maeneo hayo yote Rais husimama na kuwasilimia kwa muda mfupi.

Lakini kikubwa nachokiona katika ziara hizi kwanza ni ile idadi kubwa inayojitokeza na pili namna wanavyoshangilia hotuba zake na kumfurahia Rais Magufuli na tatu anavyosikiliza kero zao na zingine kuzitatua on the spot.

Hali hii unaweza kuitafsiri vipi kiutawala na haya maneno maneno ya kila siku hali ngumu kimaisha,utawala unakandamiza haki na demokrasia na kuuwa watu?

Kwa nchi hizi zetu za kiafrika kukuta kiongozi anapita mahali na kushangiliwa sio jambo geni, na wala hilo kama ni muelewa huwezi kulitumia kama kipimo cha ubora wake. Leo hii kiongozo yoyote wa kisiasa hapa nchini akiamua kuzunguka nchi hii na akasimama kila mahali atapata nyomi ya watu kumsikiliza, je kusikilizwa na kushangiliwa ndio itakuwa kipimo cha ubora wake?
 
Namtazama Mobutu nae alikua analakiwa na wengi kiasi kwamba hadi ndege nao walikua wakirukaruka kumsbangilia lkn mwisho wa Mobutu nani asiyeujua......
Ni suala la muda tu. Anyway mwacheni apige kazi tupate maendeleo tunayoyataka
 
Niliona malori yamepakiza watu alipokuwa iringa akizindua barabara,mimi nilikuwa nipo kwa basi naelekea dodoma,ilileta mabishabo sana ndani ya basi ile taswira
 
Asingeenda vijijini kutatua kero ingekuwa maneno na jonzi, walitaka apigwe mawe na kuzomewa matokeo yake tofauti, waliotegemea hivyo wamekasirika, wanadhihaki, akitatuwa kero za raia kwenye ziara hizo wanadhihaki, wanasisitiza bado kuna watu wanauwawa kukicha, zile ajali zinazouwa watu kila siku na watu kupoteza maisha kwa mazingira ya kawaida wanapuuzia, je wanaona damu zao tu ni nzito kuliko za wenzao?! Chochote kizuri afanyacho kwao ni kama uovu zaidi, wanaogopa na kuona wivu jinsi anavyozidi kupendwa, wanajuwa 2020 itakuwa safari nyepesi kwake kuliko ya viongozi wao, ambao wanazidi kufifia na kudakia hoja hafifu kupunguza kasi yake.
Kibiti kulitokea mauaji mengi toka kwa wale majambazi na magaidi, hakuna chama cha ukinzani hata siku moja kilitoa taarifa ya kupinga vikali matukio hayo, hata ile kuitangazia jamii za ulaya na marekani kwamba wenzetu Kibiti wanauawa kama kuku! CCM wakamezea, wakaviamini na kuviachia vyombo vya ulinzi kufanya kazi yake, wakipigwa risasi viongozi wa serikali hasa walio chama tawala kwao siyo habari, haisikitishi, haiwahusu, haina haja ya kupiga mayowe na kelele, ghafla wanakuwa viziwi na bubu!
Kwa maoni hayo wafikiri hawa ni binadamu wa aina gani?!
 
Back
Top Bottom