Wananchi wasimulia jinsi Mkenya alivyouawa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWAKA uliopita utabaki kuwa ni wa historia isiyofutika kwa familia ya marehemu Otieno Odhiambo aliyefariki baada ya kupigwa na baadhi ya waendesha pikipiki walio katika kijiwe cha Kimara Mwisho, karibu na kituo cha polisi.

Odhiambo ambaye ni raia wa Kenya, aliyekuwa anaishi hapa nchini, alifariki dunia mwezi wa nane mwaka jana baada ya kupigwa hadi kufariki kutokana na mwendesha pikipiki mmoja kudai kuwa aliibiwa pikipiki yake na marehemu huyo.

Ni habari ya kusikitisha unaposimuliwa lakini ndio ukweli wenyewe; na kama marehemu huyo kama angalijua kifo kilikuwa kikimwita asingalitoka nyumbani kwake siku hiyo.

Marehemu alikuwa ana mke anayeitwa Avijawa Hashimu na watoto wawili Ibu na Zuhura Otieno.

Abdallah Hashimu mkazi wa Goba Matosa, Jijini Dar es Salaam ni shemeji yake marehemu anaanza kwa kusimulia jinsi alivyopata taarifa za msiba huo.

Anasema, siku ya tukio la kifo hicho, alipigiwa simu na kuambiwa kuwa shemeji yake Odhiambo, aliyekuwa amezoeleka kwa jina la Shaaban amechomwa moto, hivyo afanye uchunguzi na kujua ukweli halisi.

Hashimu anasema katika uchunguzi wake aligundua kuwa, marehemu alitoka asubuhi na pikipiki, alipofika eneo la Luoga alianguka kisha pikipiki yake ikaharibika.

Anaendelea kueleza kuwa, watu waliokuwa eneo la tukio, walimshauri kuwa asiendelee na safari arudi nyumbani kupumzika, lakini akawaeleza kuwa, pikipiki ile siyo yake hivyo anakwenda kwa fundi eneo la kimara ili akaitengeneze.

Shemeji huyo wa marehemu aliendelea kusema kuwa, marehemu alipofika kwa fundi akamkuta mtu mmoja ambaye alishindwa kuiwasha pikipiki yake, kwa kuwa marehemu alikuwa ni mtundu aliiwasha na kuomba aende nayo sheli akachukue petroli kwa ajili ya kuweka kwenye ile ya kwake.

Anaendelea kueleza kuwa, marehemu yule alipotoka na ile pikipiki nyingine, mwenye pikipiki akamuona na kuanza kumwita mwizi huku akimfukuza.

“Marehemu alipofika sheli, mwenye pikipiki naye alifika akiwa na mwenzake na kuanza kumpiga, lakini wafanyakazi wa sheli waliwaambia kuwa, kama ni mwizi wasimpige wampeleke kituo cha polisi, kisha wakaondoka naye,” anaeleza shemeji huyo wa marehemu.

Anasema, baada ya hapo, waliondoka na marehemu hadi kwenye kijiwe cha madereva wa pikipiki eneo la Kimara Mwisho karibu na kituo kidogo cha Polisi, na walipofika hapo, wakaanza kumpiga kwa maelezo kuwa ni mwizi.

Maelezo hayo ya shemeji huyo wa marehemu hayakutofautiana sana na baadhi ya watu wengine waliokuwa kwenye eneo la tukio, ambao waliweza kueleza kile walichokiona siku hiyo.

Naye Maria Mangweshi, mkazi wa Kimara Mwisho aliyejitambulisha kuwa ni mwanaharakati wa haki za binadamu ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa nyumba 10, anasema siku ya tukio majira ya saa tano asubuhi, akiwa ndani ya nyumba yake, aliambiwa kuna mtu anapigwa katika eneo lake.

Anasema alitoka nje na kuuliza kulikoni, kisha akawaambia waondoke katika eneo hilo, na kushauri kama ni mwizi waende polisi, kwa kuwa hakuna sheria inayosema mtu auawe.

‘Nilichokuwa nakishuhudia niliona baadhi ya vijana wakimshika marehemu na kumburuza hadi barabarani, hapo wakaanza kumpiga kwa mawe na mbao bila huruma.

“Nilipaza sauti mwacheni mwacheni nendeni mkaite polisi. Vijana wakaenda kuita polisi lakini wakaja wameshusha sura zao sikuwatambua vizuri.Watu walipowaona polisi waliacha kumpiga kijana huyo, lakini nilisikia sauti ikitoka kwa mmoja wao kuwam mmalizeni tutampeleka wapi huyo?” anasema mama huyo na kuongeza baada ya maneno hayo watu hao waliondoka.

Kwa maelezo ya mama huyo, marehemu kabla ya kukata roho aliomba aitwe mwenye pikipiki, lakini hawakumsikiliza na baada ya muda, walichukua tairi, huku dada mmoja aliyejifunika kwa kanga, alikwenda kuchukua mafuta na kaka moja aliyevaa koti aliyapokea kisha walimwagia na kumwekea takataka juu, kisha wakamchoma.

“Kaka aliyekuwa amevaa shati lenye rangi nyekundu, bluu na nyeupe ndiye aliyewasha kibiriti. Nikapaza sauti na kusema bado mnazidi kumteketea mwenzenu kwa moto, mnauhakika gani?”anasema.

Anasema baada ya muda kupita, walifika askari kutoka kwenye kituo cha Mbezi, lakini mtu huyo alikuwa ameshafariki.

Kilichofuata askari hao, walichukua maiti na kuondoka nayo.

Kwa upande mwingine, Mjumbe wa eneo la Goba Matosa ambako marehemu alikuwa akiishi, Zabron Kyando analaani kitendo hicho kwa kusema ni makosa kwa mtu yeyote kujichukulia sheria mkononi.

Baada ya tukio hilo, Tanzania Daima ilianza kufuatilia suala hilo kwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, ili kujua upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi.

Kenyele alitoa ushirikiano wa kutosha baada ya kuitisha faili hilo na kuagiza upelelezi uanze upya, baada ya kuwataka wapelelezi kutoka kwenye ofisi yake kuanza upya upelelezi huo kutokana na upelelezi wa awali kutofikia tamati kwasababu ya wapelelezi hao kudai walikosa ushirikiano kutoka kwa wananchi.

Hata hivyo, pamoja na ushirikiano mzuri kutoka kwa Kamanda huyo, bado upelelezi huo umekuwa mgumu, na wahusika bado hawajakamatwa hata mmoja, kwa maelezo kuwa, ushirikiano kutoka kwa wananchi ni mdogo kwasababu wanaogopa endapo watataja wahusika maisha yao yatakuwa hatarini.

1. Unasemea upande mmoja pekee
2. Hizo habari za undani, swali kwa swali, jibu kwa jibu na tukio kwa tukio ni marehemu tu ajuaye, wewe umeandika umbeya
3. Acha kutulilia wana JF, Waambie wapendwa wako ccm waboreshe huduma za kijamii (usalama wa raia, mahakama, mahabusu, Elimu, afya, biashara, usafiri, makazi ya watu, maji, umeme nk)
3. Mimi uncle wangu amekufa kijijini kwa pneumonia kwa Sababu dispensary ya kijiji haina dawa muhimu na hosp ya mkoa/wilaya ipo km 40 hakupelekwa ( hakuna barabara ya uhakika, hakuna ambulance, alikuwa mwanakijiji, maskini na mzee)

punguza munkari umejuaje kama mimi ni CCM embu kaa chini na tafakari usikurupuke kwa jazba

Pole sana kwa kifo cha uncle wako. Kila kifo huwa kinawahuzunisha wafiwa. Lakini pia hata huyu aliyeuawa ni mtu na hakuna sababu ya kuzuia kuandikwa habari zake. Maana uneonekana hutaki habari hizi ziandikwe. Swala la kujichukulia sheria mkononi ni baya nadhani tungeungana kulikemea badala ya kuaanza mlolongo wenye dhihaka usio na tija

Asante kwa pole.
Siyo dhihaka bali ni ukweli kwamba yote haya ni matokeo ya ukosefu wa huduma za kijamii. Mhusika aende kwenye vyombo husika kudai haki.

Hii hali itaendelea mpaka elimu ya uraia itakapoeleweka kwa watanzania wengi, hivi sasa watu na viongozi wote mbumbumbu, vipofu wanaongoza vipofu

Ni hahari ya kusikikitisha, hivi mpaka lini watu watachukua sheria mikononi mwao, may GOD rest his soul in the eternal peace....

Ukikwapuliwa side mirror au taa ya kwenye gari tena zaidi ya mara tatu, unasema kweli acha hawa vibaka wachomwe moto, ni halali yao.

Ila kwa habari hii niliyoisoma, marehemu kanitia huruma sana ukizingatia ameacha mke na watoto wadogo wasio na msaada.

Poleni sana wafiwa, pelekeni nguvu kwenye kusaidia mjane na watoto wa marehemu kwa mahitaji muhimu, manake hata mkifuatilia kesi it wont change the fact kuwa Otieno is gone forever. Cha muhimu muachieni Mungu.

Back
Top Bottom