Wananchi wanapochezeshwa muziki badala ya kuelezwa sera za mgombea na chama chake. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wanapochezeshwa muziki badala ya kuelezwa sera za mgombea na chama chake.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kichenchele, Oct 9, 2010.

 1. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hivi kwa nini mikutano mingi ya kampeni za hawa wagombea wa CCM zimekuwa zikitumia muda mwingi sana kupiga ngoma na kuwaimbisha nyimbo wananchi badala ya kutumia muda huo kuwaeleza wananchi sera na kusikiliza kero za wananchi ?
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hawana cha kusema unadhani wafanyeje
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huu ni wakati wa burudani na mavuno.... barabara zilizoshindika sasa zinajazwa vifusi, hospitali ambazo hazikuwa na madawa miaka 20 iliyopita sasa zinapandishwa hadhi kuwa za rufaa (nadhani rufaa ya kifo). Hakuna wasiyoyajua wananchi kwa hiyo inabidi waburudishwe tu na kupewa kanga, wakidanganyika wasubiri tena miaka 5.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wasomi na wanafalsafa wanauita huo mtindo kuwa ni kutegemea hisia za watu au appealing to emotions. Yaani ukiwepo watakupamba, wataimba nakucheza huku wakiburudika lakini ukiondoka wanakusahau. Katika mtindo wa kuongea tunauita argumentun ad populum. Sisiemu wataelewa siku ya kupiga kura ndo wajue kuwa jamaa walikuwa wanafurahia bongo flavor to ila wamechoka na ufisadi!
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  umesahau na viroba mkuu.kuna m2 yupo singida anasema leo wanagawiwa msaada wa chakula na mafuta kutoka marekani wakati hiyo sehemu alizeti na mahindi wamevuna kuliko miaka yote.

  mwaka huu sisisiemu.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hakuna njia nyingine ambayo ccm wanaweza kuwaita watu bcs hawajafanya lolote miaka 5, kilichobaki nikupiga ngoma na mziki kwa sana kuwavutia watu. Hakuna mtu anavutiwa na speech zao zaidi ya ngoma kama ni sera watu wamesikiliza sana mwaka 1995.
   
 7. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unauliza jibu?

  Lile sugu kule Mbeya huwa linafanyaGA nini vile?

  Selective amnesia ni ugonjwa unaojulikana kama "hatudanganyiki lakini kudanganya ruhsa"...

  Crap mwanzo mpaka mwisho! :tonguez:
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nakwambia utafikiri ni matamasha au uzinduzi wa albam yote haya kuwapumbaza wadanganyika waendelee kula
   
Loading...