Wananchi Wanahitaji Uongozi Bora, Wanasiasa Wanahitaji Kupata Uongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Wanahitaji Uongozi Bora, Wanasiasa Wanahitaji Kupata Uongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LINCOLINMTZA, May 23, 2011.

 1. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Watanzania wezangu,

  Tanzania yetu inatakribani ya watu milioni 45 na vyama vya siasa kadha wa kadha kama vile CCM, CDM, CUF, kwa uchache. Wananchi walio wengi wanahitaji viongozi bora kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Lakini kuna kundi dongo la wanasiasa ambao ndo 'ingini' ya maendelao, wao wanahitaji kupata uongozi.

  Kwa kifupi, Wananchi walio wengi ni mashabiki tu wa vyama vya siasa lakini si wakereketwa na wafurukutwa kwa vyama hivyo vya siasa ndo maana leo wanamshabikia Dr. Slaa, 2005 walimshabikia JK, 1995 wengine walimshabikia Mrema, N.k. Wananchi wengi wako tayari kuunga mkono chama kinachowapatia matumaini ya maendeleo tofauti na wanasiasa ambao wao wanahitaji nafasi ya uongozi tu bila kujali chama kingine kimefanya nini.

  Kwa sababu hii, wanasiasa wa CDM hawawezi kufurahia kuona CCM inajisafisha na kukubalika kwa wananchi (Ikijivua magamba) vivyo hivyo kwa CCM haipendi jinsi CDM inavyokubalika kwa wananchi (kupitia Operesheni Sangara). Kwa mantiki hii, upinzani upo katika kutafuta uongozi kwa wanasiasa na siyo kwa wananchi kutafuta kiongozi.

  Hivyo CCM kama wamedhamilia kweli kujivua gamba, kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuondoa ufisadi katiaka kila eneo basi wanachi wanaweza kurudisha imani yao kwa chama na kukiungana mkono ili kiendelee kutawala lakini wapinzani wao hawatubaliana nalo kwani wao nao wanahitaji uongozi.
   
Loading...