Wananchi wamshauri Magufuli kuongoza vipindi vinne mfululizo

Status
Not open for further replies.

Josorobert

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
629
215
Hatimaye maelfu ya wananchi wamezidi kupaza sauti wakimtaka Rais Magufuli kubadili katiba na kuweza kuongoza vipindi vingi zaidi kutokana na kasi yake ambayo imekuwa chachu ya matumaini na mabadiliko nchini.

Ujinga huo ndio hatuutaki, tunawacheka nini Rwanda na sisi tunataka kufanya nini? Naamini Tz tuna kina magufuli wengi sana, muhimu kuondoa kikazi chote cha nyerere nchi itakaa sawa tu
Huyu rais jaman yupo vizur sana
 
Hatimaye maelfu ya wananchi wamezidi kupaza sauti wakimtaka Rais Magufuli kubadili katiba na kuweza kuongoza vipindi vingi zaidi kutokana na kasi yake ambayo imekuwa chachu ya matumaini na mabadiliko nchini.

Mh Magufuli usikubali, huu ni ulaghai. Hata Obama anapendwa sana USA BUT ANASTAAFU.
 
Atakuwa ni chaguo la Mungu huyu au sio? Pengine ni malaika kashuka au sio? Mwezi mmoja ambao umeleta mimba na mtoto hajazaliwa tayari mnanunua nguo za mtoto? Bado hata serikali yake haijaingia Bungeni kueleza na kujibu hoja watu wamepagawa? Kweli Tanzania na watu wake kama ndivyo walivyo basi inastahili kuingia kwenye Guinness book of record kama nchi ya majuha.
Nimesema hayo kwani JF inajinadi kama Home of Great thinkers, kwa hiyo mtoa hoja ndio GT wa nchi hii.
 
akiendelea na kasi hii maendeleo yakaonekana, watoto wetu wakasoma bure, uchumi ukakua, uzalishaji ukaongezeka, viwanda vikastawi watoto wetu wakaondokana na tatizo la ajira --- jamani kwani tunataka nini?? hata akitaka kuachia tutamlazimisha abaki aendelee kutumbua majipuuu
 
Ujinga huo ndio hatuutaki, tunawacheka nini Rwanda na sisi tunataka kufanya nini? Naamini Tz tuna kina magufuli wengi sana, muhimu kuondoa kikazi chote cha nyerere nchi itakaa sawa tu

Wewe ni mmoja wapo ya Watz wache wenye IQ kubwa na mambo kama hayo aliyo yasema mtoa mada yapo Afrika pekee kwa wenye akili huwezi yaona
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…