GE2025 Wananchi wakila Ubwabwa Same 'Uzalendo unaanza pale unapojali Afya ya mtu'

GE2025 Wananchi wakila Ubwabwa Same 'Uzalendo unaanza pale unapojali Afya ya mtu'

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Vijana wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro wameeleza kuwa wapo radhi kutoa kadi zao za kupiga kura kwa mgombea wao ili wawe na uhalali wa kujipigia kura wenyewe kutokana na kuridhishwa na sera yao ya utoaji wa ubwabwa.

Wakizungumza hivi karibuni mara baada ya mtiania wa Ubunge kupitia CHAUMMA Gervas Mgonja kurejesha fomu zoezi lililoambatana na ufunguzi wa ofisi za chama hicho Same Mjini, baadhi ya vijana wameeleza kuwa sera ya chama hicho ya kutoa chakula ni ishara tosha ya uzalendo na kujali wananchi wake.

"Nampa kadi yangu akajipigie kura kuanzia Diwani, kama wanajali afya ya mtanzania kwa kula wewe ni Mtanzania mzalendo, uzalendo unaanzia pale unapojali afya ya mtu, kama utanipa hela na mimi sijala nina njaa, nitaenda kunywa pombe kama umenipa chakula inamaana umejali afya yangu na mimi nitakubali" walieleza vijana hao.

Je unafikiri uzalendo unaweza kupimwa kwa kupewa chakula pekee na kupelekea kukabidhi kadi yako ya mpiga kura kwa mgombea?
 
Back
Top Bottom