Wananchi waasi, Polisi waua mmoja kwa risasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi waasi, Polisi waua mmoja kwa risasi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 5, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Wafunga barabara kuu Segera- Chalinze
  [​IMG] Magari yakwama, yatumia njia za panya
  [​IMG] Kisa, wakataa kunyang'anywa ardhi yao
  Baadhi ya wakazi wa Mji mdogo wa Segera wilayani hapa mkoani wa Tanga, jana walifunga barabara kuu ya Chalinze-Segera kwa kile kinachodaiwa ni kuionyesha Serikali hasira zao kufuatia kunyang'anywa ardhi.

  Wakazi hao ambao wengi wao ni wafanyabiashara ndogondogo, walifunga barabara hiyo kwa zaidi ya saa nne na kusababisha msururu mrefu wa magari na mengine kupitia barabara ya Handeni mjini - Mkata-Handeni hadi mjini Korogwe.

  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Seif Mpembenwe, alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi.

  Mpembwenwe alisema wakazi hao walifunga barabara hiyo kwa kuweka mawe na magogo.

  "Unajua chanzo cha vurugu hizo ni mgogoro wa ardhi, hapa kuna order (amri) iliyotolewa na Mahakama kuwa eneo hilo si lao. Sasa ukiangalia mgogoro huo na kufunga barabara wapi na wapi... ni upuuzi, " alisema Mpembenwe na kuongeza:

  "Ni kweli kuna mtu kapigwa risasi hapa yaani kulikuwa na mambo mawili kwa wakati mmoja, kuna gari la benki lilikuwa ikisafirisha fedha kwenda Dar es Salaam sasa nalo lilikumbwa na hali hiyo, ndipo mlinzi wa gari hilo alifyatua risasi kadhaa hewani na kumjeruhi mmoja, sina taarifa kamili kama amefariki dunia ila nipo katika eneo la tukio," alisema Mpembenwe.

  Mkuu huyo wa wilaya alisema watu hao ambao wengi wao ni vijana waliondoa magogo na mawe hao na kufungua barabara hiyo baada ya kuona vyombo vya dola vikiwasili katika eneo hilo lililopo njia panda.

  Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa vurugu hizo zilisababishwa na wamiliki wa vibanda vya biashara katika eneo hilo.

  Alisema katika vurugu hizo, mtu mmoja ambaye hajapatikana jina lake mwenye umri kati ya 13 na 15 alipigwa risasi na kufariki dunia muda mfupi baadaye.

  Afisa Mtendaji wa Kata ya Segera, Mohamed Mbwana, amethibitisha mtu huyo kuuawa kwa kupigwa risasi na kumtaja kuwa ni Omari Juma.

  Mbwana alisema hana uhakika kuhusu mazingira ambayo kijana huyo aliuawa, lakini alisema inawezekana ni wakati Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walipokuwa wakiwatawanya wananchi.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Simon Siro, hakupatikana kuelezea tukio hilo kutokana na kuwa likizo.

  Kaimu Kamanda wa Mkoa, Simon Mgawe, aliiambia Nipashe jana jioni kuwa kijana huyo aliuawa na polisi mmoja wakati yeye na mwenzake waliokuwa wanasindikiza fedha za benki ya CRDB kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam.

  Kamanda Mgawe alisema kuwa gari la kampuni ya ulinzi ya binafsi lililokuwa linasafirisha fedha hizo baada ya kufika katika eneo la tukio walikuta kundi kubwa la watu na njia ikiwa imezibwa kwa mawe na magogo.

  Alisema kuwa polisi hao waliingiwa na hofu na kuamua kuteremka katika gari kuondoa mawe na magogo, kitendo ambacho hakikuwafurahisha wananchi hao, ambao walianza kuwashambulia kwa mawe na kusababisha polisi mmoja kuanguka na kupoteza fahamu.

  “Askari wetu mwingine baada ya kuona wamezidiwa, aliamua kurusha risasi iliyompiga mtu mmoja tumboni na kufariki,” alisema Kamanda Mgawe na kuongeza kuwa muda mfupi walifika FFU na polisi wa kawaida waliokuwa wametumwa kwenda eneo hilo kutuliza gahasia hizo.

  Alisema baada ya askari hao kuwasili, walimpeleka polisi aliyejeruhiwa pamoja na majeruhi wengine katika Hospitali Taule ya Wilaya Magunga, lakini kutokana na hali ya askari huyo kuwa mbaya, alihamishiwa badaye katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo.

  Imeandikwa na Sonyo Mwenkale na Godfrey Mushi, Handeni
  CHANZO: NIPASHE

  http://www.ippmedia.com/
   
 2. O

  Omumura JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ngoja wafe, safi sana kunyimwa kiwanja na kufunga barabara wapi na wapi, tuache ushabiki wa uhuru uliopitiliza hadi tuonekane mazuzu mbele ya ulimwengu wa wastaarabu!
   
 3. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #3
  Oct 5, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Raia tunapaswa pia kujua kua silaha ya moto ni hatari. Inashangaza unapoona mtu anampiga jiwe askari aliyeshika silaha. Ni Ujinga uliopitiliza.
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sio ujinga, ni katika kutetea haki. Silaha ya moto ni hatari ndio lakini kupoteza kilicho haki yako ni hatari zaidi. Inapotokea situation kama hiyo adrenalin inapanda and the human part in you is replaced by the animal instict of survival, thats when you decide to comfront not only a police with a gun but a soldier with a tank.
   
Loading...