Wananchi wa Tanzania ni waoga au vyombo vya ulinzi vina ueledi na nguvu?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,045
10,476
ikumbukwe Mimi Baba Morgan nia yangu sio kuhamasisha maandano ni kuhoji kwa nia njema kabisa na kupongeza vyombo vyetu vya ulinzi kwa kuweza kudhibiti maandamano na migomo isiyokuwa na tija kwa taifa na vilevile kuwaomba vyombo vyetu vya ulinzi kushare ujuzi walionao kwa mataifa yanayokabiriwa na maandamano Mara kwa mara

Tunashuhudia kwenye vyombo vya habari wananchi wa mataifa mengine walivyo wepesi kuchukua hatua hasa ya kuandamana pale panapotokea sintofahamu baina yao na serikali ili kushinikiza hatua flani zichukuliwe.

Nchi Kama Myanmar ambayo ina utawala wa kijeshi ilishindwa kudhibiti maandamano ya wananchi wake lakini kwa Tanzania vyombo vya ulinzi vimeweza kudhibiti hata mawazo ya kuandamana vichwani mwa raia wake haya ni mafanikio makubwa kwa IGP

Kwa upande mwingine yawezekana vyombo vya ulinzi havina uwezo huo tunaodhani bali uoga wa raia unafanya vyombo hivyo kupata sifa wazisostahili Aya Ni maoni tu.

Maandamano sio kitu chema madhara yaliyotokea South Africa wote tunayajua.

From northern part of Tanzania.
 
Back
Top Bottom