Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,364
Nimekubali mkuu, tuambie ni wapi na ni lini tuingie barabarani
Unakubali kwenye keyboard tu ama unakubali kwa vitendo?
Nimekubali mkuu, tuambie ni wapi na ni lini tuingie barabarani
safi sana,naunga mkono kupanda kwa bei ya umeme,ari zaidi,nguvu zaidi,na kasi zaidi,mungu awatie nguvu viongozi wetu wasiache moyo huo na watende zaidi ya hapo.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!
Nimekubali mkuu, tuambie ni wapi na ni lini tuingie barabarani
Wana JF kwa tabia yao ya kifisadi TANESCO wamezima link yao inayomwezesha mtumiaji wa luku anayetaka kununua luku sasa hivi(saa 3 usiku) asiweze - wa mekata mawasiliano na makampuni ya simu ili tushindwe kununua na kupata units za umeme! Ili kesho ndo tununue/tupate kwa bei yao mpya ya kifisadi - mungu atusaidie!!
Shirika la umeme Tanzania, Tanesco limekubaliwa ombi lake la kupandisha bei ya umeme kwa 40% kuanzia kesho. Hili ni pigo kubwa kwa wananchi wa kada zote, ingawa wenyewe wametupiga siasa eti ongezeko halitawagusa walalahoi. Ukweli ni kwamba ongezeko la bei ya umeme huchochea pia ongezeko la gharama za huduma mbali mbali ikiwemo afya, Elimu, mawasiliano, nk. kwa kuwa nyingi ya huduma hizo hutegemea nishati ya umeme. Pia huongeza hata bei ya mkaa maana ndo imekua kimbilio kwa kutoshikikika kwa bei ya umeme.
Wakati umefika kwa watanzania kuvaa ujasiri na kupambana na hawa watawala wetu ambao hawana huruma na Wananchi. Tuungane katika hili bila kujali itikadi. Kuna tetesi kwamba deni la dowans limeshalipwa kinyemela ndo maana wanataka kurudisha gharama kupitia kwa wananchi wanyonge. Tulipiga kelele kuhusu kuilipa Dowans, hivi sasa wako kimyaaaaa! Napendekeza maandamano makubwa ya kitaifa kupinga ongezeko hili. Katika hili naomba watanzania tulio wengi tuungane maana sote ni wahanga. Naomba kutoa hoja.
Umesema kweli tupu.Nani wa kufanya maandamano?Wenzetu Kenya tu wanatushinda kwa ujasiri wa kuandamana.Tatizo la nchi hii ni sisi wenyewe.