Wananchi Tuungane kupinga ongezeko la bei ya umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Tuungane kupinga ongezeko la bei ya umeme

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dazu, Jan 14, 2012.

 1. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Shirika la umeme Tanzania, Tanesco limekubaliwa ombi lake la kupandisha bei ya umeme kwa 40% kuanzia kesho. Hili ni pigo kubwa kwa wananchi wa kada zote, ingawa wenyewe wametupiga siasa eti ongezeko halitawagusa walalahoi. Ukweli ni kwamba ongezeko la bei ya umeme huchochea pia ongezeko la gharama za huduma mbali mbali ikiwemo afya, Elimu, mawasiliano, nk. kwa kuwa nyingi ya huduma hizo hutegemea nishati ya umeme. Pia huongeza hata bei ya mkaa maana ndo imekua kimbilio kwa kutoshikikika kwa bei ya umeme.

  Wakati umefika kwa watanzania kuvaa ujasiri na kupambana na hawa watawala wetu ambao hawana huruma na Wananchi. Tuungane katika hili bila kujali itikadi. Kuna tetesi kwamba deni la dowans limeshalipwa kinyemela ndo maana wanataka kurudisha gharama kupitia kwa wananchi wanyonge. Tulipiga kelele kuhusu kuilipa Dowans, hivi sasa wako kimyaaaaa! Napendekeza maandamano makubwa ya kitaifa kupinga ongezeko hili. Katika hili naomba watanzania tulio wengi tuungane maana sote ni wahanga. Naomba kutoa hoja.
   
 2. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa mkubwa. Wakati wa kufanya maamuzi ni sasa, saa ya ukombozi ni sasa.
   
 3. P

  Paul J Senior Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri lakini kwa watanzania ninavyowajua mimi hawana habari na hili, wataishia kulalamika kichinichini bila action yoyote na mwisho wa siku watazoea na viongozi wetu hilo wanalijua ndo maana wanafanya maamuzi ya kijinga kama haya. Kiongozi aliyemakini huu haukuwa muda wa kupandisha bei za umeme ukizingatia tayari mfumuko wa bei uko juu sana na kuongeza bei ya umeme ni utazidi kuwa juu zaidi. Mimi binafsi nakuunga mkono nilipinga hata kabla ya kutangaza bei hii mpya, na unafiki wa viongozi wetu uliuona pale Makufuri alipotangaza nauli ya kivuko sasa subiri uone wanafiki haohao kama watapinga na hili maana linagusa kila mmoja! Mimi yangu macho, sitafanya kazi yoyote ya maendeleo na nguvu yangu naelekeza kujipatia angalau mlo mmoja kwa siku lakini naamini ikifikia asilimia kubwa ikashindwa hata kuupata huo nusu mlo tutakuwa na uwezo wa kuwa na maamuzi ya busara juu ya mstakabali wa maisha yetu na taifa letu kiujumla. Kwa sasa sioni mtanzania wa kupinga ongezeko la bei ya umeme kwa kuandamana na kama ingelikuwa hivyo mara tu baada ya Tanesco kutangaza bei mpya watu tungelikuwa barabarani tayari!
   
 4. maranduhussein

  maranduhussein Senior Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umesema kweli tupu.Nani wa kufanya maandamano?Wenzetu Kenya tu wanatushinda kwa ujasiri wa kuandamana.Tatizo la nchi hii ni sisi wenyewe.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni mimi na wewe tu tunaweza kuungana kupinga je tutaweza?
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wakati mwingine msiwe kama panzi kusahau vitu haraka kiasi hicho:

  Wakati TANESCO ilipokuwa imezidiwa na power generation kutokana na ukame, Bunge la Jamhuri na Wafanyabiasha walishauri serikali kutafuta vyanzo vingine vya dharura vya umeme ili uwepo, wakati huo walitumia maneno yafuatayo "Kheri umeme wa ghali uwepo kuliko kutokuwepo kabisa kwa umeme, kwa kuwa kutokuwepo kwa umeme kutaadhiri uchumi kwa kiasi kikubwa zaidi"; maneno haya lalitoka kwa wawakilishi wote wa wananchi wakiwepo wabunge wa Upinzani...

  Sasa swali nani anatakiwa kulipia ongezeko la gharama za umeme wa dharura? a direct consumer or indirect consumer?
   
 7. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wakiamua wameamua ndo hivyo mkigoma maneno yao pigeni mbizi.Hii ndo tz zaidi uijuavyo.Check inflation rate inatisha balaaaa
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Halafu kibaya zaidi ni kuwa tumepandishiwa vitu zaidi ya viwili ndani ya wiki lakini kama kwamba haituhusu !
   
 9. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hili ndo huwa linanishangaza sana. Tuko Kimyaaaaaaaaaaaa! Ndo maana huwa wanakurupuka tu, maana hawapati challlenge yoyote toka kwa wananchi.
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  tatizo huwa tunaishioa kwenye keyboard tu.
   
 11. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #11
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  safi sana,naunga mkono kupanda kwa bei ya umeme,ari zaidi,nguvu zaidi,na kasi zaidi,mungu awatie nguvu viongozi wetu wasiache moyo huo na watende zaidi ya hapo.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!
   
 12. f

  frontline1 Member

  #12
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wakuandamana tupo wengi tu, muda wakufanya hivyo haujafika bado, ngoja ngoma isogee, najua ugumu wa maisha utapanda mara dufu ifikapo july 2012 wazazi watakaposhindwa kulipa ada za wanawao wkashindwa kuwalisha, wakakosa maji yakukoga, etc ndipo utawaona wemyewe wanjisogeza barabarani bila kuhamasishwa kwa kutumia nguvu, wakati huo sisi tuliotayari sasa tutawaongoza kuleta mapinduzi!

  hatugomi kwa swala la umeme tu bali tunagomea mfumo mbovu uliotufikisha hapa, ni kweli kuwa heri kuwa na umeme wa ghali kuliko kuukosa kabisa bt imekuaje mpaka tutamani umeme wa ghali? hicho ndicho kinacho tusukuma kugoma!
   
 13. Lyamungo

  Lyamungo Member

  #13
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekubali mkuu, tuambie ni wapi na ni lini tuingie barabarani
   
 14. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  tulianza maandamano ya epa,ikapita,richmond mara tuzo ya dowans,mara tutaandamana mswada wa katiba ikisomwa kwa mara ya pili,sasa ni umeme. Tangu lini nchi hii ya wadanganyika watu wakaaandamana?zaidi ya wanachuo kuandamana kudai mikopo? Walimu walishatishia mara ngapi migomo na hamna kitu? Nchi ya watu legelege na mambo yake yanakwenda kiulegevulegevu,kwa sababu tumelegea wafadhili nao wanataka kutulegeza zaidi kwa kutucameroon ndio tupate msaada.
   
 15. terabojo

  terabojo JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wana JF kwa tabia yao ya kifisadi TANESCO wamezima link yao inayomwezesha mtumiaji wa luku anayetaka kununua luku sasa hivi(saa 3 usiku) asiweze - wa mekata mawasiliano na makampuni ya simu ili tushindwe kununua na kupata units za umeme! Ili kesho ndo tununue/tupate kwa bei yao mpya ya kifisadi - mungu atusaidie!!
   
 16. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Watanzania ni janga la taifa.
   
 17. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Wacha wakome, maana hawajitambui
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu wangekuwa wanakumbana na changamoto tofauti hata kutangaza wangekuwa wanakosa pa kuanziia sijui waTz tumelaaniwa ama ni pepo gani tunalo
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kidumu kwa kutuibia?
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Du tutavumilia mpaka mbali hivyo?
   
Loading...