Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,513
- 41,022
Tanzania haijawahi hata mara moja kukabiliana na majanga kwa namna ya kuridhisha. Ni kwa nini?
Kila wakati likitokea janga, Serikali inakimbilia kuunda kamati ambazo hazijawahi kutatua matatizo.
1. Tuliwahi kupata janga baya kabisa kule Mwanza la kuzama kwa meli, na watanzania wenzetu karibia 1000 waliteketea. Meli ile ikiwa imepulinduka, ilibakia bila kuzama kwa masaa zaidi ya manne lakini tulishindwa kuwaokoa abiria. Wachache waliookolewa, ilikuwa ni kwa msaada wa wavuvi.
2. Tuliwahi kupata ajali ya treni kusombwa na maji. Hata kutoa miili tu ilikuwa shida kiasi cha baadhi kutolewa viungo vikiwa vimenyofoka
3. Kuna lorry liliwahi kuangukia basi dogo pale Kimara, ilichukua zaidi ya masaa matano kulinyanyua lorry lililokuwa limelalia basi dogo likiwa na abiria ndani. Kuna abiria alipona lakini akiwa amekatika miguu, alibanwa chini akiwa analia kwa masaa zaidi ya matano. Hiyo ni Dar es Salaam, sijui ingekuwaje kama ajali ile ingekuwa imetokea Kigoma au Sumbawanga.
4. Kuna basi lilibeba wanakwaya wa Kenya lilipata ajali mkoani Tanga (nilishuhudia kwa macho yangu), ajali ilitokea saa 10 alfajiri lakini mpaka saa 2 majeruhi walikuwa bado hawajafikishwa hospitali. Kenya ilituma ndege kuja kuwachukua majeruhi na miili ya marehemu.
5. Jana limetokea janga la moto kwenye soko la Kariaokoo, katikati ya jiji, imeshindikana kuzima moto. Kama inashindikana kuzima moto uliotokea katikati ya jiji, mahali ambapo ni mita chache kutoka makao makuu ya kikosi cha zimamoto, tunatarajia wataweza kukabiliana na ajali ya moto ajali ikiwa imetokea wapi? Naamini moto hata ukitokea kwenye ofisi za makao makuu ya Zimamoto, matokeo hayatakuwa tofauti.
6. Kuna ajali nyingine nyingi za kuungua shule (watoto wetu wakapoteza maisha kutokana na uzembe wetu, na hasa Serikali), kuungua majengo ya biashara, ajali za barabarani na majini, zilizowahi kutokea, ambazo kwa hakika ukitazama jinsi zilivyoshughulikiwa, unaona kabisa kuwa hakuna uwezo wa Serikali kushughulika na majanga.
Ukifuatilia majanga ambayo yamewahi kutupata na yanayoendelea, hakika hizi kamati zinazoundwa na serikali hazina maana kabisa.
Ajali za mabasi zinapotokea, unashangaa kusikia eti uchunguzi wa Polisi umeonesha kuwa chanzo cha ajali ni kupasuka tairi la mbele. Ah! Ujinga kabisa! Hivi kweli hii ni taarifa ya kiuchunguzi toka kwa chombo kama Polisi? Mtu ungetegemea, taarifa ingekuwa ya kina, kama wanavyofanya wenzetu, kama vile:
1) basi lilikuwa katika mwendo gani. Ulikuwa mwendo sahihi au hapana? Mwendokasi ulichangia kwa kiasi gani kutokea kwa ajali na madhara yake?
2) tairi liliposuka, lilitengenezwa mwaka gani? Lilikuwa bado kwenye kipindi cha matumizi kwa kadiri ya muda ulioneshwa na mtengenezaji? Tairi lilistahili kuendelea kutumika, kwa kuangalia viashiria vya kiwango cha kutumika?
3) tairi lililopasuka, kama lilikuwa bado kwenye muda wake wa matumizi kwa vigezo vya muda wa kutengenezwa na kutokana na kiwango kilichotumika, lilikuwa na ubora unaotakiwa?
4) uchunguzi wa ubora wa matairi ya kampuni hiyo uliofanyika a kwa mtengenezaji au wakala wake, umedhihirisha matairi hayo yana ubora unaotakiwa?
6) kama chanzo cha tairi kupasuka, ni ubora wake, hatua za dharula zilizochukuliwa kuzuia matumizi ya matairi ya kampuni hiyo, ubadilishaji wa matairi ya kampuni hiyo kwa magari yote yanayotumia matairi ya kampuni hiyo.
Lakini kwa bahati mbaya inaonesha Jeshi la Polisi, halina uwezo kabisa wa kufanya uchunguzi wa kina.
Ni vema kwenye Katiba mpya, kila janga/ajali inapotokea, Serikali inapounda Kamati ya uchunguzi, wananchi kwa kupitia taasisi huru, zisizo za kiserikali, na ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na Serikali, zipewe haki ya kuunda kamati za kuichunguza Serikali, kupima yafuatayo;
1) uwezo wa jumla wa serikali kushughulikia janga lililotokea
2) uwezo wa taasisi husika katika kushughulikia na kupunguza madhara ya janga
3) proactivity ya Serikali na taasisi husika
4) kuwatambua watu ndani ya Serikali wa kuwajibishwa kutokana ama na uwezo mdogo au uzembe.