Sukrani sana kwa hizi picha,wengine wanafikiri ni suala la utani. Mkoa wa Kagera unaharibiwa hasa na watu wasio wa hapa kagera..fikiria wabunge wote wa Mkoa huu hakuna hata mmoja anayeishi Kagera au kufanya kazi Kagera,wanakuja kama wageni kuomba kura tu au kutembelea jamaa zao.
Nani alaumiwe katika hili? Wananchi waliopo kagera
wanatakiwa wajitathimini.Si rahisi mtu wa kagera anayeishi
Dar au Mbeya aje kuhangaika na barabara wakati hakai huko.
Kuna tatizo jingine ambalo halisemwi na hili
linachangia kwa kiasi kikubwa watu kutojihusisha
na maendeleo ya kwao na hili ni kuwabagua
Pindi wanapoletwa au wamefariki ili kuzikwa au kuleta ndugu zao.
unakuta wanabaguliwa kwamba huwa hawashiriki
kwenye misiba,hivyo nao ushiriki unakuwa mdogo.
Sasa chukulia ndugu wa huyo au watoto wa aliyefariki
hata kama wana uwezo watajihusisha na maendeleo
ya kijiji hicho, wakati walibaguliwa walipokuwa na msiba?
Mi naona maendeleo ya kweli yataletwa na wakazi
wa bukoba kwa kutafuta ni nini chanzo cha kukwama
na kujifunza kutoka mikoa mingine,hapo lazima pabadilike.