wananchi, Madiwani, Wabunge, Mawaziri, wote "tunaishauri serikali", serikali ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wananchi, Madiwani, Wabunge, Mawaziri, wote "tunaishauri serikali", serikali ni nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwenda_Pole, Sep 24, 2009.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Waheshimiwa kuna hii kitu inanitatiza sana siku zote,
  kila siku mitaani na kwenye vyombo vya habari ukisikia wananchi wakizungumza kuhusu tatizo flani likiwa limetokea utasikia wanatumia hii kauli ya tunaishauri serikali, Madiwani, wabunge na hata mawaziri wakati mwingine huwa wanasema tunaishauri serikali.., hivi serikali ni nani?? kwa mtazamo wa Watanzania. Kwa sababu inashangaza sana mpaka waziri wa wizara husika nae anapohojiwa kuhusu ishu inayomhusu yeye moja kwa moja kama waziri badala ya kujibu anasingizi serikali..?? nisaidieni mwanzenu manake nashindwa kuelewa serikali ni nani kwa mtazamo wa Watanzania.
   
 2. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Hawajakosea, serikali ni rais na mawaziri wake. Waziri wa maji anaweza kuishauri serikali juu ya suala linalohusu wizara ya mambo ya ndani. Sasa tatizo ni kwamba wananchi wenye upeo mdogo uchanganya majukumu ya bunge na ya serikali, hivyo basi suala lihusulo bunge, mfano utungaji sheria, wanahusisha moja kwa moja na jukumu la serikali (utekelezaji wa sheria) na ndio maana kila jambo utasikia wakisema "tunaishauri serikali."
   
Loading...