jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,556
- 25,368
Ili tuonyeshe hatujalogwa tumpe nani?
Atakayepitishwa na UKAWA
Ili tuonyeshe hatujalogwa tumpe nani?
Atakayepitishwa na UKAWA
wee lizibon mwehu kabisa,huyo ndiye mtanzania pekee ambaye ataifanya nchi hii ikae sawa,wengine wote ni manyangau tu
.
Hivi kweli unaweza kutaka kuwa rais hata swali moja bunge kwa miaka 8 hakuna??? hujui shida za watanzania harafu unataka uwe rais? Wa watanzania au wa chuo?
Ukilinganisha maendeleo ya Jimboni kwake na hao waliouliza maswali vipi? Maana maswali ni muhimu na maendeleo ni muhimu pia
Maendeleo bila maswali huwezi pata isipokuwa iwapo wewe ni fisadi, yaani unatumia fedha binafsi kujenga madarasa, barabara, maji, umeme vijiji, je EL amejenga barabara Monduli???
Ukitumia Fedha binafsi kama Ndesamburo kule Moshi au Mbowe zile ambulance maana yake ni Fisadi?
Miaka 8 bila swali hata na watetezi wake kama ni faraaaa tu, hoja ni iweje miaka 8 bila swali bungeni???
Hata mawaziri wengine waliostaafu utawaona wanakaa Nyuma kabisa kimya. Yeye anaijua serekali yote na kuuljza swali ni kama kutaka kuwaumbua hivyo kwa Busara tu utawaona wengi wako kimya
Naheshimu mawazo ya kila mtu na chaguo la mtu...lakini sidhani kama unahitaji kuwa na akili ya ziada au kuambiwa madhira waliyotusababishia watawala wetu waliopo madarakani...labda kama na wewe ni miongoni mwa hao wanaoitzfuna nchi kwa jinsi watakavyo...Endelea kuwashawishi kwa hoja watu wamfuate unayemtaka lakin heshimu pia watakaokuwa na mawazo tofauti na wewe.Hatupo sawa na hatufikiri sawa.
Demokrasia maana yake utawala wa watu, ndio maana tutaenda kwenye chaguzi, wananchi wenyewe wataamua.Vyovyote yatakavyokuwa mawazo ya wengi yatakayoonyeshwa kwenye sanduku la kura ndio mawazo ya watu wa Tanzania, na ndiye mtu sahihi waliyemuona anawafaa.Waheshimu watu hao.
Sasa yuko Bungeni kuwalinda serikali au kuwakilisha wananchi?