Wananchi hatuna imani tena na mfumo wa uandikishaji BVR

Wananchi hatuna imani tena na mfumo wa uandikishaji BVR

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,659
Reaction score
28,838
Habari wana Bodi.

Kuna kila dalili ya mfumo mpya wa uandikishwaji wa vitambulisho vya kupigia kura BVR uliletwa kwa manufaa ya kikundi au chama fulani tunapoelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Hii inatutia shaka sana wananchi huenda huu mfumo ambao umeshaonyesha mapungufu makubwa mpaka sasa ukatumika kutuibia kura kwani maeneo mengi ambayo kumeonekana kuwa na ngome nzito za upinzani wamenyimwa fursa za kujiandikisha.

Naishauri NEC isitishe huu mfumo kwani siyo salama tena na tunapoelekea huenda tukaingia katika matatizo kama hatua za makusudi hazitochukuliwa mapema.

Pia UKAWA huu siyo wakati wa kulala maana tiyari mfumo huu umeshatupunguzia kura zetu, toeni tamko kwa mamlaka husika kabla hatujaingia katika matatizo zaidi.

Nawasilisha.......
 
Hatuna imani kabisa..
 
Kitu kinanishangaza ile mikoa walikuwa wanauhakika watapata kura nyingi, bvr imekaa huko mwezi, sehemu hawakubaliki wameweka wiki moja, mara waahirishe kuandikisha, mara wasogeze mbele kimya kimya! Yaan ccm wamejaa hila na uovu!
 
Habari wana Bodi.

Kuna kila dalili ya mfumo mpya wa uandikishwaji wa vitambulisho vya kupigia kura BVR uliletwa kwa manufaa ya kikundi au chama fulani tunapoelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Hii inatutia shaka sana wananchi huenda huu mfumo ambao umeshaonyesha mapungufu makubwa mpaka sasa ukatumika kutuibia kura kwani maeneo mengi ambayo kumeonekana kuwa na ngome nzito za upinzani wamenyimwa fursa za kujiandikisha.

Naishauri NEC isitishe huu mfumo kwani siyo salama tena na tunapoelekea huenda tukaingia katika matatizo kama hatua za makusudi hazitochukuliwa mapema.

Pia UKAWA huu siyo wakati wa kulala maana tiyari mfumo huu umeshatupunguzia kura zetu, toeni tamko kwa mamlaka husika kabla hatujaingia katika matatizo zaidi.

Nawasilisha.......

Wadau;
Ndio maana tunawaomba tena Viongozi na Wanasheria wa UKAWA, wanaharakati wa Katiba, Haki na Demokrasia wasiendelee kulala, tunawaomba tena! Yapo malalamiko mengi mno yanayotokea kila kona ya Tanzania ambapo uandikishaji kwa BVR imekamilika au unaendelea. Tusipuuze hata chembe ya kilio hiki cha wananchi popote walipo. Hao watu ndio Kura zenyewe zinalalamika, kura zinatoa machozi mnyanyuke msikilize vilio hivyo. #

BVR ndio kifo cha Demokrasia ambayo mmeijenga kwa Miaka karibia 23 sasa, na viashiria vyote ninapatikana ktk visa mbalimbali, usiri wa Tume, 'kuharibika kwa mashine', 'kuahirishwa kwa uandikishwaji kwa sababu hewa' kuzuia wananchi kujiandikisha na wengine kujiandikisha zaidi ya mara 2! Hizi zote ni neema za Mungu na ishara za kufanyiwa kazi Haraka. UKAWA tukizinduka, tukitambua kuwa BVR ililetwa kwa 'lengo maalum' tutafanya maamuzi ya haraka sasa, la sivyo Ushindi utakapopokonywa na 'Majizi' haya ya Demokrasia, siku hiyo UKAWA au wanaharakati hamtakuwa tena na mwanya kamwe wa kurekebisha uovu huo na kuirudisha imani ya wananchi kuwa mnaweza lolote ktk Demokrasia, maana MUDA NDIO SASA, mnaombwa kunyanyuka na kutenda, hamtendi inavyotakiwa sasa, na baadaye Uchaguzi ukeshafanyika na Majizi yakaiba kura kuvuruga HAKI na Ushindi wa Umma, hamtakuwa na kauli kwa umma! Itaonekana ni malalamishi tu yatatupwa!!

@Mh Lissu, @Mh Nyaucho Marando, Prof Safari, @Mh Mbowe, @Mh Mbatia, Prof Lipumba;
nyie ndio Mwanga na taa ya Taifa kwa sasa kuelekea Demokrasia kamili. Mnapokalia kimya hali hii, Udhaifu huu wa BVR, Uozo huu wa Serikali kuua Demokrasia, wananchi wanazuiwa kujiandikisha, mashine za BVR 'zinaharibika' kisanii na uandikishaji 'unaahirishwa' tu kimikakati kwa sababu hewa, wakati timu ya Wanasheria wa UKAWA inakaa tu kimya na kungojea 'Huruma' ya tume ifanye itakavyo kujisahihisa [Jambo ambalo kamwe ni kinyume na mikakati yao], hayo madhara yake kupoteza KURA na Ushindi, itakuwa ngumu mara 200 kuyatatua pale uchanguzi utakapoisha na kupoteza ushindi na kuvuruga Haki ya Umma ulivyoamua. Tunawaomba tena mchukue hatua KALI sasa na sio baadaye!!
 
Ww jisemee mwenyewe na kama huna imani na Bvr ni mfumo upi utumike kwani wa zamani haufai
 
Ukawa ndo zenu kulialia kama wanawake hamna jipya october inakuja mnapigwa kweupee msisingizie BVR
 
ccm baada ya ila zao kugonga mwamba wanawachochea ukawa wakatae bvr...

ukawa wana support raia kujiandikisha kwa wingi.
 
Ukawa ushauri huu sio wa kupuuza kabisa. Nendeni mahakamani na huko mahakamani wakiamua kiaiasa hapo itakapofika october kitendo cha kuchakachua tu tunaingia mtaani na nguvu ya umma itachukua hatua kali. Watu wanafanya makusudi kamili kwa ajili ya kukibeba chama fulani. Ikumbukwe kuwa ili kuweza kuchakachua inabidi wapiga kura wachache. Lakini idadi ikiwa kubwa itakuwa shida.

Cc. Tumaini Makene, Ben Saanane, Julius Mtatiro
 
Habari wana Bodi.

Kuna kila dalili ya mfumo mpya wa uandikishwaji wa vitambulisho vya kupigia kura BVR uliletwa kwa manufaa ya kikundi au chama fulani tunapoelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Hii inatutia shaka sana wananchi huenda huu mfumo ambao umeshaonyesha mapungufu makubwa mpaka sasa ukatumika kutuibia kura kwani maeneo mengi ambayo kumeonekana kuwa na ngome nzito za upinzani wamenyimwa fursa za kujiandikisha.

Naishauri NEC isitishe huu mfumo kwani siyo salama tena na tunapoelekea huenda tukaingia katika matatizo kama hatua za makusudi hazitochukuliwa mapema.

Pia UKAWA huu siyo wakati wa kulala maana tiyari mfumo huu umeshatupunguzia kura zetu, toeni tamko kwa mamlaka husika kabla hatujaingia katika matatizo zaidi.

Nawasilisha.......

We nani uwasemee wananchi? eti hatuna imani! wafuasi wa chagadema mna vituko sana.
 
UKAWA Kazi Kwenu Maana Kuingia Ikulu si Lelemama, Njia Yenu Kuelekea Magogoni si tambalale Kama Mnavyoweza Kudhani. Mapema kabisa Inawabidi Kuchukua Hatua Kukataa Mikakati yote Yenye Kuwapotezea Kura Zenu.

Watu Wanawasililiza tu Ninyi Maana Mabadiriko Yanasubiliwa Kwa Muda Mrefu, WapigaKura Wapo Tayari Kufanya Change Swala ni Ninyi Viongozi Kuzuia Ngiriba Zozote zile Toka CCM na Pia Kuzilinda kura zetu Tutakazowapa.
 
Kuingia kwenye uchaguzi bila kuwa na idadi ya kueleweka ya wapiga kura ni udhaifu ambao hauwezi kuvumilika...

We have got to act...!!
 
Back
Top Bottom