Wananchi Haiti washitaki Umoja wa Mataifa

Wananchi Haiti washitaki Umoja wa Mataifa

juve2012

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
3,343
Reaction score
2,041
Karibu wananchi 1500 wa Haiti wamefungua kesi dhidi ya Umoja wa mataifa wakidai fidia toka kwa Taasisi hiyo kutokana na askari wake kusababisha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu mwishoni mwa mwaka 2010 ambapo hadi hivi sasa umeua zaidi ya watu 8000 na kuathiri zaidi ya watu 600000.

Uchunguzi wa kisayansi umeonyesha kwamba Kipindupindu nchini Haiti kililetwa na askari wa U.N Wenye asili ya Nepal ambako ugonjwa huo umeenea na kuwa sugu.

Katibu mkuu wa U.N,bwana Ban Ki Moon alisema taasisi yake haiwezi kulazimika kisheria kulipa fidia Kutokana na kinga ya kidiplomasia iliyo nayo,hata hivyo alitangaza mpango wa dola bilioni 2.27 Ili kuisaidia Haiti kupambana na ugonjwa huo mwaka 2012.

Mwanzoni mwa mwezi March mwaka huu,wananchi hao wamefungua kesi katika mahakama ya Brooklyn nchini Marekani,wakidai fidia kwa ajili ya vifo na athari ya ugonjwa huo pamoja na gharama za kusafisha na kutengeneza miundo mbinu yake ya maji ambayo askari hao wa U.N walidaiwa kumwagia takamwili zao zilizosababisha maambukizi na kuenea kwa kipindupindu katika nchi ya Haiti ambayo haijawahi kuwa na historia ya ugonjwa huo kwa zaidi ya miaka 100 kabla ya hapo.

Katika kesi hiyo,upande wa mashtaka unataka kutumia hati za umoja huo zinazoonyesha kuwa unaweza Kushitakiwa. Mojawapo ya hati hizo ni makubaliano ya mwaka 2004 yanayoeleza hadhi ya majeshi hayo nchini Haiti ambapo katika sehemu ya maelezo yake imeandikwa kuwa taasisi hiyo itawajibika kwa madhara yoyote ambayo yatasababishwa kwa third party kutokana na makubaliano baina yake na serikali ya Haiti. Uwajibikaji huo ni pamoja na fidia.

Hati nyingine inaeleza kuwa Baraza la Usalama la U.N linawajibika kwa madhara yoyote yanayosababishwa na askari wa majeshi yake wanapokuwa wanatekeleza kazi zao.Hati hii imetumika mara nyingi katika nchi 193 wanachama wa umoja huo na hata Baraza lake la Usalama linaichukulia hati hiyo kama mojawapo ya sera zake rasmi.

Msemaji wa U.N bwana Stephane Dujarric amekataa kuzungumzia chochote juu ya kesi au kinga ya taasisi hiyo akidai kuwa masuala ya kisheria yatabaki kwenye sheria lakini U.N itaendelea kutoa ushirikiano kwa serikali ya Haiti ili kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.

Makundi ya haki za binadamu yalifungua kesi inayofanana na hiyo mwezi wa October mwaka jana Katika mahakama ya Manhattan wakiutuhumu Umoja wa Mataifa kwa kusababisha ugonjwa huo na kudai fidia kwa waathirika.

Walifungua kesi ya "class action status"(kundi la watu wenye maslahi mamoja katika kesi kushitaki kundi au mtu mwingine wenye collective liability) wakitaka misaada kwa waathirika wote wa ugonjwa huo,ambao walidai umeenezwa kwa uchafuzi wa mto mkuu ambao unategemewa na Haiti kwa matumizi ya binadamu.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani bi Jen Psaki alisema kwamba wizara yake imeiandikia ujumbe mahakama ya Manhattan kuieleza kwamba U.N,majeshi yake na Katibu wake mkuu hawawezi kushtakiwa katika kesi hiyo.

Hata hivyo mawakili wa upande wa mashitaka wamesema kuwa Marekani huenda haijui uwepo wa hati hizo.

"Kwa heshima na taadhima kwa serikali ya Marekani,nasema hivi,yeyote anayefikiri U.N ina kinga katika kesi hii,amekosea sana!" alisema Tim Howard,mmojawapo wa mawakili hao.

"Chini ya maazimio na sheria za U.N,kinga iliyoondolewa haiwezi kurudishwa.Na katika hili,U.N ilishajiondolea kinga zamani hata kabla ya tukio hili kutokea." Stanley Alpert,mwanasheria mwingine,alisema kwamba hadhani kama U.N ingetoa kilio hicho cha kinga kama tukio kama hilo lingekuwa limetokea kwenye miji ya New York na Paris."The lack of regard for the value of Haitian lives is distressing and indefensible."alimalizia.

Imetoka Associated Press
 
Nadhani ni vizuri na Tanzania kuishitaki dola ya Ujerumani kwa kuleta ugonjwa wa tauni nchini Tanzania
 
Back
Top Bottom