Wananchi "Demokrasia"! - Wanasiasa"Tumbokrasia"!

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,944
Ndio maana tunaona, baadhi ya wapinzani wakitumika na watawala,ili kuwapindua wapinzani wenzao,kwenye vyama vyao halali....tatizo "Tumbo"

Ndio maana tunawaona,wale waliotuaminisha kuwa wanapigania Demokrasia,
sasa wakiwa bega kwa bega na waliokuwa wakiwalaumu kuminya Demokrasia nchini hapo awali...tatizo "Tumbo"

Ndio maana tunawaona viongozi wakubwa kitaifa,wakigeuka kuwa ma-Chawa wa watawala na kuwatelekeza wale waliowapigia kura huku wakiwaahidi kuwasaidia kuibana serikali itatuwe kero zao,kupitia Bungeni.
Lakini wakiingia Huko wanageuka na kuwa Chawa....tatizo "Tumbo"

Wako wengine kina "Yuda Iskariote" wamejazana serikalini na huko CCM.

Kuanzia ngazi ya Taifa hadi Mashinani,wameliharibia taifa kizazi,kwa kuligeuza na kuwa taifa lenye kipaji cha "Unafiki"....tatizo "Tumbo".

Na wengine wamegeuka mabubu ghafla,hawasemi tena,wala hawataki kusemeshwa,sababu midomo yao iko busy ikimung'unya utamu wa "Asali" ....yote tatizo ni "Tumbo".

Kwa hiyo,wananchi tunaolilia Demokrasia,tusibweteke na kudhani tunao wapigania Demokrasia wa ukweli.

Kinachoendelea ni kila mwanasiasa anatafuta jinsi ya kupenya na kuufikia ulaji,wa tumbo lake na ndugu zake.

Ndio maana nimesema tunao "WANA-TUMBOCRASIA"

Alamsiki....
 
Voicer ongeza kidogo sauti huenda hatimaye wote wakakusikia🚶
 
Tatizo ni la wananchi kuendekeza uoga uliozaa unafiki na uchawa.

Katiba mbovu wakuipigania tunawasakazia wapinzani. Badala ya kuipigania wote.
 
Voicer ongeza kidogo sauti huenda hatimaye wote wakakusikia[emoji124]
@Tindo

Kinachoendelea hivi sasa nchini,haihitajiki hata kupiga kelele,bali kufunguka akili na macho tu.

Samia amekwisha fundishwa jinsi ya kuishi na siasa za nchi hii kwa kutukaanga na mafuta yetu wenyewe.

Nadhani unanielewa mpaka hapo!
 
Tatizo ni la wananchi kuendekeza uoga uliozaa unafiki na uchawa.

Katiba mbovu wakuipigania tunawasakazia wapinzani. Badala ya kuipigania wote.
Nchi hii imekeishaharibiwa kwa kuharibu mifumo ya elimu,hivyo vijana wanakaririshwa bila maarifa yao kichwani.

Ni hiyo Gap inayotumiwa na CCM kuendelea kutawala wananchi.
Huku tukiemdelea kutopea kwenye lindi la umaskini!

Wakati tukizalisha kina Rutto wengi Tanzania.
 
Mabadiliko ya kweli Tanzania yataletwa kwa njia ya mapinduzi iwe ya kiraia au ya kijeshi mwisho.

Hakuna taka taka yoyote inayo itwa uchaguzi itakayo leta mabadiliko ya kweli hapa Tanzania.

: Katika kosa kubwa alilo wahi kufanya Mwalimu Nyerere maisha mwake ni sisi kupata uhuru kwa njia ya amani hili ni kosa kubwa sana alifanya.
 
Mmmh.....[emoji419][emoji188]
 
Back
Top Bottom