elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
SERIKALI imesema mpaka sasa, idadi ya wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro ambao wamenufaika na punguzo la bei la kuunganishiwa umeme vijijini kwa Sh. 27,000 bila kulipishwa gharama za nguzo wanafikia 7,000.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alisema jana kuwa mpango huo ulipoanzishwa Mei, mwaka huu, kwa amri ya Rais John Magufuli, watu 5,000 waliunganishiwa huduma hiyo Juni na Julai peke yake. Alikuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kyeri, wilayani Hai wakati wa uzinduzi wa umeme kwenye kaya zilizonufaika na mpango huo. "Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza Tanzania kwa kuwa na umeme katika maeneo mengi sawa na asilimia 87. Kilimanjaro ina kata 148 ambazo zote zina umeme, una vijiji 519 ambavyo kati yake 453 vina umeme.
Ukiangalia bado kuna vijiji 66 tu ambavyo viko Hai (vitano), Siha (saba), Rombo (vinane), Mwanga (vinne), Moshi (22) na Same (20) ambavyo vinasubiri huduma hiyo," alisema Mgalu. "Mheshimiwa Rais Magufuli ametuagiza tupunguze gharama za kuunganishia wananchi umeme vijijini kutoka Sh. 177,000 hadi Sh. 27,000," alisema.
Naibu Waziri alisema kati ya vijiji 66 vya mkoa wa Kilimanjaro ambavyo bado havijaunganishiwa umeme, vitakavyobakia hadi Desemba mwaka huu ni 35 na kati ya hivyo, serikali imeliagiza Shirika la Umeme (Tanesco) kuchukua vijiji 18 ili iviunganishe. Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu ya mzunguko wa pili utaunganisha vijiji 17 tu vitakavyokuwa vimesalia.
Akiwa katika kijiji hicho, Naibu Waziri huyo wa Nishati, alitoa namba yake ya simu ya mkononi kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na kuwaelekeza 'wambipu' ili awapigie na kutatua kero husika endapo wataambiwa na Tanesco au mkandarasi yeyote kwamba walipie nguzo, nyaya au mita wakati wakipeleka maombi ya kuunganishiwa umeme. Aidha, Mgalu alitoa onyo kwa mameneja wa Tanesco ngazi ya wilaya na mkoa ambao watakaidi agizo la serikali linaloelekeza kuwa wananchi wote wa vijijini waunganishiwe umeme kwa gharama ya Sh. 27,000 tu.
source :NIPASHE