Mkuu, siyo kwamba mie niliishia upenzi wangu na WENGE. Baada ya makundi haya kufa, nilipunguza sana upenzi wangu. Huyu jamaa ndiyo nikiri kabisa kwamba sijamfuatilia kabisa kwa karibu na hivyo siwezi kukupa majina ya hao jamaa. Hata hivyo asante kwa video.
Tatizo kubwa kwa hawa Wanamuziki wengi wa EX-Wenge ni kuwa hawana UONGOZI mzuri inavyokuja kwenye STAGE. Wanafanya vitu vingi kwa kulipua. Wanakuwa kama watu waliozoea kuongozwa. Ukiangalia mara nyingi, jamaa anafanya vitu kwa kuangalia kushoto na kulia aone kama amepatia. Nenda kamuangalie Mzee Nyokalongo, anacheza na kuimba bila kuangalia kushoto wala kulia kwa sababu ana uhakika hakuna anayekosea na yeye pia hakosei....
Ila nakubaliana na wewe kuwa Wacongo wakiwa kwenye STAGE, wanajituma si kawaida.....