Asili, mwanzo na kusambaratika kwa Wenge Musica 4 x 4 bcbg

Roga Roga

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
656
483
Kama nilivyoahidi siku za nyuma, hatimaye naomba nilete kwenu maelezo yaihusuyo iliyokuwa Wenge Musica 4X4 Tout Terrain BCBG.Kiufupi Bendi hii ndiyo ilini-inspire kuupenda muziki wa kongo lakini ujio wa Extra Musica (mwaka 1995) ulinifanya nibadili bendi na kuhamia Extra Musica BPBL. Maelezo yangu yametokana na mkusanyioko wa blog mbalimbali za kikongo. Karibu tupate ku-share mambo mazuri kama nilivyoahidi. contacs ni email; bislisk@yahoo.com

Mwaka 1981 (kati ya Juni-julai) huko Bandalugwa (Bandal), Didier Masela akiwa likizo (alikuwa akisoma huko mji mdogo wa Mbonza boma ulioko Kinshasa) pamoja na Aime Buanga walianzisha wazo la kuimba nyimbo pamoja, baada ya siku chache Noel Ngiama “Werrason” na Alain Mwanga “zing zong” nao walijiunga na Didier Masela & Aime Bwanga. Baada ya Muda Didier Masela akamualika Alain Makaba “Prince” kujiunga nao katika kundi lao, kabla ya mwaliko huu Masela na Makaba waliwahikuwa wote Katika shule ya Kikatoliki ya Notre dame de mbanzaboma na ndipo huko walipojifunzia upigaji wa gitaa. Werrason naye akawaleta Ladins Montana na binamu yake Machiro Kifaya.

Kuelekea mwishoni mwa mwaka huohuo Jean Luvutula alijiunga katika timu hii, na baada ya muda mfupi alimtambulisha schoolmate wake Jean Bedel Tshituka Mpiana “JB Mpiana”. Ilikuwa hivi, Siku moja JB Mpiana akiwa anarudi nyumbani kutoka kwa shangazi yake njiani alikutana na vijana wakiwa wanafanya mazoezi ya kuimba kwa kutafsiri wimbo wa Victoria Eleison uitwao ngabelo. Vijana hao walikuwa ni Werrason, Aime Bwanga, Machiro Kifaya, na Jean Belix Luvutula. Machiro ndiye aliyekuwa anaimba sauti za Debaba wa Victoria Eleison lakini hakuimba kwa ufasaha hasa sauti za juu kama afanyavyo Debaba, kuona hivyo JB akaomba ajaribu kuimba yeye na kufanikiwa kuimba kwa ufasaha na baada ya hapo alirudi nyumbani. Baada ya siku chache Jean Belix Luvutula ambaye alikuwa akisoma shule moja na JB, alimuomba kama anaweza kujiunga nao kwani alionekana ni mwimbaji mzuri naye bila ajizi akajiunga na Wenge Musica, na mazoezi yote walikuwa wanafanyia kwao Didier Masela.

Jean Badel Mpiana naye akaja na mpiga rhythm Christian Zitu, na baada ya siku chache Evo Nsiona mpiga Tumba (Mbonda) naye alijiunga nao. Waimbaji Anicet Pandu “Anibo charm” na Dede Masolo "Deno star" walijiunga na bendi hii Disemba, na baada ya kama wiki mbili hivi mwimbaji Blaise Bula alitambulishwa katika bendi hii ya Wenge na rafiki yake waliyesoma shule moja ambaye sio mwingine ni JB Mpiana.

Mwaka 1982 Adolphe Ebondja “Dominguez” alijiunga na Wenge lakini ukaribu wake na Defao Matumona ukamfanya aende Choc stars (kipindi hiki Defao akiwa bado mwimbaji wa choc stars). Pia mwimbaji Bienvenue Wes Koka na drummer Maradona Lontomba waliwasili kundini. Kiujumla wote walikuwa bado wanafunzi na walifanya mazoezi ya pamoja kipindi cha likizo, baadhi walikosa hata hayo mazoezi sababu wazazi wao hawakuwaruhusu kuchanganya muziki na masomo kwa pamoja. Tamasha lao la kwanza kufanya kama waimbaji ni katika baa ya Olympia kipindi cha likizo mwaka 1982 na baada ya hapo wote wakarudi shule.

Mwaka 1983, na 1984 wakaanza kufanya matamasha zaidi, muda mwingi wakiimba nyimbo za Victoria Eleison na Viva la Musica. Jina la Wenge lilikuja kutoka katika timu ya mpira wa miguu ya huko Bandal iitwayo Wenge, na jina Musica walikopi toka Viva la Musica (ni bendi iliyo wa –inspire). Wakati huo maraisi wa bendi hawakuwa wanamuziki wa kundi hilo. Mfano maraisi wawili wa kwanza wa kundi hili walikuwa ni wafadhili wao ambao ni Papy Kimbi na Mavo Voka. Mwaka 1985 kundi likaanza kubadilika na kufanya kazi zake kiweledi zaidi baada ya kuwa wanapewa nafasi ya kuimba/watumbuizaji wa mwazo katika matamasha yaliyozihusisha bendi za Viva la Musica, Empire Bakuba na Victoria Eleison. Walianza kuimba nyimbo walizo tunga wenyewe kama Laura ya Blaise Bula, Bebe ya Alain Mwangazing zong”, Kin e bouger I na Ginette za JB Mpiana, Caserine ya Werrason na zingine nyingi.
upload_2017-8-2_21-1-12.jpeg

Mwaka 1985 Adolphe Ebondja “Dominguez” rasmi akajiunga na kundi hili, lakini haikuchukua muda wazazi wake wakampeleka Ulaya kwaajiri ya masomo. Ni kipindi hiki ambacho miongoni mwa waasisi ambao ni Aime Buanga na Alain Mwanga “Zing Zong” nao wakapelekwa ulaya na wazazi wao kwa ajiri ya masomo, pia Christian Zitu naye akapelekwa ulaya na wazazi wake na huu ukawa ndio mwisho wa wao kuitumikia Wenge Musica (isipokuwa Dominguez alirejea mwanzoni mwa miaka ya 90). Wengine ni Dédé Masolo "Deno star" aliyejitoa katika bendi na kuwa mchungaji (Muhubiri) huku Wes Koka akiugeukia muziki wa injiri. Taratibu kundi likaanza maandalizi ya album yao ya kwanza, na wakati huohuo Werrason akamgundua mwanamuziki mdogo Alain Mpela Tshwkulenda huko Kingasani (Siyo Kisangani) wakati huo akiwa likizo (kiasili Mpela anatoka mji wa Matete). Alain Mpela alikuwa akiimba nyimbo za Victoria Eleison hasa wimbo Ngabelo ndipo Werrason akamgundua. Pia kipindi hiki mwimbaji Ricoco Bulambemba akajiunga na kundi la Wenge Musica. Mwaka huohuo, mkaanga chipsi (drummer) aitwaye Pipo, mpiga gitaa la rhythm Djolina Mandudila waliwasili katika bendi, pia waliwasili mpiga gitaa la mi-solo Blaise Kombo na mpiga gitaa la besi Eddy Kandimbo.

Wakati wa kiangazi 1987, mwimbaji Marie Paul Kambulu alijiunga na bendi. Mwishoni mwa mwaka huo 1987, Jean Baptise Mileya maaarufu kama Manda Chante alijiunga na bendi lakini yeye akianzia reserve team. Eddy kandimbo alijitoa katika bendi mwanzoni mwa mwaka 1988 na nafasi yake kuchukuliwa na Christian Mwepu Mabanga aliyejiunga mwezi mmoja baadae tangu kuondoka kwa Eddy. Mwanamuziki Christian Mwepu alijiunga siku moja na kaka yake Alain Mwepu aliyekuja kuwa msaidizi wa Alain Makaba katika gitaa la solo.

Kundi liliandaa album yao ya kwanza katika studio ya Bobongo na kwa mara ya kwanza raisi wa kundi alitokana na waimbaji wa kundi. Hadi kufikia mwaka 1988, bendi ilikuwa chini ya uongozi wa wao wenyewe ambao ni Werrason (akiwa Financial Director), Alain Makaba (akiwa Artistic Director) na JB Mpiana (akiwa President). Katika album yao ya kwanza walichagua nyimbo nne tu na kati ya hizo tatu za JB Mpiana na Moja ni Alain Makaba. Hali hii haikumfurahisha Blaise Bula na kusababisha akose sehemu kubwa ya rekodi nyimbo hizi katika studio ya Bobongo na nafasi yake kuchukuliwa na kijana mdogo Alain Mpela ambaye muda mwingi alikuwa anasimama kwenye kreti ya soda akiwa studio ili aweze kuifikia microphone, mwishoni mwa kurekodi album hii Blaise Bula alikubali kushiriki na album hii ikawa mwanzo mzuri wa kundi la Wenge Musica BCBG na kuwazidi mahasimu wao hasa Dakamuda’s Lavinora.

Album yao ya kwanza bouger bouger(maarufu kama Mulolo) ilirekodiwa studio za bobongo ni ya mafanikio japo sio sana, wenge musica kiasi kikubwa iliakisi uimbaji wa Victoria Eleison (Werrason akiimba kama King Kester, blaise Bula kama Joly, Jb Mpiana kama Debaba n.k). Wimbo wa mulolo ulichaguliwa kama wimbo bora wa mwaka Congo kwa kipindi hicho. Katika album ya bouger bouger safu ya waimbaji ilikuwa na Werrason, JB Mpiana, Blaise Bula na Ricoco Bulambemba. (Alain Mpela, Marie Paul na Manda Chante wakitumika kama Reserve), Gitaa la solo akiwa Alain Makaba, Djolina akiwa katika rhythm gitaa, Blaise Kombo akiwa katika mi-solo gitaa, Didier Masela akiwa katika gitaa la besi, Don Pierrot akiwa katika mbonda (tumba), na Maradona akiwa katika drums (mkaanga chips). Atalaku alikuwa ni Noel Ngiama “Werrason”.
upload_2017-8-2_20-56-8.jpeg

Muda mfupi tangu kutoka kwa album hii mpiga gitaa la mi-solo aitwaye Collegien Zola, mpiga gitaa la besi Delo Bass na mwimbaji Jean Didier Loko(JDL) walijiunga na Wenge Musica lakini kabla hata hajamaliza mwezi katika bendi, JDL alipelekwa na wazazi wake masomoni huko Ufaransa hivyo ikawa ndio mwisho wa yeye katika bendi hii. Kundi likawa maarufu sana Kinshasa na Congo kiujumla. Hivyo wakaona wapanue wigo wa kujulikana zaidi Ulaya na duniani kwa ujumla, wakaamua kufanya tour ulaya kwaajili ya kutambulisha album yao ya kwanza na pia kwenda kurekodi album yao ya pili ulaya. Na nikipindi hiki Patient Kusangila alijiunga na kundi kama mpiga gitaa la rhythm sababu ikiwa kundi lilikuwa tayari lina wapiga gitaa la base watatu (ambao ni Didier Masela, Delo Bass na Christian Mwepu Mabanga)

Pia atalaku wa kwanza wa kundi Roberto Wunda alijiunga na Wenge kipindi hiki, akiwa na maataluku wenzake Full King na Kennedy wakitokea kundi liiitwalo Folkloric Group Bana Odeon. Mkaanga chips alikuja kujizolea sifa kibao Titina El capone ambaye ni School mate wa Jb Mpiana na Blaise bula alijiunga na kundi hili. Atalaku Kennedy hakumaliza muda akajitoa katika kundi na kwenda katika kundi la Folkloric Group Swede Swede.

Mwanzoni mwa mwaka 1990 viongozi wa kundi walikamatwa baada ya kujaribu kusafiri kuelekea ulaya wakiwa na hati feki za kusafiria na kuwekwa kizuizini kwa siku nzima, viongozi waliokamatwa ni JB Mpiana, Werrason, Makaba na Masela lakini waliachiwa baadaya watoto wa Raisi wa Congo wa wakati huo Mobutu kuingilia kati. Watoto wa Mobutu ambao ni Manda MobutuMaitre madova”, Nzanga MobutuNovember” na Jose kongolo mobutuSaddam Hussein” ambao walikuwa ni marafiki wakubwa wa bendi hasa kwa JB Mpiana na Werrason. Kukamatwa kwao kulifanya waweke maneno haya katika wimbo wa Kin e Bouge "wele oyo toyoka na sango to vivre yango ba jaloux basepeli basali feti bameli masanga, ba famille na biso mawa na mitema bakolelaka biso"(before we were seeing images of prisons on tv now we've experienced it, our haters are partying and drinking beer, while our families are crying for us). Katika safari hii waliofanikiwa kuingia Ulaya na hati feki ni wawili tu ambao ni drummer Pipo la Musica na mwimbaji Ricoco Bulambemba. Huko Ufaransa, Ricoco Bulabemba na Pipo la Musica, wakaungana na Alain Mwanga “zing zong” na Aime Mbwanga waliokuwa wamemaliza masomo na kuanza mazoezi ya pamoja. Na nikipindi hiki Alain Mwanga “zing zong” na Aime Mbwanga waliwasajiri “recruit” waimbaji kama Ya yuyu, JDT Mulopwé, Savanet Depitsho na Rento Vena, mpiga kinanda Nzenze, mpiga gitaa la besi boss Matuta na mpiga gitaa la rhythm Lidjona, Adolphe Dominguez naye alikuwa ni miongoni mwa walioshiriki mazoezi haya huko Paris.

Julai 1990 Kinshasa, Sintofahamu ikaibuka katika kundi baada ya mpiga gitaa la mi-solo Blaise Kombo kufariki kwa ajari ya gari wakati akirejea nyumbani kutoka kwenye moja ya show za Wenge Musica. Hii ilileta mkanganyiko sana sababu baadhi ya wanachama wa kundi hili walikuja kunukuliwa kuwa ajari hii ilipangwa, na ilikuwa ni atakayekuwa wa kwanza kupanda stejini siku hiyo ya show atafariki, na Blaise Kombo alikuwa wa kwanza kupanda stejini kwenda kutest sauti la gitaa lake akifuatiwa na Maradona. Baada ya tukio hili Maradona na Delo Base walijitoa katika bendi.

Mwaka 1991 hatimaye bendi ikafanikiwa kufika Paris bila uwepo wa Manda Chante, Atalaku Full King na Alain Mpela (aliyekuwa kwenye mitihani na nafasi yake kuchukuliwa Marie Paul Kumbulu), Wakarekodi album yao ya Kin e Bouger iliyokuwa na mafanikio makubwa huku JB Mpiana akipata tuzo ya mwimbaji bora kutoka Kongo. Moja ya kivutio katika album hii ya Kin e bouge ni kuwepo waimbaji watatu wa base (Werrason, Marie Paul na Blaise Bula) ambao wanaimba pamoja na wanang’ara. Baada ya album hii Adolphe Dominguez akajiunga na bendi kwa mara nyingine baada ya masomo huku Marie Paul Kumbulu akijitoa Jumla katika bendi akihisi kutothaminiwa na viongozi wa bendi.
upload_2017-8-2_20-58-31.jpeg

Marie Paul Kumbulu akaungana na Alain Mwanga, Aime Mbwanga na Bulambemba, muda mfupi atalaku Full king aliyekua amejitoa wenge muda mrefu, akajiunga. Ujio wa Marie Paul ukabadilisha mtazamo kutoka mazoezi na kuunda kundi la Wenge Musica Aile Paris, baadae walikuaja kurekodi album ya kwanza ya Wenge Musica Aile Paris iitwayo Molangi ya malasi (perfume bottle), ambao wimbo wa molangi ya malasi uliotungwa na Ricoco Bulambemba ulitakiwa kuwa ni moja ya nyimbo katika album ya Kin e Bouge ya Wenge. Mwaka 1992 wakatoa album ya pili iitwayo Nganga Nzambe na baadaye drummer maradona aliyekuwa amejitoa wenge siku nyingi, akajiunga Wenge Aile Paris. Mwaka 1993 mgogoro ukaibuka na kumfanya Aime bwanga ajitoe na kuunda kundi lake liitwalo Wenge Musica Aile Paris Kumbela, na ni kipindi hiki Manda chante naye akajitoa Wenge Musica 4x4 BCBG baada ya album ya Kalayi Boieng kutoka. Huko Ufaransa Manda Chante akajiunga na Ricoco, Alain Mwanga na Marie Paul na kubadili jina toka Wenge Aile Paris (Paris-based wenge) kutokana na kujitoa kwa Aime Mbwanga na kuwa Wenge El Paris (wenge who is the king of Paris).
upload_2017-8-2_20-54-42.jpeg
upload_2017-8-2_21-8-37.jpeg
upload_2017-8-2_21-8-3.jpeg

Tukirudi upande wa Wenge Musica BCBG baada ya Kin E bouge kutoka, Mwaka 1992 kundi likarekodi album ya Pleins Feux huko Brussels ikiwa na nyimbo kama Djolino ya Werrason, Dady Bitodi mtunzi akiwa Djolina, Ave Maria ya Blaise Bula n.k. Ni katika album hii mpiga gitaa la mi-solo Fifi Mwamba "Ficarré Ngenge" Na mpiga kinanda Désiré kalala walijiunga na kundi na kushiriki katika kurekodi, pia mwimbaji Manda Chante alishiriki katika album hii. Album hii ilirekodiwa tu na haikutoka kwa wakati sababu ikiwa ni mgogoro kati ya moja ya watoto wa Mobutu ambaye ni Jose kongolo Mobutu a.k.a Saddam Husein. Chanzo cha mgogoro huu inaelezwa kuwa ni mwanamke aliyekubali kuwa mpenzi wa JB (kabla JB hajawa na Amida Shatur) na kumtosa Kongolo Mobutu, hivyo naye akaamuwa kuwaadhibu kwa kutoruhusu album hii kwenda sokoni mpaka pale mwanamke huyu alipokubali kuwa upande wa Saddam Hussein. Album hii ilikuja kuingia sokoni miaka minne tangu kurekodiwa baada ya Kalayi boing (1993) na Les Anges Adorables (1994) kuwa zimetoka.
upload_2017-8-2_21-2-46.jpeg

Mwaka 1993 kundi likarekodi album ya Kalayi Boeing huko Ulaya na kutoka mwaka huo huo, muda mfupi baada ya album hii kutoka, Manda Chante (anayesika sana katika wimbo wa kalayi Boieng) akajitoa na kujiunga Wenge El Paris (Rejea maelezo ya aya hapo juu). Alijitoa baada ya viongozi wa kundi kutoonyesha ushirikiano wowote alipougua ugonjwa wa ajabu wa ngozi (matete kuwanga). Alimshutumu sana Werrason kushindwa kumlipa hela kipindi alichokuwa anaumwa. Manda Chante miaka ya hivi karibuni amekuwa akihusisha ugonjwa huu na nguvu za giza huku shutuma kali akizipeleka kwa JB Mpiana kuwa alitaka kumuua kutokana na sauti yake manda chante kupendwa sana wakati album hii inatoka.

upload_2017-8-2_20-59-16.jpeg

Baada ya kujitoa kwa Manda Chante, kundi likarejea nyumbani na kuanza kutafuta mbadala wa Manda chante. Wengi wakajitokeza kwenye majaribio ili apatikane wa kuziba pengo la Manda chante. Baaadhi watu maarufu waliojitokeza katika usaili huo ni Babia Chokoro (ni former mate group wa manda chante huko Yoka Choc), Papy Sesele “Adjani sesele”, Blaise Yombo Lumbu maarufu kama Tutu Caludji, na Aimelia Lias Miankodila ambaye alishinda kinyang’anyiro hicho na hivyo kuwa mbadala wa Manda chante. Lakini Tutu Caludji akapelekwa katika sekta ya uatalaku baada ya kuonekana pia anaweza kughani. Pia baada ya album hii ya Kalayi Boieng, Alain Makaba aliamua kubaki ulaya na kufanya makazi yake huko, hivyo Ficarré mwamba akawa mpiga gitaa la solo kiongozi, na baadaye Vincent Kasongo Mbokaliya Burkina Faso akajiunga katika kundi. Na ni kipindi hiki Ali Mbonda alijiunga ili kuziba pengo la Don Pierrot aliyekua amejitoa wakati bendi ilipofanya tour ulaya mwaka 1992.
upload_2017-8-2_21-4-33.jpeg

Mwaka 1994 Kundi likarejea ulaya tena kwa ajili ya tour bila uwepo wa Tutu Caludji na Mboka liya na kurekodi album iliyofuatia ya Les Anges Adorables ambayo ni moja ya album bora kabisa za wenge Musica (Album hii ina kopi mbili yaani Version I and Version II). Baada ya album hii Papa Denewade aliwashauri viongozi wanne ambao ni waasisi (Yaani Makaba, Masela, Werrason na JB Mpiana) kila moja kutoa album yake kama solo. Hivyo Alain Makaba akawa wa kwanza kutoa album iitwayo Pile ou Face mwaka mmoja baadae yaani 1995, ambapo aliwashirikisha wanamuziki watatu tu toka Wenge, ambao ni Titina, Le Grand Chibuta Roberto Ekokota na Jb Mpiana, wengine hawakuwa member wa Wenge maana aliwashirikisha mzee Sam Mangwana, Dindo Yogo, Luciana Demingongo, Abby Suriya, Ballou Canta na King Kester Emeneya.

Mwaka 1995, Burkina Faso akawa mpiga gitaa la solo kiongozi Kinshasa (kumbuka Makaba alikuwa kaweka makazi ulaya). Mwaka huo huo bendi ikamsajili mpiga gitaa Fiston Savimpi Zamuangana (Mtoto wa Enoch Zamuangana wa Zaiko Langa langa) na muimbaji Hervé Gola Bataringe maarufu kama Ferre Chair De Poule wote kutoka kundi la Des Jeunes, na pia mpiga drummer na tumba (mbonda) aitwaye Blaise Seguin Bongongo maarufu kama Seguin Mignon akitokea Kibinda nkoyi.

Mwaka 1996 bendi ikafanya tour Marekani bila ya Alain Makaba aliyekuwa ulaya, baadae bendi ikaenda Ubeligiji na kurekodi album ya Pentagone huku Alain Makaba akishiriki kikamirifu, baada ya kurejea Kinshasa Japonais Maladi Kambuku alijiunga na Wenge akitokea Japana group. Na nikipindi hiki ndipo ubinafsi ukaanza kuonekana kati ya JB Mpiana na Werrason hasa baada ya JB mpiana na producer Simon Ndjonang “Simon Music” kuanza kurekodi album ya Feux de L'amour kama solo album ya JB Mpiana. Werrason hakukubaliana na wazo la JB Mpiana sababu ikiwa ni tayari walishaanza maandalizi ya album mpya ya kundi na kuipromote album ya Pentagone iliyokuwa tayari sokoni, lakini mwisho wa siku album ya Feux de L'amour ikatoka mwishoni kabisa wa mwaka 1996. Tofauti na mwenzake Makaba aliyetumia wanamuziki watatu tu wa Wenge, JB Mpiana alitumia takribani bendi nzima huku mwanamuziki mwalikwa akiwa ni mmoja tu tena mshauri wake Papa Wemba ambaye naye aliishiriki wimbo mmoja tu uitwao Cavalier Solitaire.
upload_2017-8-2_21-3-38.jpeg

Sintofahamu iliendelea na kuigawa bendi katika makundi mawili yaani kundi la Werrason (akiwa supported na Masela na Adolph Dominguez) na kundi la JB Mpiana ambalo kwa sehemu kubwa ni wanamuziki wengi wa Wenge (kama Blaise Bula, Makaba, Alain Mpela, Aimelia, Ficcare Mwamba, n.k). Hatimaye disemba 1997 rasmi kundi likagawanyika na kuwa vipande viwili (Yaani Wenge Musica Maison Mere na Wenge BCBG)
upload_2017-8-2_21-6-45.jpeg
upload_2017-8-2_21-7-23.jpeg

Moja ya vituko vilivyotokea wakati bendi ipo katika mgogoro ni hiki cha 1997 huko Kinshasa ndani ya Grand Kin Hotel ambapo kulifanyika concert maalumu ya kuitambulisha album ya Faux de L'Amour ambayo hakuna mpenzi wa muziki hasa wa wenge ndani ya congo ataisahau maana concert hiyo ilikuja kubatizwa kama “concert de la separation” ambapo yalitokea majibishano makali baina ya Werrason na Blaise Bula mbele ya Papa Wemba ambae alikuja hapo kama mualikwa, Kiufupi tu ni kwamba Baise Bula na Werrason siku hiyo walitukanana sana, Blaise Bula akamwambia Werrason maneno hayo “rafiki yangu kila siku unaota uwe kama mimi,uwe kama Jb,uwe kama Makaba,hizo ni ndoto kaka yangu” mwisho wa kunukuu.

(KUHUSU SABABU ZA MGOGORO HUU ULIOIGAWA WENGE MUSICA FUATILIA LINK HIZI HAPA CHINI).

SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu ya I) (sehemu ya kwanza mpaka ya nane)

1. Album Bouger Bouger (1988)

1. Bakolo budget (JB Mpiana)
2. Fisol (Alain Makaba
3. La fille du roi (JB Mpiana)
4. Mulolo (JB Mpiana)

2. Album Kin E Bouge (1991)

1. Eve Sukali (Blaise-Bula
2. Kaskin (Werrason)
3. Kin E Bougé (J.B. M'Piana)
4. Ngoma Maguy (Roberto Ekokota)
5. Princesse Pathy (Alain Makaba)

3. Album Kalayi Boeing (1993)
1. C'est trop tard Djenga (Alain Makaba)
2. Cresois (Didier Masela)
3. Danico (JB Mpiana)
4. Jessy couchou de london (Blaise Bula)
5. Kala Yi Boeing (Werrason)
6. Mon ami coboss (JB Mpiana)
7. Voyage Mboso (Adolphe Dominguez)

4. Album ya Les Anges Adorable (1994)
a) Version I

1. Douglas Ilumbe (Alain Makaba)
2. Hi Ho Ha New Image (JB Mpiana)
3. La tempete du désert (Didier Massela)
4. Lavie (Adolphe Dominguez)
5. Surprise Kapangala(Werrason)
6. Tuna Tina Jack KitshindJa (Alain Makaba)

b) Version II

7. Capitaine de Benelux (JB Mpiana)
8. Kama (Titina Mbwinga 'el capone)
9. Masampu (Blaise Bula)
10. Promesse bouboule (Alain Mpela)
11. Sourires Des Vendeurs (Werrason)
12. Willy muntu (Didier Massela)

5. Album Pleins Feux (1995)

1. Ambiance instrument
2. Ave maria ( Blaise Bula)
3. Dady bitodi (Djolina)
4. Djino (Werrason)
5. La vie
6. Nazareth
7. Tchacho mbala

6. Album Pentagone (1996)

1. Pentagone (Roberto Wunda Ekokota)
2. Coco Madimba( Werrason)
3. Dizo izo (Alan Prince Makaba)
4. Djojo Ngonda (Fi Carre Mwamba)
5. Etepé Buengoi (Didier Massela)
6. Filandu (Blaise Bula)
7. Héritier Itele (Werrason)
8. No comment Shengen (J.B Mpiana)
9. Roco Martini (Adolphe Dominguez
10. Daddet (Autant)(Didier Massela)
11. Cometes de L'an 2000 (Patient Kusangila)

Waasisi
Didier Masela; 1981-1997 (gitaa la besi/ kiongozi, Muasisi mkuu)
Werrason Ngiama Makanda "Nkoyi de la forêt" 1981-1997 (kiongozi wa fedha, muasisi mwandamizi, mwimbaji)
Aimé Bwanga 1981-1986 (gitaa la besi, muasisi mwandamizi)
Alain Mwanga "Docteur Zing" 1981-1986 (gitaa la solo, na mi-solo),(muasisi mwandamizi)
Jean-Belis Luvutula 1981-1987 (Muasisi mwandamizi

Waimbaji
JB Mpiana "Mukulumpa" 1981-1997 (Raisi wa kundi);
Machiro Kifaya, 1981-1982;
Dede Masolo "Deno Star", 1981-1986 ;
Anibo Panzu, 1981-1986 ;
Blaise Bula Monga "Ingénieur Celebu", 1981-1997 (Chef d'Orchestre wa kwanza, kiongozi);
Adolphe Dominguez Ebodja 1981-1997 (kiongozi na pia kama mnenguaje);
Bienvenue Wes Koka 1982-1985;
Ricoco Bulambemba "le fils de Mbulamatari", 1986-1989;
Alain Mpelasi Tshwakulenda, 1986-1997 ;
Marie Paul Kambulu "Atshisa Bélési", 1987-1991;
Manda Chante, 1987-1993;
Aimélia Lias Demingongo, 1993-1997;
Ferre Gola, 1995-1997.

Wapiga gitaa na kinanda
Alain "Prince" Mabaka 1981-1997 (gitaa la solo, mi-solo na besi, kinanda, tumba, kiongozi, arranger na Artistic Director);
Christian Zitu 1981-1985 (gitaa la rhythm);
Djolina Mandudila 1985-1992 (gitaa la rhythm);
Kandimbo Eddy 1986-1989 (gitaa la besi);
Blaise Kombo 1986-1990 (Alifariki Julai 1990) (gitaa la mi-solo);
Alain Mwepu 1988-1993 (gitaa la solo na mi-solo);
Delo Bass 1989-1990 (gitaa la besi);
Patient Kusangila Lutu
1989-1997 (gitaa la solo na rhythm);
Aridjana Solo 1984-1990 (gitaa la mi-solo);
Collegien Zola 1988-1992 (gitaa la rhythm);
Christian Mwepu Mabanga 1988-1997 (gitaa la besi);
Master Ficarré Mwamba 1991-1997 (gitaa la solo na mi-solo);
Kalala desired "Syntha-syntha"1991-1993 (kinanda),;
Burkina Faso Mbokaliya 1993-1997,(gitaa la solo na mi-solo);
Japanese Kambuku Maladi 1996-1997. (Gitaa la solo, mi-solo na besi);
Theo Bidens Kiavuanga 1996-1997 (kinanda);
Son Zamuangana Savimpi 1996-1997 (gitaa la rhythm);

Ngoma na Tumba (mbonda)

Ladin Montana
1981-1987 (ngoma);
Evo Nsiona Adiataki 1981-1988 (ngoma);
Maradona Lontomba 1981-1990 (ngoma);
Pipo la Musica (ngoma) 1987-1989;
Titina Mbwinga "Al Capone" 1988-1997 (ngoma);
Don Pierrot Mbonda1988-1993 (ngoma / mbonda);
Ali Mbonda 1993-1997 (mbonda);
Seguin Mignon Bongongo 1996-1997 (ngoma / mbonda).

Atalaku
Kennedy Mbala"na ba Mputu",1988-1989;
Full King, 1986-1993;
Roberto Wunda Ekokota, 1988-1997;
Tutu Caludji, 1993-1997.

Wanenguaji
Mama Rosa 1990 to 1991
Nana Boanga 1993-1996;
Carine Evoloko 1993-1995; ''
 
Attachments

  • upload_2017-8-2_21-6-17.jpeg
    upload_2017-8-2_21-6-17.jpeg
    8.3 KB · Views: 267
Aisee Hongera sana kwa kuwaelezea vizuri kwa kinaga ubaga hawa jamaa.

Nilikuwa nikiwasikiliza nikiwa kid na kucheza nyimbo zao ila sikujua historia yao.

Sasahv Werrason na JB Mpiana ndio wanachuana vikali sio?
 
Nakumbuka mwaka 1997 marehemu mama (Mungu amrehemu) alinunua albamu ya faux de L'Amour,na tulikua tunaicheza sana kipindi hicho nipo Kakola Salawe,na ngoma ya Masuwa mpaka leo inanikuna sana.
 
Kama nilivyoahidi siku za nyuma, hatimaye naomba nilete kwenu maelezo yaihusuyo iliyokuwa Wenge Musica 4X4 Tout Terrain BCBG.Kiufupi Bendi hii ndiyo ilini-inspire kuupenda muziki wa kongo lakini ujio wa Extra Musica (mwaka 1995) ulinifanya nibadili bendi na kuhamia Extra Musica BPBL. Maelezo yangu yametokana na mkusanyioko wa blog mbalimbali za kikongo. Karibu tupate ku-share mambo mazuri kama nilivyoahidi. contacs ni email; bislisk@yahoo.com

Mwaka 1981 (kati ya Juni-julai) huko Bandalugwa (Bandal), Didier Masela akiwa likizo (alikuwa akisoma huko mji mdogo wa Mbonza boma ulioko Kinshasa) pamoja na Aime Buanga walianzisha wazo la kuimba nyimbo pamoja, baada ya siku chache Noel Ngiama “Werrason” na Alain Mwanga “zing zong” nao walijiunga na Didier Masela & Aime Bwanga. Baada ya Muda Didier Masela akamualika Alain Makaba “Prince” kujiunga nao katika kundi lao, kabla ya mwaliko huu Masela na Makaba waliwahikuwa wote Katika shule ya Kikatoliki ya Notre dame de mbanzaboma na ndipo huko walipojifunzia upigaji wa gitaa. Werrason naye akawaleta Ladins Montana na binamu yake Machiro Kifaya.

Kuelekea mwishoni mwa mwaka huohuo Jean Luvutula alijiunga katika timu hii, na baada ya muda mfupi alimtambulisha schoolmate wake Jean Bedel Tshituka Mpiana “JB Mpiana”. Ilikuwa hivi, Siku moja JB Mpiana akiwa anarudi nyumbani kutoka kwa shangazi yake njiani alikutana na vijana wakiwa wanafanya mazoezi ya kuimba kwa kutafsiri wimbo wa Victoria Eleison uitwao ngabelo. Vijana hao walikuwa ni Werrason, Aime Bwanga, Machiro Kifaya, na Jean Belix Luvutula. Machiro ndiye aliyekuwa anaimba sauti za Debaba wa Victoria Eleison lakini hakuimba kwa ufasaha hasa sauti za juu kama afanyavyo Debaba, kuona hivyo JB akaomba ajaribu kuimba yeye na kufanikiwa kuimba kwa ufasaha na baada ya hapo alirudi nyumbani. Baada ya siku chache Jean Belix Luvutula ambaye alikuwa akisoma shule moja na JB, alimuomba kama anaweza kujiunga nao kwani alionekana ni mwimbaji mzuri naye bila ajizi akajiunga na Wenge Musica, na mazoezi yote walikuwa wanafanyia kwao Didier Masela.

Jean Badel Mpiana naye akaja na mpiga rhythm Christian Zitu, na baada ya siku chache Evo Nsiona mpiga Tumba (Mbonda) naye alijiunga nao. Waimbaji Anicet Pandu “Anibo charm” na Dede Masolo "Deno star" walijiunga na bendi hii Disemba, na baada ya kama wiki mbili hivi mwimbaji Blaise Bula alitambulishwa katika bendi hii ya Wenge na rafiki yake waliyesoma shule moja ambaye sio mwingine ni JB Mpiana.

Mwaka 1982 Adolphe Ebondja “Dominguez” alijiunga na Wenge lakini ukaribu wake na Defao Matumona ukamfanya aende Choc stars (kipindi hiki Defao akiwa bado mwimbaji wa choc stars). Pia mwimbaji Bienvenue Wes Koka na drummer Maradona Lontomba waliwasili kundini. Kiujumla wote walikuwa bado wanafunzi na walifanya mazoezi ya pamoja kipindi cha likizo, baadhi walikosa hata hayo mazoezi sababu wazazi wao hawakuwaruhusu kuchanganya muziki na masomo kwa pamoja. Tamasha lao la kwanza kufanya kama waimbaji ni katika baa ya Olympia kipindi cha likizo mwaka 1982 na baada ya hapo wote wakarudi shule.

Mwaka 1983, na 1984 wakaanza kufanya matamasha zaidi, muda mwingi wakiimba nyimbo za Victoria Eleison na Viva la Musica. Jina la Wenge lilikuja kutoka katika timu ya mpira wa miguu ya huko Bandal iitwayo Wenge, na jina Musica walikopi toka Viva la Musica (ni bendi iliyo wa –inspire). Wakati huo maraisi wa bendi hawakuwa wanamuziki wa kundi hilo. Mfano maraisi wawili wa kwanza wa kundi hili walikuwa ni wafadhili wao ambao ni Papy Kimbi na Mavo Voka. Mwaka 1985 kundi likaanza kubadilika na kufanya kazi zake kiweledi zaidi baada ya kuwa wanapewa nafasi ya kuimba/watumbuizaji wa mwazo katika matamasha yaliyozihusisha bendi za Viva la Musica, Empire Bakuba na Victoria Eleison. Walianza kuimba nyimbo walizo tunga wenyewe kama Laura ya Blaise Bula, Bebe ya Alain Mwangazing zong”, Kin e bouger I na Ginette za JB Mpiana, Caserine ya Werrason na zingine nyingi. View attachment 556604

Mwaka 1985 Adolphe Ebondja “Dominguez” rasmi akajiunga na kundi hili, lakini haikuchukua muda wazazi wake wakampeleka Ulaya kwaajiri ya masomo. Ni kipindi hiki ambacho miongoni mwa waasisi ambao ni Aime Buanga na Alain Mwanga “Zing Zong” nao wakapelekwa ulaya na wazazi wao kwa ajiri ya masomo, pia Christian Zitu naye akapelekwa ulaya na wazazi wake na huu ukawa ndio mwisho wa wao kuitumikia Wenge Musica (isipokuwa Dominguez alirejea mwanzoni mwa miaka ya 90). Wengine ni Dédé Masolo "Deno star" aliyejitoa katika bendi na kuwa mchungaji (Muhubiri) huku Wes Koka akiugeukia muziki wa injiri. Taratibu kundi likaanza maandalizi ya album yao ya kwanza, na wakati huohuo Werrason akamgundua mwanamuziki mdogo Alain Mpela Tshwkulenda huko Kingasani (Siyo Kisangani) wakati huo akiwa likizo (kiasili Mpela anatoka mji wa Matete). Alain Mpela alikuwa akiimba nyimbo za Victoria Eleison hasa wimbo Ngabelo ndipo Werrason akamgundua. Pia kipindi hiki mwimbaji Ricoco Bulambemba akajiunga na kundi la Wenge Musica. Mwaka huohuo, mkaanga chipsi (drummer) aitwaye Pipo, mpiga gitaa la rhythm Djolina Mandudila waliwasili katika bendi, pia waliwasili mpiga gitaa la mi-solo Blaise Kombo na mpiga gitaa la besi Eddy Kandimbo.

Wakati wa kiangazi 1987, mwimbaji Marie Paul Kambulu alijiunga na bendi. Mwishoni mwa mwaka huo 1987, Jean Baptise Mileya maaarufu kama Manda Chante alijiunga na bendi lakini yeye akianzia reserve team. Eddy kandimbo alijitoa katika bendi mwanzoni mwa mwaka 1988 na nafasi yake kuchukuliwa na Christian Mwepu Mabanga aliyejiunga mwezi mmoja baadae tangu kuondoka kwa Eddy. Mwanamuziki Christian Mwepu alijiunga siku moja na kaka yake Alain Mwepu aliyekuja kuwa msaidizi wa Alain Makaba katika gitaa la solo.

Kundi liliandaa album yao ya kwanza katika studio ya Bobongo na kwa mara ya kwanza raisi wa kundi alitokana na waimbaji wa kundi. Hadi kufikia mwaka 1988, bendi ilikuwa chini ya uongozi wa wao wenyewe ambao ni Werrason (akiwa Financial Director), Alain Makaba (akiwa Artistic Director) na JB Mpiana (akiwa President). Katika album yao ya kwanza walichagua nyimbo nne tu na kati ya hizo tatu za JB Mpiana na Moja ni Alain Makaba. Hali hii haikumfurahisha Blaise Bula na kusababisha akose sehemu kubwa ya rekodi nyimbo hizi katika studio ya Bobongo na nafasi yake kuchukuliwa na kijana mdogo Alain Mpela ambaye muda mwingi alikuwa anasimama kwenye kreti ya soda akiwa studio ili aweze kuifikia microphone, mwishoni mwa kurekodi album hii Blaise Bula alikubali kushiriki na album hii ikawa mwanzo mzuri wa kundi la Wenge Musica BCBG na kuwazidi mahasimu wao hasa Dakamuda’s Lavinora.

Album yao ya kwanza bouger bouger(maarufu kama Mulolo) ilirekodiwa studio za bobongo ni ya mafanikio japo sio sana, wenge musica kiasi kikubwa iliakisi uimbaji wa Victoria Eleison (Werrason akiimba kama King Kester, blaise Bula kama Joly, Jb Mpiana kama Debaba n.k). Wimbo wa mulolo ulichaguliwa kama wimbo bora wa mwaka Congo kwa kipindi hicho. Katika album ya bouger bouger safu ya waimbaji ilikuwa na Werrason, JB Mpiana, Blaise Bula na Ricoco Bulambemba. (Alain Mpela, Marie Paul na Manda Chante wakitumika kama Reserve), Gitaa la solo akiwa Alain Makaba, Djolina akiwa katika rhythm gitaa, Blaise Kombo akiwa katika mi-solo gitaa, Didier Masela akiwa katika gitaa la besi, Don Pierrot akiwa katika mbonda (tumba), na Maradona akiwa katika drums (mkaanga chips). Atalaku alikuwa ni Noel Ngiama “Werrason”.View attachment 556600

Muda mfupi tangu kutoka kwa album hii mpiga gitaa la mi-solo aitwaye Collegien Zola, mpiga gitaa la besi Delo Bass na mwimbaji Jean Didier Loko(JDL) walijiunga na Wenge Musica lakini kabla hata hajamaliza mwezi katika bendi, JDL alipelekwa na wazazi wake masomoni huko Ufaransa hivyo ikawa ndio mwisho wa yeye katika bendi hii. Kundi likawa maarufu sana Kinshasa na Congo kiujumla. Hivyo wakaona wapanue wigo wa kujulikana zaidi Ulaya na duniani kwa ujumla, wakaamua kufanya tour ulaya kwaajili ya kutambulisha album yao ya kwanza na pia kwenda kurekodi album yao ya pili ulaya. Na nikipindi hiki Patient Kusangila alijiunga na kundi kama mpiga gitaa la rhythm sababu ikiwa kundi lilikuwa tayari lina wapiga gitaa la base watatu (ambao ni Didier Masela, Delo Bass na Christian Mwepu Mabanga)

Pia atalaku wa kwanza wa kundi Roberto Wunda alijiunga na Wenge kipindi hiki, akiwa na maataluku wenzake Full King na Kennedy wakitokea kundi liiitwalo Folkloric Group Bana Odeon. Mkaanga chips alikuja kujizolea sifa kibao Titina El capone ambaye ni School mate wa Jb Mpiana na Blaise bula alijiunga na kundi hili. Atalaku Kennedy hakumaliza muda akajitoa katika kundi na kwenda katika kundi la Folkloric Group Swede Swede.

Mwanzoni mwa mwaka 1990 viongozi wa kundi walikamatwa baada ya kujaribu kusafiri kuelekea ulaya wakiwa na hati feki za kusafiria na kuwekwa kizuizini kwa siku nzima, viongozi waliokamatwa ni JB Mpiana, Werrason, Makaba na Masela lakini waliachiwa baadaya watoto wa Raisi wa Congo wa wakati huo Mobutu kuingilia kati. Watoto wa Mobutu ambao ni Manda MobutuMaitre madova”, Nzanga MobutuNovember” na Jose kongolo mobutuSaddam Hussein” ambao walikuwa ni marafiki wakubwa wa bendi hasa kwa JB Mpiana na Werrason. Kukamatwa kwao kulifanya waweke maneno haya katika wimbo wa Kin e Bouge "wele oyo toyoka na sango to vivre yango ba jaloux basepeli basali feti bameli masanga, ba famille na biso mawa na mitema bakolelaka biso"(before we were seeing images of prisons on tv now we've experienced it, our haters are partying and drinking beer, while our families are crying for us). Katika safari hii waliofanikiwa kuingia Ulaya na hati feki ni wawili tu ambao ni drummer Pipo la Musica na mwimbaji Ricoco Bulambemba. Huko Ufaransa, Ricoco Bulabemba na Pipo la Musica, wakaungana na Alain Mwanga “zing zong” na Aime Mbwanga waliokuwa wamemaliza masomo na kuanza mazoezi ya pamoja. Na nikipindi hiki Alain Mwanga “zing zong” na Aime Mbwanga waliwasajiri “recruit” waimbaji kama Ya yuyu, JDT Mulopwé, Savanet Depitsho na Rento Vena, mpiga kinanda Nzenze, mpiga gitaa la besi boss Matuta na mpiga gitaa la rhythm Lidjona, Adolphe Dominguez naye alikuwa ni miongoni mwa walioshiriki mazoezi haya huko Paris.

Julai 1990 Kinshasa, Sintofahamu ikaibuka katika kundi baada ya mpiga gitaa la mi-solo Blaise Kombo kufariki kwa ajari ya gari wakati akirejea nyumbani kutoka kwenye moja ya show za Wenge Musica. Hii ilileta mkanganyiko sana sababu baadhi ya wanachama wa kundi hili walikuja kunukuliwa kuwa ajari hii ilipangwa, na ilikuwa ni atakayekuwa wa kwanza kupanda stejini siku hiyo ya show atafariki, na Blaise Kombo alikuwa wa kwanza kupanda stejini kwenda kutest sauti la gitaa lake akifuatiwa na Maradona. Baada ya tukio hili Maradona na Delo Base walijitoa katika bendi.

Mwaka 1991 hatimaye bendi ikafanikiwa kufika Paris bila uwepo wa Manda Chante, Atalaku Full King na Alain Mpela (aliyekuwa kwenye mitihani na nafasi yake kuchukuliwa Marie Paul Kumbulu), Wakarekodi album yao ya Kin e Bouger iliyokuwa na mafanikio makubwa huku JB Mpiana akipata tuzo ya mwimbaji bora kutoka Kongo. Moja ya kivutio katika album hii ya Kin e bouge ni kuwepo waimbaji watatu wa base (Werrason, Marie Paul na Blaise Bula) ambao wanaimba pamoja na wanang’ara. Baada ya album hii Adolphe Dominguez akajiunga na bendi kwa mara nyingine baada ya masomo huku Marie Paul Kumbulu akijitoa Jumla katika bendi akihisi kutothaminiwa na viongozi wa bendi.
View attachment 556602

Marie Paul Kumbulu akaungana na Alain Mwanga, Aime Mbwanga na Bulambemba, muda mfupi atalaku Full king aliyekua amejitoa wenge muda mrefu, akajiunga. Ujio wa Marie Paul ukabadilisha mtazamo kutoka mazoezi na kuunda kundi la Wenge Musica Aile Paris, baadae walikuaja kurekodi album ya kwanza ya Wenge Musica Aile Paris iitwayo Molangi ya malasi (perfume bottle), ambao wimbo wa molangi ya malasi uliotungwa na Ricoco Bulambemba ulitakiwa kuwa ni moja ya nyimbo katika album ya Kin e Bouge ya Wenge. Mwaka 1992 wakatoa album ya pili iitwayo Nganga Nzambe na baadaye drummer maradona aliyekuwa amejitoa wenge siku nyingi, akajiunga Wenge Aile Paris. Mwaka 1993 mgogoro ukaibuka na kumfanya Aime bwanga ajitoe na kuunda kundi lake liitwalo Wenge Musica Aile Paris Kumbela, na ni kipindi hiki Manda chante naye akajitoa Wenge Musica 4x4 BCBG baada ya album ya Kalayi Boieng kutoka. Huko Ufaransa Manda Chante akajiunga na Ricoco, Alain Mwanga na Marie Paul na kubadili jina toka Wenge Aile Paris (Paris-based wenge) kutokana na kujitoa kwa Aime Mbwanga na kuwa Wenge El Paris (wenge who is the king of Paris).
View attachment 556598View attachment 556620View attachment 556619

Tukirudi upande wa Wenge Musica BCBG baada ya Kin E bouge kutoka, Mwaka 1992 kundi likarekodi album ya Pleins Feux huko Brussels ikiwa na nyimbo kama Djolino ya Werrason, Dady Bitodi mtunzi akiwa Djolina, Ave Maria ya Blaise Bula n.k. Ni katika album hii mpiga gitaa la mi-solo Fifi Mwamba "Ficarré Ngenge" Na mpiga kinanda Désiré kalala walijiunga na kundi na kushiriki katika kurekodi, pia mwimbaji Manda Chante alishiriki katika album hii. Album hii ilirekodiwa tu na haikutoka kwa wakati sababu ikiwa ni mgogoro kati ya moja ya watoto wa Mobutu ambaye ni Jose kongolo Mobutu a.k.a Saddam Husein. Chanzo cha mgogoro huu inaelezwa kuwa ni mwanamke aliyekubali kuwa mpenzi wa JB (kabla JB hajawa na Amida Shatur) na kumtosa Kongolo Mobutu, hivyo naye akaamuwa kuwaadhibu kwa kutoruhusu album hii kwenda sokoni mpaka pale mwanamke huyu alipokubali kuwa upande wa Saddam Hussein. Album hii ilikuja kuingia sokoni miaka minne tangu kurekodiwa baada ya Kalayi boing (1993) na Les Anges Adorables (1994) kuwa zimetoka. View attachment 556606

Mwaka 1993 kundi likarekodi album ya Kalayi Boeing huko Ulaya na kutoka mwaka huo huo, muda mfupi baada ya album hii kutoka, Manda Chante (anayesika sana katika wimbo wa kalayi Boieng) akajitoa na kujiunga Wenge El Paris (Rejea maelezo ya aya hapo juu). Alijitoa baada ya viongozi wa kundi kutoonyesha ushirikiano wowote alipougua ugonjwa wa ajabu wa ngozi (matete kuwanga). Alimshutumu sana Werrason kushindwa kumlipa hela kipindi alichokuwa anaumwa. Manda Chante miaka ya hivi karibuni amekuwa akihusisha ugonjwa huu na nguvu za giza huku shutuma kali akizipeleka kwa JB Mpiana kuwa alitaka kumuua kutokana na sauti yake manda chante kupendwa sana wakati album hii inatoka.

View attachment 556603

Baada ya kujitoa kwa Manda Chante, kundi likarejea nyumbani na kuanza kutafuta mbadala wa Manda chante. Wengi wakajitokeza kwenye majaribio ili apatikane wa kuziba pengo la Manda chante. Baaadhi watu maarufu waliojitokeza katika usaili huo ni Babia Chokoro (ni former mate group wa manda chante huko Yoka Choc), Papy Sesele “Adjani sesele”, Blaise Yombo Lumbu maarufu kama Tutu Caludji, na Aimelia Lias Miankodila ambaye alishinda kinyang’anyiro hicho na hivyo kuwa mbadala wa Manda chante. Lakini Tutu Caludji akapelekwa katika sekta ya uatalaku baada ya kuonekana pia anaweza kughani. Pia baada ya album hii ya Kalayi Boieng, Alain Makaba aliamua kubaki ulaya na kufanya makazi yake huko, hivyo Ficarré mwamba akawa mpiga gitaa la solo kiongozi, na baadaye Vincent Kasongo Mbokaliya Burkina Faso akajiunga katika kundi. Na ni kipindi hiki Ali Mbonda alijiunga ili kuziba pengo la Don Pierrot aliyekua amejitoa wakati bendi ilipofanya tour ulaya mwaka 1992.
View attachment 556614
Mwaka 1994 Kundi likarejea ulaya tena kwa ajili ya tour bila uwepo wa Tutu Caludji na Mboka liya na kurekodi album iliyofuatia ya Les Anges Adorables ambayo ni moja ya album bora kabisa za wenge Musica (Album hii ina kopi mbili yaani Version I and Version II). Baada ya album hii Papa Denewade aliwashauri viongozi wanne ambao ni waasisi (Yaani Makaba, Masela, Werrason na JB Mpiana) kila moja kutoa album yake kama solo. Hivyo Alain Makaba akawa wa kwanza kutoa album iitwayo Pile ou Face mwaka mmoja baadae yaani 1995, ambapo aliwashirikisha wanamuziki watatu tu toka Wenge, ambao ni Titina, Le Grand Chibuta Roberto Ekokota na Jb Mpiana, wengine hawakuwa member wa Wenge maana aliwashirikisha mzee Sam Mangwana, Dindo Yogo, Luciana Demingongo, Abby Suriya, Ballou Canta na King Kester Emeneya.

Mwaka 1995, Burkina Faso akawa mpiga gitaa la solo kiongozi Kinshasa (kumbuka Makaba alikuwa kaweka makazi ulaya). Mwaka huo huo bendi ikamsajili mpiga gitaa Fiston Savimpi Zamuangana (Mtoto wa Enoch Zamuangana wa Zaiko Langa langa) na muimbaji Hervé Gola Bataringe maarufu kama Ferre Chair De Poule wote kutoka kundi la Des Jeunes, na pia mpiga drummer na tumba (mbonda) aitwaye Blaise Seguin Bongongo maarufu kama Seguin Mignon akitokea Kibinda nkoyi.

Mwaka 1996 bendi ikafanya tour Marekani bila ya Alain Makaba aliyekuwa ulaya, baadae bendi ikaenda Ubeligiji na kurekodi album ya Pentagone huku Alain Makaba akishiriki kikamirifu, baada ya kurejea Kinshasa Japonais Maladi Kambuku alijiunga na Wenge akitokea Japana group. Na nikipindi hiki ndipo ubinafsi ukaanza kuonekana kati ya JB Mpiana na Werrason hasa baada ya JB mpiana na producer Simon Ndjonang “Simon Music” kuanza kurekodi album ya Feux de L'amour kama solo album ya JB Mpiana. Werrason hakukubaliana na wazo la JB Mpiana sababu ikiwa ni tayari walishaanza maandalizi ya album mpya ya kundi na kuipromote album ya Pentagone iliyokuwa tayari sokoni, lakini mwisho wa siku album ya Feux de L'amour ikatoka mwishoni kabisa wa mwaka 1996. Tofauti na mwenzake Makaba aliyetumia wanamuziki watatu tu wa Wenge, JB Mpiana alitumia takribani bendi nzima huku mwanamuziki mwalikwa akiwa ni mmoja tu tena mshauri wake Papa Wemba ambaye naye aliishiriki wimbo mmoja tu uitwao Cavalier Solitaire.
View attachment 556609

Sintofahamu iliendelea na kuigawa bendi katika makundi mawili yaani kundi la Werrason (akiwa supported na Masela na Adolph Dominguez) na kundi la JB Mpiana ambalo kwa sehemu kubwa ni wanamuziki wengi wa Wenge (kama Blaise Bula, Makaba, Alain Mpela, Aimelia, Ficcare Mwamba, n.k). Hatimaye disemba 1997 rasmi kundi likagawanyika na kuwa vipande viwili (Yaani Wenge Musica Maison Mere na Wenge BCBG) View attachment 556617View attachment 556618
Moja ya vituko vilivyotokea wakati bendi ipo katika mgogoro ni hiki cha 1997 huko Kinshasa ndani ya Grand Kin Hotel ambapo kulifanyika concert maalumu ya kuitambulisha album ya Faux de L'Amour ambayo hakuna mpenzi wa muziki hasa wa wenge ndani ya congo ataisahau maana concert hiyo ilikuja kubatizwa kama “concert de la separation” ambapo yalitokea majibishano makali baina ya Werrason na Blaise Bula mbele ya Papa Wemba ambae alikuja hapo kama mualikwa, Kiufupi tu ni kwamba Baise Bula na Werrason siku hiyo walitukanana sana, Blaise Bula akamwambia Werrason maneno hayo “rafiki yangu kila siku unaota uwe kama mimi,uwe kama Jb,uwe kama Makaba,hizo ni ndoto kaka yangu” mwisho wa kunukuu.

(KUHUSU SABABU ZA MGOGORO HUU ULIOIGAWA WENGE MUSICA FUATILIA LINK HIZI HAPA CHINI).

SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu ya I) (sehemu ya kwanza mpaka ya nane)

1. Album Bouger Bouger (1988)

1. Bakolo budget (JB Mpiana)
2. Fisol (Alain Makaba
3. La fille du roi (JB Mpiana)
4. Mulolo (JB Mpiana)

2. Album Kin E Bouge (1991)

1. Eve Sukali (Blaise-Bula
2. Kaskin (Werrason)
3. Kin E Bougé (J.B. M'Piana)
4. Ngoma Maguy (Roberto Ekokota)
5. Princesse Pathy (Alain Makaba)

3. Album Kalayi Boeing (1993)
1. C'est trop tard Djenga (Alain Makaba)
2. Cresois (Didier Masela)
3. Danico (JB Mpiana)
4. Jessy couchou de london (Blaise Bula)
5. Kala Yi Boeing (Werrason)
6. Mon ami coboss (JB Mpiana)
7. Voyage Mboso (Adolphe Dominguez)

4. Album ya Les Anges Adorable (1994)
a) Version I

1. Douglas Ilumbe (Alain Makaba)
2. Hi Ho Ha New Image (JB Mpiana)
3. La tempete du désert (Didier Massela)
4. Lavie (Adolphe Dominguez)
5. Surprise Kapangala(Werrason)
6. Tuna Tina Jack KitshindJa (Alain Makaba)

b) Version II

7. Capitaine de Benelux (JB Mpiana)
8. Kama (Titina Mbwinga 'el capone)
9. Masampu (Blaise Bula)
10. Promesse bouboule (Alain Mpela)
11. Sourires Des Vendeurs (Werrason)
12. Willy muntu (Didier Massela)

5. Album Pleins Feux (1995)

1. Ambiance instrument
2. Ave maria ( Blaise Bula)
3. Dady bitodi (Djolina)
4. Djino (Werrason)
5. La vie
6. Nazareth
7. Tchacho mbala

6. Album Pentagone (1996)

1. Pentagone (Roberto Wunda Ekokota)
2. Coco Madimba( Werrason)
3. Dizo izo (Alan Prince Makaba)
4. Djojo Ngonda (Fi Carre Mwamba)
5. Etepé Buengoi (Didier Massela)
6. Filandu (Blaise Bula)
7. Héritier Itele (Werrason)
8. No comment Shengen (J.B Mpiana)
9. Roco Martini (Adolphe Dominguez
10. Daddet (Autant)(Didier Massela)
11. Cometes de L'an 2000 (Patient Kusangila)

Waasisi
Didier Masela; 1981-1997 (gitaa la besi/ kiongozi, Muasisi mkuu)
Werrason Ngiama Makanda "Nkoyi de la forêt" 1981-1997 (kiongozi wa fedha, muasisi mwandamizi, mwimbaji)
Aimé Bwanga 1981-1986 (gitaa la besi, muasisi mwandamizi)
Alain Mwanga "Docteur Zing" 1981-1986 (gitaa la solo, na mi-solo),(muasisi mwandamizi)
Jean-Belis Luvutula 1981-1987 (Muasisi mwandamizi

Waimbaji
JB Mpiana "Mukulumpa" 1981-1997 (Raisi wa kundi);
Machiro Kifaya, 1981-1982;
Dede Masolo "Deno Star", 1981-1986 ;
Anibo Panzu, 1981-1986 ;
Blaise Bula Monga "Ingénieur Celebu", 1981-1997 (Chef d'Orchestre wa kwanza, kiongozi);
Adolphe Dominguez Ebodja 1981-1997 (kiongozi na pia kama mnenguaje);
Bienvenue Wes Koka 1982-1985;
Ricoco Bulambemba "le fils de Mbulamatari", 1986-1989;
Alain Mpelasi Tshwakulenda, 1986-1997 ;
Marie Paul Kambulu "Atshisa Bélési", 1987-1991;
Manda Chante, 1987-1993;
Aimélia Lias Demingongo, 1993-1997;
Ferre Gola, 1995-1997.

Wapiga gitaa na kinanda
Alain "Prince" Mabaka 1981-1997 (gitaa la solo, mi-solo na besi, kinanda, tumba, kiongozi, arranger na Artistic Director);
Christian Zitu 1981-1985 (gitaa la rhythm);
Djolina Mandudila 1985-1992 (gitaa la rhythm);
Kandimbo Eddy 1986-1989 (gitaa la besi);
Blaise Kombo 1986-1990 (Alifariki Julai 1990) (gitaa la mi-solo);
Alain Mwepu 1988-1993 (gitaa la solo na mi-solo);
Delo Bass 1989-1990 (gitaa la besi);
Patient Kusangila Lutu
1989-1997 (gitaa la solo na rhythm);
Aridjana Solo 1984-1990 (gitaa la mi-solo);
Collegien Zola 1988-1992 (gitaa la rhythm);
Christian Mwepu Mabanga 1988-1997 (gitaa la besi);
Master Ficarré Mwamba 1991-1997 (gitaa la solo na mi-solo);
Kalala desired "Syntha-syntha"1991-1993 (kinanda),;
Burkina Faso Mbokaliya 1993-1997,(gitaa la solo na mi-solo);
Japanese Kambuku Maladi 1996-1997. (Gitaa la solo, mi-solo na besi);
Theo Bidens Kiavuanga 1996-1997 (kinanda);
Son Zamuangana Savimpi 1996-1997 (gitaa la rhythm);

Ngoma na Tumba (mbonda)

Ladin Montana
1981-1987 (ngoma);
Evo Nsiona Adiataki 1981-1988 (ngoma);
Maradona Lontomba 1981-1990 (ngoma);
Pipo la Musica (ngoma) 1987-1989;
Titina Mbwinga "Al Capone" 1988-1997 (ngoma);
Don Pierrot Mbonda1988-1993 (ngoma / mbonda);
Ali Mbonda 1993-1997 (mbonda);
Seguin Mignon Bongongo 1996-1997 (ngoma / mbonda).

Atalaku
Kennedy Mbala"na ba Mputu",1988-1989;
Full King, 1986-1993;
Roberto Wunda Ekokota, 1988-1997;
Tutu Caludji, 1993-1997.

Wanenguaji
Mama Rosa 1990 to 1991
Nana Boanga 1993-1996;
Carine Evoloko 1993-1995; ''
Mkuu nimeona jina lako nimewakumbuka extra muzic

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom