Ijue tofauti kubwa kati ya Wanamuziki wa Kongo DR na wa Kitanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,216
Wanamuziki wa Congo DR
  • Wamesomea Muziki
  • Wanapiga Vyombo zaidi ya moja
  • Mazoezi yao ni ya Masaa nane ( 8 ) bila ya Kupumzika
  • Kabla ya kuanza kutumbuiza hufanya testing ya Saa 1 hadi Masaa 2
  • Wale wanaowafagilia katika Nyimbo huzilipa Bendi kati ya USD 100 hadi USD 1000
  • Magitaa ya Solo ( Lead Guitars ) huwa ni mawili ili kuufanya Mziki kuwa mzito
  • Wanaheshimu sana ratiba na hawapendi kuwaudhi Wahudhuriaji
  • Wanafanya sana Mazoezi na pia wanapumzika ( kulala ) muda wa kutosha
  • Wanakula Vyakula vyenye kuwajenga Kimwili na vinavyotengeneza Sauti zao vizuri
  • Hawaendekezi Ngono baina yao kwa wao ( Wanamuziki )
  • Mpangilio wao Nyimbo watakazopiga hupendekezwa na Wahudhuriaji
Wanamuziki wa Tanzania
  • Wanabahatisha tu na hawana hata a,b,c's za Muziki
  • Wengi wanapiga tu Chombo kimoja na huking'ang'ania hicho hicho hadi akistaafu Mziki
  • Mazoezi yao ni Masaa mawili ( 2 ) huku wakiwa wanapumzika pumzika
  • Kabla ya kuanza kutumbuiza hufanya testing ya kati ya dakika 25 hadi 35 tu
  • Wale wanaowafagilia katika nyimbo huwalipa Wanamuziki Pombe au Mademu
  • Gitaa la Solo ( Lead Guitar ) huwa ni moja tu kupelekea Muziki kuwa mwepesi
  • Hawaheshimu ratiba wanaweza kupanda Jukwaani Saa 4 usiku na kumaliza Show Saa 5 na nusu usiku huo huo na wala wasijali Kitu.
  • Mazoezi yao huyafanyia Kitandani Guest House / Lodge na hawapumzishi miili yao
  • Wanajilia lia tu hovyo Mivyakula ndiyo maana wengi wao Sauti zao hubadilika mara kwa mara na kuzidi tu kuwa mbaya
  • Ufanyaji Ngono baina yao kwa wao huwa ni kama Ibada ya kila siku.
  • Mpangilio wa Nyimbo watakazopiga huchaguliwa na wao wenyewe ( Wanamuziki )
Tuwaachieni tu Muziki Wakongo ( Wazairwaa / Bandeko Nangai ) na sisi Watanzania tubaki tu Kutekana, Kurogana na kufanyiana Fitna.

Siku yoyote ile ijayo endapo utasikia kuwa kuna Bendi au Mwanamuziki yoyote kutoka Congo / Kongo DR inakuja / anakuja kutumbuiza nchini Tanzania nakusihi usipoteze muda wako kuwaza bali wahi kakate tiketi yako na uwahi ukale zake ' Misebene ' na ' Mirhumba ' ya hatari kiasi kwamba hutojutia kulipia Kiingilio chako.

Wanamuziki wa Bendi za Muziki wa Dansi Tanzania hebu badilikeni haraka sana vinginevyo kila siku mtakuwa mnatulaumu Watanzania kuwa tunawapenda sana akina Jean Bedele Tshituka Mpiana na Wenge Musica BCBG Band yake, Charles Antoine Koffi Olomide na Quarter Latin Band yake, Ngiama Makanda Werrason na Wenge Musica Maison Mere yake na Ibambi Ikombi ( Roga Roga ) na Extra Musica Zangul Band yake bila kuwasahau akina Fally Ipupa ' Dicaprio ' na Ferre Gola ' Fetie ' na kuwadharau au kutowapeni ' ushirikiano ' nyie Bendi za Miziki ya Dansi za Kibongo.
 
Mambo mengine si kweli hata kidogo - mbona Franco kwa mfano alikuwa hajui kabisa kusoma note za musiki - lakini alikuwa gwiji wa mziki. Vile vile si kweli kusema wanamziki wa Tanzania hawako serious na tasnia ya mziki ingawa kuna ukweli kidogo linapokuja suala la wanamsikizi wa kizazi kipya ambao wanategemea sana music synthesizers kuliko kutumia vyombo vya musiki, hapo ndipo wamenoa sana labda wabadirike.

Tanzania iliwahi kuwa na bendi za kuotea mbali hata ukisikiliza nyimbo za miziki yao unakubali kwamba walikuwa zaidi-chukulia Bendi za zamani kama:NUTA/JUWATA,KILWA,JAMUHURI, TABORA, SAFARI TRIPPERS, DAR JAZZ, ATOMIC, MAGEREZA, VIJANA, MORO JAZZ, CUBAN MALIMBA, SIKINDE, MARA, AFROSA nk hivi sasa bendi nyingi kati ya hizo zimekufa na hilo limewatokea hata bendi za Congo, nyingi hazipo tena hilo ni jambo la kawaida - mifano niliyo eleza hapa inaonyesha kwamba kumbe Watanzania wakihamua kufanya kitu kwa nia moja uwezo huo wanao sana.
 
anamzungumzia hiki kizazi kipya sio hao uliowataja
 
Back
Top Bottom