wanakunywa majivu kukinga ukimwi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
BAADHI ya wakazi wa Manispaa wametakiwa kuacha imani potofu ya kunywa majivu kabla ya kujamiina kwa madai kuwa kwa kufanya hivyo ni kujikinga na
maambukizi mapya.

Mratibu wa Ukimwi Shinyanga, Dkt. Charles Mashenene amewataka wananchi wa Kata ya Ndala, Manispaa ya Shinyanga kuachana na imani hiyo potofu kuwa wakinywa majivu hawawezi kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuwa huo ni upotoshaji mkubwa na unaongeza kasi ya maambukizi.

Dkt. Mashenene alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Shinyanga Foundation Fund (SFF) linalojihusisha na masuala ya ukimwi chini ya ufadhiri wa Shirika la Rapid Funding Envelop la jijini Dar es Salaam.

Akitoa mada iliyohusu 'ukweli kuhusu ukimwi' kwenye mkutano wa hadhara ulifanyika viwanja vya viwandani kata ya Ndala mjini hapa na kuhudhuriwa na umati wa wananchi ambapo aliwaeleza umuhimu wa kubadili tabia ili kupunguza kasi ya maambukizi ya vvu pamoja na kupima kwa hiari afya zao.

Kwa upande wa mratibu wa ukimwi manispaa ya Shinyanga Rhobi Gwesso alidai kuwa wananchi kutowanyanyapaa waathirika wa ukimwi na badala yake washirikiane nao katika shughuli za maendelo na kwamba kuugua ukimwi siyo mwisho wa maisha.

Kwa upande wake meneja wa shirika hilo, Bw. Paul Sangija alisema shirika lake limeshaanza kubaini makundi mbalimbali katika jamii yanayojihusisha na biashara ya ngono wakiwemo wanaume sita wanaojihusisha na biashara ya ngono kinyume na maumbile; na wanawake 150 wanaofanyanya biashara ya ngono pamoja na mamalishe wenye uhusiano wa kimapenzi na wateja wao kwa lengo kuwa karibu na watu 1,050.

Alisema kuwa tayari shirika hilo limeanza kujenga vibanda 60 vya maduka
vitakavyotumiwa na makundi hayo ambavyo vitagharimu sh. milioni 300 kupitia kwa wafadhili wao Rapid Funding Envelop.
 
bado kuna imani potofu nyingi sana ktk jamii kuhusu ukimwi na maambukizi ya VVU ,nafikiri hili liwe jukumu letu sote kama jamii kutoa elimu fasaha juu ya gonjwa hili na jinsi ya kujikinga, kuna jamii zilizokuwa zikiamini muathirika akilala na mtoto mchanga/mdogo anakuwa cured hii ni hatari
 

Majivu na ukimwi wapi na wapi? Hakuna mantiki licha ya ukweli hakuna chemically known substance kwenye hayo majivu. Maana haya majivu tumekula kupitia magadi kwa maisha yetu yote. Tusipoangalia taifa hili litaangamia kwa ujinga huu wa KIENYEJI.
 
Back
Top Bottom