Wanakijiji watimua Mwalimu Mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanakijiji watimua Mwalimu Mkuu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 27, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  UONGOZI wa kijiji cha Bangata, Arumeru mkoani hapa ukishirikiana na wakazi wa kijiji hicho, umevamia shule ya msingi Bangata na kumtimua Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ephraimu Loi, kwa madai ya ubadhirifu wa fedha.

  Mbali ya madai hayo ya kufuja fedha, uongozi huo pamoja na wananchi wa kijiji hicho, unautuhumu uongozi wa shule hiyo kwa kuchangisha fedha wanafunzi wa shule hiyo bila kushirikisha walimu na wazazi.

  Pia Loi anadaiwa kufunga ofisi ya kijiji hicho hali iliyosababisha uongozi wa kijiji kufanyia kazi nje na kutumbukiza chooni sweta za wanafunzi zaidi ya 100 kwa madai kuwa si sare ya shule.

  Uongozi wa kijiji ulichukua uamuzi huo jana baada ya kikao cha uongozi huo na wananchi ambao ulijadili tabia ya mwalimu huyo na kutolewa kauli kuwa wamechoshwa naye kutokana na vitendo vyake.

  Katika mkutano huo, mwalimu huyo alidaiwa kukataa kushirikiana na uongozi wa kijiji hicho kwa madai kuwa hautambui ikiwa ni pmoja na kutoitisha mkutano na wazazi tangu ahamie shule hiyo mwaka 2003.

  Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika chini ya mti nje ya ofisi ya kijiji hicho, Mwenyekiti wa Kijiji, Samweli Ndosi alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kumvumilia kwa muda mrefu na kwamba amekuwa kero katika kijiji hicho.

  Ndosi alisema kitendo cha mwalimu huyo kuingia darasani na kuwavua watoto wote sweta zisizo sare za shule na kutupa chooni, kimewasikitisha sana wazazi na ndugu wa watoto hao.

  Baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji, Loi Simoni, Julius Lukumay, Obeid Songoya na Meshack Mollel, walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akila rushwa kwa kuwaingiza shule wanafunzi wengi wanaorudia elimu ya msingi na kusababisha wanafunzi wa kijiji hicho kukosa nafasi shuleni hapo.

  Mwalimu Loi alikiri kutoshirikisha viongozi wa kijiji hicho katika uamuzi wa utendaji wa shule hiyo, akidai kuwa Mwenyekiji wa Kijiji anatoka chama cha upinzani.

  “Ni kweli nimeamriwa niondoke kwa madai kuwa nimekuwa nikichangisha fedha bila kushirikisha wazazi nami pia nimeona ni bora niondoke, kwani inavyoonekana wananchi na viongozi wao wananichukia na nikiendelea kukaa nitakuja kuuawa bure,” alisema Mwalimu huyo.
   
Loading...